Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 9, 2022

KIFO CHA MTANGAJI SUA TV ASKOFU ASEMA JIMBO LIMEPOTEZA MTU MUHIMU. MTOTO WA MAREHEMU ALIZA WATU KANISANI.


                              Marehemu Cathe enzi za uhai wake

...Askofu Staafu Teresphor Mkude akitoe heshima zake za mwili
...Kaimu Askofu wa jimbo la Morogoro Salvatus Kwembe anaye akitoa heshima zake za mwisho

Machapa 3 Waandishi wa habari wakongwe mkoa wa Morogoro Ratifa Ganzel [wa mbele] anayepiga nkazi magazeti ya uhuru ambaye pia ni diwani wa viti maalumu kwa leseni ya CCM. wa kati ni Lililia Lucas Kasenene anayepiga kazi gazeti la Mwananchi ambaye pia ni katibu Mkuu wa Cha Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro na wa mwisho nii ldda Mushu anayepiga mzigo ITV Radio One ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro






...Wana kwaya wakimwimbia mwana kwaya mwenzao wimbo maarumu hata hivyo baadhi ya wana kwaya waliangua vilio na shindwa kuendelea kuimba wimbo huyo


Mtoto wa Marehemu Michael Edward akiangalia kwa uchungu Akofu akitoa heshima  za mwisho kwenye jenela la mpendwa mama yake





Kaimu Mkuu wa Chuo cha SUA Akitoa wadhifu wa marehemu
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari akizungumza
                   Mwenyekiti wa kaya akitoa salam za kwaya
.            ...Askofu Mstaafu akitoa maelezo yake juu ya marehemu
                   ...Mama Mzazi  wa marehemu Bi Chistina Tinde
Mama wa marehemu akiangua kilio baada ya kuguswa na maneno ya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari
...Watanagzaji wa SUA Media Josephine Maharangu kushoto] na Farida Mkongwe wakiangua vilio baada ya kumshuhduia mtoto wa marehemu akilia wakati mwili wa mama yake ukiingizwa kwenye gari

...Mtoto wa marehemu akiangua kilio huku akiangalia kw amajonzi mwili wa mpendwa mama yake ukitolewa kanisani na kuingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kamaha

                              ....Mwili ukitolewa kanisania
....Safari ya kuelekea Kahama Shinyanga ikianza jana jioni

...inauma sana wana kwaya wakiwapungia  ikiwa ni ishara ya kuwaaga watu walikuwa kwenye gari hilo

                


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

KAIMU Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Padre Salvanus Kwembe amesema kifo cha Mtangazaji mahiri wa SUA Media Catherine Mangula Ogesa[45]ni pigo kumbwa ndani ya jimbo hilo.

Kaimu Askofu huyo ambaye pia ni Padre kiongozi wa kanisa kuu la Mt Patrick Jimbo la Morogoro aliyasema hayo kwenye lbada ya kumuombea marehemu huyo iliyofanyika kanisa la Bikira Maria Mama wa Kanisa Parokia ya Kigurunyembe.

Kwa upande wake Askofu Mstaa wa Jimbo hilo  Teresphor Mkude aliyeongoza lbada hiyo akishirikiana na mapadre 3 alisema anamfahamu vizuri Catherine kwa utumishi wake  kwenye jimbo hilo  hasa uimbaji wake wa kwaya ya Demi Aziz anapoongoza ‘Kwaya Master.’

 

 Naye Naibu wa Makamo Mkuu wa Chuo Cha SUA Utawala na fedha Profesa Amandus Muharwa,akizungumza Kwa  niaba ya wanafamilia wote wa Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine ‘SUA’ alipokuwa akifanya kazi Marehemu,

 

  alisema Chuo kimepoteza mtu muhimu kwenye kitengo cha habari na mawasiliano.

 

”Tumepoteza mtu muhimu sana mbali ya kuwa mtangazaji  kwenye vituo vyetu Radio na Televishen  pia alikuwa katibu wa Chama cha Wafanyakazi Kwenye chuo chetu.

“Marehemu alianza kupatiwa matibabu kwenye hospital yetu ya SUA toka mwezi uliopita akisumbuliwa na ugonjwa wa lni”alisema Profesa huyo.

 

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ Nickson Mkilanya alisema hadi marehemu anafariki dunia alikuwa Mwanachama hai na mwadilifu wa chama hicho.

 

”Kipekee nimemfahamu Cathe miaka kama 10 iliyopita tulisoma wote Digirii Chuo Kikuu Huria  Tanzania ni Mwanamke mpambani mwenye hofu ya Mungu asiye kuwa na Makuu”alisema Mkilanya.

Maneno hayo yalimchoma Mama mzazi  wa marehemu Bi mkumbwa Cristina Tinde ambaye alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi huku akijifuta na upande wa khanga.

 

 Mwenyekiti wa Kwaya ya Demi Aziz aliyokuwa kiitumikia Marehemu Cathe Bw Charles Kaumbe alisema Kwaya imepotea mtu  Muhimu kwani enzi za uhai wake alikuwa katibu wa Kwaya hiyo kabla ya kuandika barua hivi karibu ya kujiuhudri wadhifa huyo kwa sababu alizoahinisha za ugonjwa.

 

Katika hatua nyingine mwisho wa lbada hiyo Kwaya hiyo iliimba wimbo maarumu kwa marehemu ambapo wimbo huo ulijaa mahudhui yenye majonzi uliliza  watu wengi wakiwemo baadhi ya wana kwaya kwalioshindwa  kuimba na kujikuta wakiketi chini na kuangua vilio.

 

 Aidha Wakati jeneza lililobeba mwili wa Cathe likiingizwa kwenye basi ndogo aina ya Coaster tayari kwa safari ya kwenda kupunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele nyumbani kwao Kahama mkoani Shinyanga.

 

 Mtoto pekee wa marehemu Michael Edward aliangua kilio akimlilia mpendwa Mama wake  hali hiyo ilipelekea watangaji wa SUA Media Josephine Malangu ‘Maarufu Josephine Andenyenye’ na Farida Mkongwe nao kuangua vilio kwa sauti walipomshuhudia mtoto huyo.

Kama kawaida kwenye maswali mengi Mwandishi wa habari hizi hutafuta majibu, baadhi ya watu kanisani hapo waliulizana swali lililokosa majibu kwamba Marehemu Cathe alikuwa akiimba kwaya kanisa kuu la Mt Patrick lililopo Mjini iweje maiti yake isaliwe kwenye kanisa hili la Parokia ya Kigurunyembe.?

 

 

Mara baada ya kutamatika kwa  lbada hiyo  Mtandao huu ulimuliza swali hilo mmoja wa viongozi wa kanisa kuu la Mt Patrick Katekista Banzi ambaye alisema.

”Ni kweli Marehemu alikuwa akiimba kwaya kwenye kanisa letu hivi karibuni amefanikiwa kuhamia kwenye nyumba yake alijojenga hapo juu jirani na Chuo cha Uwalimu Kigurunyembe toka alivyohamia kwenye nyumba yake alikuwa akisali hapa ndio maana  lbada hii imefanyika hapa tuko pamoja shekidele”alisema Kiongozi huyo.

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...