Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 31, 2022

BEKI WA YANGA AFUNGUKA ALIVYOPASUANA NA MSHAMBULIAJI WA SIMBA.



 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 Beki Kisiki wa Yanga Kibwana Shomary amefunguka  alivyopasuana Vichwa na Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis.

 

 Jana Mtandao huu uliripoti habari ya wachezaji hao kupasuana na ukaahidi kumpigia simu  Mwana Morogoro, Kibwana kwa lengo la kumpa Pole na kujua maendeleo yake baada ya ajari hiyo ya Kisoka.

 

Majira ya saa 1 usiku wa jana Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia simu beki huyo wa kushoto wa Mabingwa hao watarajiwa wa Msimu huu unaoelekea Ukingoni.

  Mazungumzo yalikuwa hivi.

 

Mwandishi- Mambo Vipi?

.

 Kibwana- Hoo Safi bro Shekidele habari za Moro.

Mwandishi- Mungu ni Mwema huku tuko salama, Wana Moro walishuhudia gemu ya Yanga na Simba kupitia Luninga wakakuona Mwana Morogoro mwenzo umeshindwa kuendelea na mchezo baada ya kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji wa Simba Kibu Denis na baadae ukakimbizwa hospital je unaendelea je  na umeshatoka hospital?.  

Kibwana- Asanteni sana wana Morogoro wenzangu kwa upendo wenu kwangu kweli niligongana na Kibu nikashindwa kuendelea na mchezo kikakimbizwa hospital nashukuru Mungu nimepata matibabu kwa muda wa msaa kadhaa madaktari wakaniruhusu nikarejea kambini.

Kupitia Mtandao wa Shekidele ambao mimi ni mdau mkubwa toka nikiwa Mtibwa niwatoe hofu wana Moro na wana Yanga kwa ujumla kwamba kwa sasa naendelea Vizuri na tayari niko kambi ya timu ya Taifa, juzi na jana nimefanya mazoezi na wenzangu.

 

Mwandishi. Ok swali la Mwisho kuna Picha umekumbatiana na Kibu Denis Mkiwa hospital je alifunga safari kuja hapo hospital kukuona au naye alifika hapo kwa matibabu?

Kibwana. Kibu naye aliretwa pale hospital niliyokuwepo ambayo jina lake nimelisahau baada ya kutibiwa na kupewa muda wa kupunzika alikuja kwenye wodi yangu kuniona tukapeana Pole tukakumbatiana then akarejea kwenye wodi yake kwa kuwa mimi nilikuwa wakwanza kufika na kupata tiba niliruhusiwa kabla yake So  nikaenda kwenye wodi yake nikamuaga.

Mwandishi- Asante sana kwa ushirikiano wako

 Kibwana- Poa poa Shekidele kupitia Mtandao wako tunapata habari za nyumbani Morogoro.

Kwa sasa timu ya Yanga inawachezaji watatu ambao ni wadau wakubwa wa Mtandao wa Shekidele.

 wachezaji hao walioibuliwa Vipaji vyao na  taasisi ya Moro Kids ambao badae wakaenda Mtibwa B kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa  kisha kutimkia yanga kwa nyakati tofauti ni Kibwana Shomary,  beki wa kati Dikson Job na Kipa Abutwalib Msheri.


 

Monday, May 30, 2022

UCHANGUZI. HII IMEKAA VIZURI, SIMBA NA YANGA SI UADUI.


 


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Juzi Jumamosi Mei 28 nchini ilisimama kwa muda wa dakika 90 kupisha gemu ya watani wa Jadi kutoka eneo Moja la Kariakoo Jijini Dar es salaa.

 

 

  Timu hizo kongwe nchini ni Yanga  iliyoanzishwa Mwaka 1935 yenye Maskani yake  Makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo, huku Simba iliyoanzishwa Mwaka 1936 Maskani yake yakiwa Mtaa wenye Pilikapilika nyingi Mtaa wa Msimbazi  Kariakoo.

Wababe hao wa Soka la Tanzania Walikutana Juzi kwenye Mchezo wa nusu fainali ya Michuano ya F.A Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

 

 

Katika gemu hiyo kulitokea matukio mengi moja ya matukio hayo ni beki wa Yanga Mluguru wa Kinole Morogoro Kibwana Shomari kugongana  Vichwa na Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis aliyepewa Uraia wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Tanzania Mwaka jana.

 

 

Katika ajari hiyo ya Soka Wawili hao walipasuka Vichwa huku Kibwana akishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa nje baada ya kupata maumivu makali, nafasi yake ikachukuliwa

na Farid Mussa.

 

Kibu aliyekuwa na uhai  kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba alitibiwa kwa takribani dakika 4 akavishwa bendeji kubwa kichwani lililoficha Rasta zake akarejea uwanjani kuipigania timu yake.

 

Mara baada ya gemu hiyo kutamatika kwa Wananchi Yanga Kumua Mnyama Simba kwa kumchoma mshale 1-0,Kibu alimtafuta Kibwana kwa lengo la kujua maendeleo yake na kufanikiwa kumuona  Vyumbani.

 

  Alipomuona alimjulia hali sambamba na wawili hao kuombana msamaha kasha wakakumbatiana huku kila mmoja akiwa na bendeji la jeraha Kichwani.  

 

 

 

Kibwana Shomari Mtoto wa Morogoro aliyeibuliwa Kipaji chake na tasisi ya Moro Kids akapelekwa Mtibwa B akaonyesha kiwango kizuri akapandishwa timu ya wakubwa kabla ya kutimkia Yanga.

 

 

Kibu Denis amejiunga na Simba Msimu uliopita akitokea Mbeya City ya Jijini Mbeya.

Kibwana na Kibu wote ni wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania'Taifa Stars'

 

Baadaye leo Mtandao huu utampigia simu  Mwana Morogoro  Kibwana Shomari kwa lengo la kumpa pole  sambamba na kujua maendeleo yake baada ya kupata dhuruba hilo.

 

Saturday, May 28, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU LEO JUMAPILI MEI 29



 

YEREMIA 33-3

“Niite nami nitakuitika, name nitakuonyesha  Mambo Makubwa,Magumu usiyoyajua”Hilo ndilo neon letu la leo Jumapili ya Mei 29

Friday, May 27, 2022

KUMBUKIZI YA MIAKA 8 YA MSANII ALBERT MANGWEHA.


 


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 Mei 28 -2013 Mkali wa Muziki wa Hip Hop nchini Albert Keneth Mangweha’Ngwea’ alifariki dunia  nchini Afrika Kusini na kuzikwa wiki iliyofuata Mkoani hapa, hivyo  leo mei 28-2022 Msanii huyo ametimiza miaka 9 toka alivyoiaga dunia.

 

Famila ya Hayati Mangweha inayoishi Kihonda Mtaa wa Mazimbu Road Morogoro anafanya lbada ya kumuombea mpendwa sambamba na kudhuru kwenye kaburi la Msanii huyo lililopo nje ya kanisa Katolini Jimbo la Morogoro Parokia ya Mt Monica Kihonda.

 

  Mtandao huu leo unakamirisha matukio ya Kifo cha Msanii huyo Kipenzi cha wengi kwa tukio la Msanii mwenzake Kala Jeremiah kudhuru kwenye kaburi la Ngwea kisha kutinga nyumba na kumkabidhi Mama Tuzo Mama Mangweha.

 

 Mara baada ya  kutwaa tuzo 3 kwa mpigo  za Kili Music Award 2013 Msanii wa Miondoko ya Hip Hop nchini,Kala Jeremiah baada ya kukabidhiwa Tuzo hizo Msaani huyo alifunga safari kitoka Dar Mpaka Moro  na kudhuru kaburi la Ngwea akiwa na Tuzo hizo 3.

 

 

 

Baada ya kutoka makaburini akiwa na Mwandishi wa habari hizi alitinga nyumbani kwa Mama Mzazi wa  ‘Ngwea’ Bi Denisia Mangweha na kumkabidhi tuzo moja kama ishara ya  kutambua mchanga wa Msanii mwenzake huyo aliyetangulia mbele za haki.

 

 

Kwa uchungu Bi Mkubwa huyo mara baada ya kupokea Tuzo hizo aliangua kilio akimkumbuka Mpendwa Mtoto wake Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo lililofanyika nyumba kwa Mama huyo Mtaa wa Mazimbu Road, Mwandishi wa habari hizi alipata wasaha wa kuzungumza na Msanii huyo ambaye kwa sasa yuko kimya sana kimuziki.

 

KUMBUKIZI. AFANDE SELE SIMBA WA MOROGORO AFURAHI KUTEMBELEWA NA WATOTO WA PAPARAZI




 


Msanii Mkongwe nchini wa Muziki wa Kizazi Kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’akiwa na Tumain Dunstan Shekidele’Kulia’na Neema Dunstan Shekidele[Kushoto].

 

 Tumaini ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mwandishi wa habari hizi amesoma darasa la kwanza mpaka la 7 na Mtoto wa kwanza wa Afande Sele Tundajema’ Maarufu Tunda Katika shule ya Msingi Nguzo iliyopo jirani na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

 

 Mwendelezo wa Matukio ya kumbukizi ya Miaka 9 ya Kifo cha Msanii Albert Mangweha yataendelea kesho ambapo pia hiyo kesho Mei 28 ndio  kilele cha Kumbiziki hiyo.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...