Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, May 30, 2022

UCHANGUZI. HII IMEKAA VIZURI, SIMBA NA YANGA SI UADUI.


 


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Juzi Jumamosi Mei 28 nchini ilisimama kwa muda wa dakika 90 kupisha gemu ya watani wa Jadi kutoka eneo Moja la Kariakoo Jijini Dar es salaa.

 

 

  Timu hizo kongwe nchini ni Yanga  iliyoanzishwa Mwaka 1935 yenye Maskani yake  Makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo, huku Simba iliyoanzishwa Mwaka 1936 Maskani yake yakiwa Mtaa wenye Pilikapilika nyingi Mtaa wa Msimbazi  Kariakoo.

Wababe hao wa Soka la Tanzania Walikutana Juzi kwenye Mchezo wa nusu fainali ya Michuano ya F.A Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

 

 

Katika gemu hiyo kulitokea matukio mengi moja ya matukio hayo ni beki wa Yanga Mluguru wa Kinole Morogoro Kibwana Shomari kugongana  Vichwa na Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis aliyepewa Uraia wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Tanzania Mwaka jana.

 

 

Katika ajari hiyo ya Soka Wawili hao walipasuka Vichwa huku Kibwana akishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa nje baada ya kupata maumivu makali, nafasi yake ikachukuliwa

na Farid Mussa.

 

Kibu aliyekuwa na uhai  kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba alitibiwa kwa takribani dakika 4 akavishwa bendeji kubwa kichwani lililoficha Rasta zake akarejea uwanjani kuipigania timu yake.

 

Mara baada ya gemu hiyo kutamatika kwa Wananchi Yanga Kumua Mnyama Simba kwa kumchoma mshale 1-0,Kibu alimtafuta Kibwana kwa lengo la kujua maendeleo yake na kufanikiwa kumuona  Vyumbani.

 

  Alipomuona alimjulia hali sambamba na wawili hao kuombana msamaha kasha wakakumbatiana huku kila mmoja akiwa na bendeji la jeraha Kichwani.  

 

 

 

Kibwana Shomari Mtoto wa Morogoro aliyeibuliwa Kipaji chake na tasisi ya Moro Kids akapelekwa Mtibwa B akaonyesha kiwango kizuri akapandishwa timu ya wakubwa kabla ya kutimkia Yanga.

 

 

Kibu Denis amejiunga na Simba Msimu uliopita akitokea Mbeya City ya Jijini Mbeya.

Kibwana na Kibu wote ni wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania'Taifa Stars'

 

Baadaye leo Mtandao huu utampigia simu  Mwana Morogoro  Kibwana Shomari kwa lengo la kumpa pole  sambamba na kujua maendeleo yake baada ya kupata dhuruba hilo.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...