Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KITENGO cha Sayansi ya Jamii[Forensic Bureau]maelezo yake yametia fora katika kikao kazi kati ya Waandishi wa habari na Vigogo wa Polisi kutoka Vitengo mbali mbali vya jeshi hilo.
Katika Kikao hicho kilichofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa JKT Bwalo la Umwemam Vigogo wa Polisi kutoka Vitengo vya Dawati la Jinsi, Usalama barabarani, kitengo cha Afya na Kitengo cha Sayansi ya Jamii Mkoa kila mmoja alitoa maelezo ya kitengo chake kwa Waandishi wa habari.
Huku maelezo ya kitengo cha Sayansi ya Jamii yaliyowasilishwa vyema na Mtaalamu wa kitango hicho Afande CPL Alphonce Kimaro yakiwavutia Waandishi wengi akiwemo Mwandishi wa Mtandao huu.
Hii ni kwa sababu ya mambo mapya ya kitengo hicho tofauti na yale yaliyowasirishwa na Vigogo wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia, Usalama barabara na Afya, ambapo mengi ni yale yale ya siku zote.
Akiwa mbele ya kamera za Waandishi wa habari Afande Kimaro alisema kitendo hicho kina vifaa vya kisasa vya kisayansi vinavyoweza kunasa vinasaba vya muhalifu aliyefanya uhalifu eneo la tukio. “ Kwa mfano mwizi kavunja vioovya gari haiba vitu vya dhamani vilivyondani ya gari hilo, tukifika eneo la tukio kifaa hicho kitanasa vinasaba vya mwizi huyo. Hivyo kupitia nyinyi Waandishi tunaomba kuwataalifu wananchi yanapotokea matuki kama hayo watoe taarifa Polisi na wasisogee eneo la tukio.
Kwani walisoge tukifika eneo la tukio na kifaa hicho kinanasa vinasaba vya watu wengi hivyo tutashinda kubaini aliyefanya uhalifu”alisema Afande Kimaro na kuongeza.
“ lkumbukwe kwenye tukio la Mlipuko wa Lori la Mafuta Pale Msamvu watu wengi waliungua kiasi cha kutotambulika lakini kitendo chetu kupitia vifaa hivyo vya Sayansi ya Jamii tulichukua sampuli za marehmu na zile za ndugu wa marehemu na kuwatambua marehemu na kwamba baada ya utambuzi huo ndugu walikabidhi marehemu wao na kwenda kuwazika”alisema Mtaalamu huyo.
Baada ya kikao hicho Mwandishi wa habari hizi alifanya mahojiano Maalum na Afande Kimaro ambapo alipoulizwa kifaa hicho kisayansi kinauwezo wa kunasa vinasaba hivyo baada ya muda gani? Afande huyo alijibu.
“ Kifaa hicho kina uwezo wa kunasa tukio baada ya masaa 24 toka tukio kufanyika hivyo nawasihi wananchi unapotoea uhalifu kwenye maeneo yao watoe taarifa mapema kwa jeshi la Polisi”alisema Afande Kimaro.
Baadae tutakamirisha taarifa hizi kwa Polisi kujibu swali la Mwandishi wa habari hizi alipouliza kwa nini Vituo vidogo vya Polisi vinafungwa Majira ya saa 12 jioni ili hali uzoefu unaonyesha uhalifu mwingi hufanyika nyakati za usiku? endelea kuwa jirani na mtandao huu muda wote kusikia walichojibu Polisi .
Pichani Afande Kimaro aliyevalia kiraia akiwa na Vigogo wengine wa Polisi kati ni kigogo wa Dawati la Jinsia na kulia ni Afande Emmanuel kutoka kitengo la Usalama barabarani.
Mtandao huu unalipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa kazi nzuri wanazofanya kwenye Vitengo vyote.
No comments:
Post a Comment