Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, September 29, 2021

KUMBUKIZI.KIJANA ABADIRISHANA MATE NA NGEDELE



            Kijana huyo akbadirishana Mate na Ngedele


                    Na Dunstan Shedekiele,Morogoro.

Hii ni hatari kiafya,  Kijana Mmoja ambaye aligoma kutaja majina yake alinaswa  akimtumia Mnyama Ngedele kujipatia kipata kwa kubadirishana naye Mate ‘Kura Denda’.

 

Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye Pilikapilika zake za kusaka matukio  alimnasa Kijana huyo akimtumia Mnyama huyo kujipatia Kipata jambo ambalo ni hatari kwa afya wake.

 

Tukio hilo lilinaswa kwenye Mitaa iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro  Kijana huyo alikusanya Umati Mkumbwa wawatu kwa kitendo chache cha kubusiana na Mnyama huyo aliyemfundisha kila kitu ambapo kila kitu alichoelekezwa na bosi wake alikitii.

 

Kufuatia hali hiyo Kijana huyo aliutangazia Umati huo wawatu kwamba wamrushie Pesa ili azidi kufanya manjonjo na Ndedele huyo yakiwemo ya kubadirishana Mate na Mnyama huyo.

 

Wananchi hao waliokuwa na shahuku kubwa ya kuona tukio hilo la binadam kubusiana na Mnyama,walitii agizo hilo na kwa umoja wao walirusha Pesa za kutosha hivyo Kijana huyo alimwita Ndegele huyo aliyemvisha Kibwaya chekundu na kumwambia.

 

 “Njoo tubusiane” Ngedele huyo aliitika wito wa bosi wake akanyongea na alipofika alinyanyuka kama anavyoonekana Pichani  akafungua  mdomo na  Kijana huyo naye akafungua mdomo  na zoezi  la kubadirishana Mate likafanyika kwa takribani dakika 2 huku baadhi ya watu wakigubikwa na  mshangao Mkubwa.

 

Mara baada ya kukamilika kwa show hiyo hatarishi Mwandishi wa Mtandao huu alimfuata Kijana huyo kwa lengo la kuzungumza naye sambamba na kumuliza kama anafahamu kwamba kubadirishana Mate na Mnyama huyo ni hatari kwa afya yake.

 

Kijana huyo aligoma kutoa ushirikiano kwa Mwandishi huyo alihofia kwamba huenda alikuwa mtu wa Serikali,licha ya kutolewa hofu hiyo kijana huyo aliendeleakugoma alivyoona Mwandishi huyo anazidi  alimpaka Ngedele wake huyo’Kitega Uchumi chake’ na kuondoka eneo hilo.

 

Akizungumza na Mtandao huu kuhusiana na tukio hilo Mmoja wa madaktari wa Mkoani Morogoro aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Kitendo hicho ni hatari  kwa afya ya Kijana huyo.

 

”Baadhi ya wanyama wana bakteria kali hivyo kitendo cha Kijana yule kumeza mate ya Ngedele ni hatari sana kwa afya yake na kimsingi madhara hayo hawezi kuyaona sasa hivi atayaona siku zijazo na kama ana mwenzi wake naye akibadirishana naye Mate kuna uwezekana Mkubwa  kumwambukiza bakteria hizo ”alisema Daktari huyo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...