Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, July 8, 2022

TANZIA. MTANGAZAJI MAARUFU WA LUNINGA AFARIKI DUNIA.


                    Marehemu Catherine Ogesa enzi za Uhai wake

 

                                             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

MTANGAZAJI Maarufu wa SUA Media inayomilikiwa na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine’SUA’ cha Mkoani hapa,Catherine Mangula Ogesa, amefariki dunia jana kwenye hospital ya SUA alipokuwa akipatiwa matibabu kwa wiki kadhaa.

 

Mwanahabari huyo Msomi wa revo ya Digrii ya Uandishi wa habari aliyoipata Chuo Kikuu Huria Tanzania kifo chake kimeumia mioyo ya watu wengi kufuatia tabia yake vyema kwa jamii ya kada zote.

 

 ,Pia ‘Cathe’ambaye pia ni Mwanachama hai wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro [Morogoro Press Club] amekuwa kioo kizuri cha Jamii katika tasnia hiyo muhimu nchini.

 

 

Nakumbuka usomaji wake mzuri wa Taarifa za habari katika Luninga ya SUA TV, ulikuwa kivuto kufuatia muonekano wake wa uhalisia  alioumbwa nao Mungu na kamwe hujawahi kujibadirisha rangi wala nywele.

 

Alibaki na rangi yake halisi ‘Nature Color’ Metarick Color  kwa minajili hiyo alikuwa kivutio kwa  Watazamaji wengi wa SUA Tv akiwemo Mwandishi wa habari hizi.

 

 

Binafsi tangu namfahamu zaidi ya miaka 10  sijawahi kumuona umejibadilisha rangi wala nywele mpaka unaondoka ulimwenguni  jana majira ya saa 7 mchana  siku zote muonekana wake ulikuwa halisi kama anavyoonekana  kwenye Picha hii ya enzi za uhai wake.

 

  Kamwe sijakuona ukijipodoa kupitiliza kwa maana ya kubadiri langi yako sambamba na kuvaa nywele za bandia [Mawigi].

 

 

Licha ya Usomi wako na umaarufu wako wa utangazaji kwenye Lunginga hukujimwambavai[Kujivuna] badala yake ulizidi kijishusha na kujiweka wa kawaida kwa watu wote.

 

Lkumbukwe baadhi ya watangazaji hutumia fursa hiyo kujipodoa kwa lengo la kuuza sura kwenye Luninga lakini kwa ‘Cathe’ ilikuwa tofauti  uliuza sura yako halisia aliokuumba nayo Muumba wako.

 

 Hii imetokana na hofu kumbwa ya Mungu uliyojaliwa kuwa nayo nadhibitisha hilo kwa ushahidi kwamba licha ya usomi wako na Umaarufu wako lakini ulimsifu Mungu kwa kuimba kwaya mbalimbali ndani ya kanisa katolik Jimbo la Morogoro.

” Umezimika kama Mshumaa ‘Cathe’Nenda salama Mwanahabari Mwenzangu, Mwanachama Mwenzangu wa MOROPC.

  Tutaonana badae sisi, tumekupenda lakini Mungu amekupenda zaidi, Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe wote tuseme Amen”

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...