Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 11, 2022

GEMU YA TIBU KIBWANA NA TIMU JOB YAVUNJA REKODI, UWANJA WAFUNGWA BAADA YA MASHABIKI KUHARIBU MIUNDO MBINU WAKIGOMBEA KUINGIA UWANJANI.

Beki wa timu  Kibwana Nickson Kibabage anayekipiga timu ya Ligi Kuu ya Halmashauri ya Kinondoni'KMC' akimthibiti Winga hatari wa timu Job Shiza Kichuta abayekipiha Namungo ya Lindi ambapo kunatetesi zinazoda Kichuya huenda akarejea Simba Msimu ujao.

 Mastaa hao wote wametokia kituo cha kukuza na kuibua vipaji cha Moro Kids




Bondia Twaha Kiduku aliyeitumikia timu Kibwana akiteja jambo na Winga wa Mtibwa Sugar Salum Kihimbwa Chuji' a.k.a Ras wa Manungu.
Super Sub  Twaha Kiduku akimsikiliza Kocha wakati wa mapunziko
              ...Kiduku akiteta jambo na mchezaji mwenzake
Baada ya gemu kutamatika kundi la mashabiki lilimvamia Stamini na kugombea kupiga naye picha kwa kutumia katmera za simu zao


             Mwenyetimu Kibwana Shomary akimiliki Mpira

Beki kisiki wa timu ya Mbeya City Hamad Waziri'Kuku' akimiliki Mpira huku kipa wake Abuutwar Mshery akijianda kutoa msaada


Goooooo. Kiapa Mshery akiuangalia mpira uliopigw aumbali wa takribani mita 26 uliopigwa na Simon Msuvo na kujaa wavuni akiiandikia timu yake ya Kibwana bao 2 kabla Temsi Evansi kupachika la 3
            Kipa wa Yanga timu Job Abuutwarib Mshery

Kibwana Shomari akiwahamashija wenzake kulind aushindi wao wakati wa mapunziko
Simon Msuva akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mapunziko

Mshambuliaji wa timu Job Suma akijiandaa kufumua shuti huku beki wa timu Kibwana Zawadi 'Gift' Mauya akijiandaa kumthibiti






 Dickson JonJezi no 5 kati na Abuutwarib Mshery kushoto wakizunguka uwanja wa Saba saba kuomba pesa kwa mashabiki


 

                                             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 

 MCHEZO wa hisani ya kuchangia watu wenye uhitaji wakiwemo wajawazito wa hospital  ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyoandaliwa na wachezaji nyota wa Yanga Wazaliwa wa Morogoro Kibwana Shomary na Dickson Job, imevunja rekodi kwa kuingia mashabiki wengi kwenye uwanja wa Saba saba ulipo Mkoani hapa.

 

Hata hivyo taarifa zinadai Umati huo uliofulika uwanjani hapo uliharibu baadhi ya Miundombinu ua uwanja huo likiwemo geti pekee la kuingia na kutoka kwenye uwanja huo walioikuw awakigombea kuingia uwanjani hapo kuwashuhudia mastaa hao.

 

Juzi kituo kimoja cha redio Mkoani Morogoro kiriripoti kwamba Uongozi wa Uwanja huo unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi wametangaza kuufunga kwa siku zisizojulikana.

 

Baadhi ya mashabiki  waliohojiwa na Mtandao huu waliwashauri wandaji wa mchezo huo Kibwana na Job mwakani panapo majaliwa waupeleke uwanja Mkubwa wa Jamhuri kufuatia ukubwa wa mchezo wenyewe.

 

Kufuatia hali hiyo michezo ya Ndondo Cup iliyokuwa ikiendelea kwenye uwanja huo haikufanyika, hata hivyo kituo hicho kiliendelea kudai kwamba huenda michuano hiyo ya ‘The Gunness Ndondo Cup’ ikaendelea leo Jumatatu kama  mafundi wamefanikiwa kukarabati miundombinu hiyo.

 

Ukiondoa kasoro hiyo gemu hiyo ilifana kufuatia mastaa kibao wakiwemo Viongozi wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Abert Msando na Mh Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood juzi wameshiriki kwa vitendo kwenyea gemu hiyo kwakukipiga.

 

 

 

Katika Mchezo huo Mh Abood aliitumikia timu ya Kibwana Shomary kwa takribani dakika 15 huku Mkuu wa Wilaya Msando akiitumika timu ya Job pia kwa takribani takika 17.

 

 

 Wakati gemu hiyo ikiendelea Kibwana na Job walizunguka uwanjani wakiomba pesa kwa mashabiki.

 

 

Kama wanavyonekana Pichani Dickson Job[jezi no 5] akiwa na Kipa namba 2 wa Yanga Abuutwarib Msheri[Kushoto]wakilindwa na mabausa,baada ya kukamilisha zoezi hilo Job na Kibwana waliingia kipindi cha pili kuzitumikia timu zao hizo za Timu Kibwa na timu Job.

 

 

 

Job na Kibwana  ambao ni wazariwa na Mkoa wa Morogoro walifanya hivyo kwa lengo la kurejesha sehemu ya mafaniko yao kwa jamii ya mkoani kwao Morogoro.

 

Baada ya kutamatika kwa ligi kuu na ile  ya F.A   wanasoka hao walireja nyumbani kwa mapunzika na kuamua kuanda mchezo huo wa hisani,Uliounda  timu Kibwana na timu Job .

 

 

 Katika mchezo huo uliojaa mastaa kibao akiwemo Bondia maarufu nchini mwana Morogoro Twaha  Kassim’ Marufu Twaha Kiduku’ na Msanii  wa muziki wa kizazi Kipya Stamina ambaye pia ni Mwana Morogoro wawili hao waliingia dakika za mwisho mwisho wakitumikia timu Kibwana.

 

 

 

Katika mtanange huo uliojaza nyomi ya watu kwa kingilio cha buku 2 ulitamatika kwa timu Kibwana kuibuka na ushindi wa bao 3-0.

 

 

Mabao yawashindi yalifungwa na Simon Msuva anayekipiga soka la kuripwa nchini Morocco ambaye kwa sasa anatajwa kurejea timu yake ya zamani ya Yanga, huku bao la tatu likipachikwa na Temsi Evans anayekipiga Azam Fc.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...