Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MJI wa Morogoro jana na leo Umegubingwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha mtu Maarufu mwenye vyazifa nyingi Bi Salma Yange.'Mrs Mkalaboko'
Hayari Salma, alikuwa ni Kigogo wa Kiwanda wa Tumbaku, Kada Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi’CCM’ Wilaya ya Morogoro, Mfanyabiashara Maarufu wa Magari na mwisho alikuwa ni mke wa diwani wa Kata ya Mindu Mh Zuberi Mkalaboko.
lkumbukwe Mh Mkalaboko kabla ya kutimia kwenye siasa na uchaguzi Mkuu uliopita kufanikiwa kutwaa n nafasi hiyo ya udiwani alikuwa ni Mtangazaji Maarufu wa Abood Media.
Taarifa za awari ambazo Mtandao huu umezipata zilidai kwamba Mpendwa wetu Salma alijisikia vibaya jana asubuhi akakimbizwa Zahanati ya Jeshi la Wanachini’JWTZ’ Kambi ya Mzinga, wakati madaktari akiendelea kumtibabu arifariki dunia muda huo huo wa asubuhi.
Msiba upo nyumbani kwao Kata ya Mafiga Mtaa wa Misufini jirani kabisa na Msikiti wa Alhaj Omar ldd Mahira I.G.P Mstaafu
INASIGITISHA SANA KWA FAMILIA HII YA YANGE.
Ndani ya Miaka Michache Familia hiyo imeondokewa na watu watano mfurulizo. Mwandishi wa habari hizi ambaye kwa Neema za Mwenyezi Mungu alifanikiwa kushiriki Misiba yote hiyo na kumbukumbu zinaonyesha kwamba. Awari alianza kufariki Rashid Yange aliyekuwa lspecter wa Kampuni ya Mabasi ya Abood, takribani miaka 2 iliyofuata akafariki Yahaya Yange aliyekuwa mfanyakazi wa Tumbaku akisimamia ununuzi wa Tumbaku kwa wakulima wa Mkoani Tabora.
Ina uma sana kwa sasa amebaki Leyla Yange peke yake Mungu akutie nguvu dada yetu kwenye kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Wapendwa wako.
siku za hizi karibuni baba yao Mzazi Mzee Yange naye alifariki dunia na Jana ndio hivyo tumepokea taarifa zilizoumiza mioyo yetu za kifo cha Mpendwa wetu Salma.
Kwa sasa Mitando mingi ya kijamii inayomilikiwa na wana Morogoro imechafuka Picha zako wapendwa wako wakikulilia mtu wawatu Salama Yange.
Kazi ya Mungu haina Makosa Kila nafsi itaonya Umauti,tangulia dada Salma tutaonana badaye.
No comments:
Post a Comment