Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, September 30, 2021

AFANDE SELE KAMA RONALDO KAPITA KWENYE VYAMA VYOTE VIKUU NCHINI.

          Afande Sele alipokuwa Mwanachama wa Chadema
...Alihama Chadema na kujiunga ACT Wazalendo akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu ofisi cha ACT iliypo Boma Road Manispaa ya Morogoro
...Tangazo lake la kugombea ubunge kupita ACT Wazalendo
...Akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni rais wa  Tanzania Hayati Magufuli mara baada  ya Afande Sele kujiunga na CCM
        Star wa dunia Cristiano Roanald akiwa Real Madrid
                                  ....Ronaldo akiwa Juventus
                               ...Roanald akiwa Mani U

 

                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mwanamuziki Mkongwe nchini wa ,Muziki wa Kizazi Kipya ambaye pia ni Mwanasiasa Chipukizi Selema Msindi ‘Afande Sele’ameweka rekodi ya kuwa Mwanamuziki pekee aliyefanikiwa kuvitumikia kwa vyakati tofauti vyama vikuu vya Siasa hapa Tanzania Chama Cha Demokrasia na Maendeleo’CHADEMA’, Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’. Na Chama Cha ACT Wazalendo

 

Afande Sele a.k.a Baba Tunda Mkazi wa Maeneo ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro kitendo chake hicho cha kuupiga mwingi kwenye vyama hivyo vikuu nchini ana fananishwa na Mwanasoko Maarufu dunia Cristiano Ronald Raia wa Ureno ambaye kwa nyakati tofauti naye amefanikiwa kuvitumikia vilabu vikubwa dunia.

 

Ronaldo amefanikiwa kuichezea timu  Maarufu dunia ya Real Madrid ya Hispania, baadaye akahamia timu nyingine Maarufu dunia Juventus  na juzikati ameikacha timu hiyo na kujiunga na timu tajiri dunia Manchester United’Mashetani wekundu’ ya England anayoutumika mpaka sasa ambapo jana Usiku kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’ Ronaldo aliifungia timu yake hiyo  bao la 2 dakika 90 nakuifanya timu hiyo ya Man U kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Villareal.

 

Kwa Upande wa Afande Sele awari alikuwa Chadema, baadae akatimkia ACT Wazalendo akiwa kwenye vyama  hivyo viwili kwenye chaguzi kuu alionyesha nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini.

Hata hivyo Mfalme huyo wa Rymes nchini alishindwa kuingia Mjengoni Dodoma kujiunga na wasanii wenzie  Joseph Haule’Profesa J’ aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi Morogoro kwa leseni ya Chadema na Joseph Mbilinyi’ Sugu’ aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kwa leseni ya Chadema kufuatia kushindwa kumng’oa Mpinzani wake Kipenzi cha Wana Morogoro Aziz Abood aliyepeperusha bendera za CCM vyema kwa kipindi cha tatu sasa.

 

Mwaka Juzi aliyekuwa rais wa awamu ya 5 hayati John Pombe Magufuli alipotinga mkoani Morogoro kuzindua kiwanda kipya cha Tumbaku Afande Sele mbele ya Rais Magufuli alitangaza kukihama chama cha ACT Wazalenzo na kujiunga na CCM’ akiunga mkono Juhuzi za rais huyo ‘Mzee wa Maamuzi Magumu’.

Kwa furaha Rais Magufuli alimkumbatia Afande Sele kisha akapiga naye picha kama wanavyoonekana Pichania

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...