Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 31, 2022

BEKI WA YANGA AFUNGUKA ALIVYOPASUANA NA MSHAMBULIAJI WA SIMBA.



 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 Beki Kisiki wa Yanga Kibwana Shomary amefunguka  alivyopasuana Vichwa na Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis.

 

 Jana Mtandao huu uliripoti habari ya wachezaji hao kupasuana na ukaahidi kumpigia simu  Mwana Morogoro, Kibwana kwa lengo la kumpa Pole na kujua maendeleo yake baada ya ajari hiyo ya Kisoka.

 

Majira ya saa 1 usiku wa jana Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia simu beki huyo wa kushoto wa Mabingwa hao watarajiwa wa Msimu huu unaoelekea Ukingoni.

  Mazungumzo yalikuwa hivi.

 

Mwandishi- Mambo Vipi?

.

 Kibwana- Hoo Safi bro Shekidele habari za Moro.

Mwandishi- Mungu ni Mwema huku tuko salama, Wana Moro walishuhudia gemu ya Yanga na Simba kupitia Luninga wakakuona Mwana Morogoro mwenzo umeshindwa kuendelea na mchezo baada ya kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji wa Simba Kibu Denis na baadae ukakimbizwa hospital je unaendelea je  na umeshatoka hospital?.  

Kibwana- Asanteni sana wana Morogoro wenzangu kwa upendo wenu kwangu kweli niligongana na Kibu nikashindwa kuendelea na mchezo kikakimbizwa hospital nashukuru Mungu nimepata matibabu kwa muda wa msaa kadhaa madaktari wakaniruhusu nikarejea kambini.

Kupitia Mtandao wa Shekidele ambao mimi ni mdau mkubwa toka nikiwa Mtibwa niwatoe hofu wana Moro na wana Yanga kwa ujumla kwamba kwa sasa naendelea Vizuri na tayari niko kambi ya timu ya Taifa, juzi na jana nimefanya mazoezi na wenzangu.

 

Mwandishi. Ok swali la Mwisho kuna Picha umekumbatiana na Kibu Denis Mkiwa hospital je alifunga safari kuja hapo hospital kukuona au naye alifika hapo kwa matibabu?

Kibwana. Kibu naye aliretwa pale hospital niliyokuwepo ambayo jina lake nimelisahau baada ya kutibiwa na kupewa muda wa kupunzika alikuja kwenye wodi yangu kuniona tukapeana Pole tukakumbatiana then akarejea kwenye wodi yake kwa kuwa mimi nilikuwa wakwanza kufika na kupata tiba niliruhusiwa kabla yake So  nikaenda kwenye wodi yake nikamuaga.

Mwandishi- Asante sana kwa ushirikiano wako

 Kibwana- Poa poa Shekidele kupitia Mtandao wako tunapata habari za nyumbani Morogoro.

Kwa sasa timu ya Yanga inawachezaji watatu ambao ni wadau wakubwa wa Mtandao wa Shekidele.

 wachezaji hao walioibuliwa Vipaji vyao na  taasisi ya Moro Kids ambao badae wakaenda Mtibwa B kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa  kisha kutimkia yanga kwa nyakati tofauti ni Kibwana Shomary,  beki wa kati Dikson Job na Kipa Abutwalib Msheri.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...