Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, September 30, 2021

AFANDE SELE KAMA RONALDO KAPITA KWENYE VYAMA VYOTE VIKUU NCHINI.

          Afande Sele alipokuwa Mwanachama wa Chadema
...Alihama Chadema na kujiunga ACT Wazalendo akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu ofisi cha ACT iliypo Boma Road Manispaa ya Morogoro
...Tangazo lake la kugombea ubunge kupita ACT Wazalendo
...Akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni rais wa  Tanzania Hayati Magufuli mara baada  ya Afande Sele kujiunga na CCM
        Star wa dunia Cristiano Roanald akiwa Real Madrid
                                  ....Ronaldo akiwa Juventus
                               ...Roanald akiwa Mani U

 

                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mwanamuziki Mkongwe nchini wa ,Muziki wa Kizazi Kipya ambaye pia ni Mwanasiasa Chipukizi Selema Msindi ‘Afande Sele’ameweka rekodi ya kuwa Mwanamuziki pekee aliyefanikiwa kuvitumikia kwa vyakati tofauti vyama vikuu vya Siasa hapa Tanzania Chama Cha Demokrasia na Maendeleo’CHADEMA’, Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’. Na Chama Cha ACT Wazalendo

 

Afande Sele a.k.a Baba Tunda Mkazi wa Maeneo ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro kitendo chake hicho cha kuupiga mwingi kwenye vyama hivyo vikuu nchini ana fananishwa na Mwanasoko Maarufu dunia Cristiano Ronald Raia wa Ureno ambaye kwa nyakati tofauti naye amefanikiwa kuvitumikia vilabu vikubwa dunia.

 

Ronaldo amefanikiwa kuichezea timu  Maarufu dunia ya Real Madrid ya Hispania, baadaye akahamia timu nyingine Maarufu dunia Juventus  na juzikati ameikacha timu hiyo na kujiunga na timu tajiri dunia Manchester United’Mashetani wekundu’ ya England anayoutumika mpaka sasa ambapo jana Usiku kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’ Ronaldo aliifungia timu yake hiyo  bao la 2 dakika 90 nakuifanya timu hiyo ya Man U kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Villareal.

 

Kwa Upande wa Afande Sele awari alikuwa Chadema, baadae akatimkia ACT Wazalendo akiwa kwenye vyama  hivyo viwili kwenye chaguzi kuu alionyesha nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini.

Hata hivyo Mfalme huyo wa Rymes nchini alishindwa kuingia Mjengoni Dodoma kujiunga na wasanii wenzie  Joseph Haule’Profesa J’ aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi Morogoro kwa leseni ya Chadema na Joseph Mbilinyi’ Sugu’ aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kwa leseni ya Chadema kufuatia kushindwa kumng’oa Mpinzani wake Kipenzi cha Wana Morogoro Aziz Abood aliyepeperusha bendera za CCM vyema kwa kipindi cha tatu sasa.

 

Mwaka Juzi aliyekuwa rais wa awamu ya 5 hayati John Pombe Magufuli alipotinga mkoani Morogoro kuzindua kiwanda kipya cha Tumbaku Afande Sele mbele ya Rais Magufuli alitangaza kukihama chama cha ACT Wazalenzo na kujiunga na CCM’ akiunga mkono Juhuzi za rais huyo ‘Mzee wa Maamuzi Magumu’.

Kwa furaha Rais Magufuli alimkumbatia Afande Sele kisha akapiga naye picha kama wanavyoonekana Pichania

 

Wednesday, September 29, 2021

KUMBUKIZI.KIJANA ABADIRISHANA MATE NA NGEDELE



            Kijana huyo akbadirishana Mate na Ngedele


                    Na Dunstan Shedekiele,Morogoro.

Hii ni hatari kiafya,  Kijana Mmoja ambaye aligoma kutaja majina yake alinaswa  akimtumia Mnyama Ngedele kujipatia kipata kwa kubadirishana naye Mate ‘Kura Denda’.

 

Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye Pilikapilika zake za kusaka matukio  alimnasa Kijana huyo akimtumia Mnyama huyo kujipatia Kipata jambo ambalo ni hatari kwa afya wake.

 

Tukio hilo lilinaswa kwenye Mitaa iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro  Kijana huyo alikusanya Umati Mkumbwa wawatu kwa kitendo chache cha kubusiana na Mnyama huyo aliyemfundisha kila kitu ambapo kila kitu alichoelekezwa na bosi wake alikitii.

 

Kufuatia hali hiyo Kijana huyo aliutangazia Umati huo wawatu kwamba wamrushie Pesa ili azidi kufanya manjonjo na Ndedele huyo yakiwemo ya kubadirishana Mate na Mnyama huyo.

 

Wananchi hao waliokuwa na shahuku kubwa ya kuona tukio hilo la binadam kubusiana na Mnyama,walitii agizo hilo na kwa umoja wao walirusha Pesa za kutosha hivyo Kijana huyo alimwita Ndegele huyo aliyemvisha Kibwaya chekundu na kumwambia.

 

 “Njoo tubusiane” Ngedele huyo aliitika wito wa bosi wake akanyongea na alipofika alinyanyuka kama anavyoonekana Pichani  akafungua  mdomo na  Kijana huyo naye akafungua mdomo  na zoezi  la kubadirishana Mate likafanyika kwa takribani dakika 2 huku baadhi ya watu wakigubikwa na  mshangao Mkubwa.

 

Mara baada ya kukamilika kwa show hiyo hatarishi Mwandishi wa Mtandao huu alimfuata Kijana huyo kwa lengo la kuzungumza naye sambamba na kumuliza kama anafahamu kwamba kubadirishana Mate na Mnyama huyo ni hatari kwa afya yake.

 

Kijana huyo aligoma kutoa ushirikiano kwa Mwandishi huyo alihofia kwamba huenda alikuwa mtu wa Serikali,licha ya kutolewa hofu hiyo kijana huyo aliendeleakugoma alivyoona Mwandishi huyo anazidi  alimpaka Ngedele wake huyo’Kitega Uchumi chake’ na kuondoka eneo hilo.

 

Akizungumza na Mtandao huu kuhusiana na tukio hilo Mmoja wa madaktari wa Mkoani Morogoro aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Kitendo hicho ni hatari  kwa afya ya Kijana huyo.

 

”Baadhi ya wanyama wana bakteria kali hivyo kitendo cha Kijana yule kumeza mate ya Ngedele ni hatari sana kwa afya yake na kimsingi madhara hayo hawezi kuyaona sasa hivi atayaona siku zijazo na kama ana mwenzi wake naye akibadirishana naye Mate kuna uwezekana Mkubwa  kumwambukiza bakteria hizo ”alisema Daktari huyo.

Monday, September 27, 2021

TANZIA – KADA MAARUFU WA CCM AFARIKI DUNIA.

                        Salama Yange enzi za Uhai wake

 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MJI wa Morogoro jana na leo Umegubingwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha mtu Maarufu mwenye vyazifa nyingi Bi Salma Yange.'Mrs Mkalaboko'

 

 Hayari Salma, alikuwa ni Kigogo wa Kiwanda wa Tumbaku, Kada Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi’CCM’ Wilaya ya Morogoro, Mfanyabiashara Maarufu wa Magari na mwisho alikuwa ni mke wa diwani wa Kata ya Mindu Mh Zuberi Mkalaboko.

 

lkumbukwe Mh Mkalaboko kabla ya kutimia kwenye siasa na uchaguzi Mkuu uliopita kufanikiwa kutwaa n nafasi hiyo ya udiwani alikuwa ni Mtangazaji Maarufu wa Abood Media.

 

 Taarifa za awari ambazo Mtandao huu umezipata zilidai kwamba Mpendwa wetu Salma alijisikia vibaya jana asubuhi  akakimbizwa Zahanati ya Jeshi la Wanachini’JWTZ’ Kambi ya Mzinga, wakati madaktari akiendelea  kumtibabu arifariki dunia muda huo huo wa asubuhi.

 

Msiba upo  nyumbani kwao   Kata ya Mafiga Mtaa wa Misufini jirani kabisa na Msikiti wa Alhaj Omar ldd Mahira I.G.P Mstaafu 

INASIGITISHA SANA KWA FAMILIA HII YA YANGE.

Ndani ya Miaka Michache Familia hiyo  imeondokewa na watu watano mfurulizo. Mwandishi wa habari hizi ambaye kwa Neema za Mwenyezi Mungu alifanikiwa kushiriki Misiba yote hiyo na kumbukumbu zinaonyesha kwamba. Awari alianza kufariki  Rashid Yange aliyekuwa lspecter wa Kampuni ya Mabasi ya Abood, takribani miaka 2 iliyofuata akafariki Yahaya Yange aliyekuwa mfanyakazi wa Tumbaku akisimamia ununuzi wa Tumbaku kwa wakulima wa Mkoani Tabora.

Ina uma sana kwa sasa amebaki Leyla Yange peke yake Mungu akutie nguvu dada yetu kwenye kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Wapendwa wako.

 

 siku za hizi karibuni baba yao Mzazi Mzee Yange naye alifariki dunia na Jana ndio hivyo tumepokea taarifa zilizoumiza mioyo yetu za kifo cha Mpendwa wetu Salma. 

 Kwa sasa Mitando mingi ya kijamii inayomilikiwa na wana Morogoro imechafuka Picha zako wapendwa wako wakikulilia mtu wawatu Salama Yange.

 

Kazi ya Mungu haina Makosa Kila nafsi itaonya Umauti,tangulia dada Salma tutaonana badaye.

 

Sunday, September 26, 2021

UJUMBE WA NENEO LA MUNGU LEO JUMA;ILI

Mwandishi wa habari hizi akipokea wosi kutoka kwa bibi yake Mzaa Mama, Bi Kete Abdallah Batimayo[103].
Jeneza lililobena Mwili wa bibi Kete likiwa hospital ya Amana Jijini Dar kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwake  Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.

 Bibi Kete  alifariki dunia mwaka juzi akiwa na umri wa miaka 103



 

 

                              1TIMOTHEO 4. 14-16

 

“Usiache kutumia karama ile iliyomo ndani yako,uliyopewa kwa Unabii  kwa kuwekewa mikono na Wazee.

 

Uyatafakari hayo ukae katika hayo  ili kuendelea kwako  kuwe dhahiri kwa watu wote.

 

Jitunze nafsi yako  na mafundisho yako.Dumu katika Mambo hayo maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia”

 

Hili ndio neno letu la leo Jumapili ya Septemba 26.

                  

Hayati bibi Kete ameacha watoto 3 Tumaini  Samwel Juma, Mrs Shekidele. David Samwel Juma na Neema Samwel Juma’Mrs Mulokozi.

 

Pia ameacha wajukuu.Vitukuu na Vilembwe zaidi ya 200

“Bwana ametoa na Bwana ametwa Jina lake lihimidiwe’

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...