Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 10, 2021

MMILIKI WA GEST ATOA UFAFANUZI TAA YA BARABANI KUWEPO KWENYE ENEO LAKE, MWENYEKITI WA MTAA NAYE ATIA NENO.

                   Taa hiyo  Mali ya Serikali ikiwa eneo la Gest
Taa hiyo nayo iligongwana gari barabara hiyo hiyo ya Kichangani
Siku mbili mbele Mwandishi wa Mtandao huu alipokatiza eneo hilo alikuta taa hiyo haipo kama inavyoonekana Pichani
 Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mchuma  Kata ya Kichangani Athanael Chacha akihojiwa na Mtandao huu leo asubuhi.


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Juzi Mtandao huu uliriripoti habari ya chini ya kapeti ya Taa ya barabarani kunaswa nyumba ya kualala wa geni[ Gest House].

 

 Mwandishi wa habari hizi baada ya kupiga Picha taa hiyo ikiwa eneo la gest hiyo alitinga ndani ya gest hiyo kwa lengo la kuzungumza na Mmiliki lakini kwa siku hiyo yaani juzi Mmiliki huyo akuwepo.

 

Hivyo jana Mtandao huu ulitinga tena na kufanikiw akuzungumz ana Mmiliki wa gesti hiyo iliyopo maeneo ya Kichangani jirani kabisa na Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kichani.

Mmiliki huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mtui alipoulizwa kwani nini  Taa hiyo mali ya serikali iko kwenye nyumbani yake alijibu.

 

”Hii taa imeletwa hapa kwangu toka mwezi wa 12 mwaka jana, kama utakumbuka mwezi huo ulikuwa ni mwezi wa mvua zilizoambatana na upepo Mkali. Hivyo taa hii iliangukiwa na mti ulioangushwa na Upepo, mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huu kwa kushirikiana na watu wa TARURA walifika hapa na kuniomba niwahifadhia taa hii kwa muda. Ikaweka ndani chaajabu toka mwaka jana mpaka leo mwezi wa 8 hawakuja kuichukua kwa vile naendelea na ukarabati kwenye gesti yangu nikaamua kuitoa nje na kuiweka nje jirani na barabara ili wahusika waione waje kuichukua”alisema Mmiliki huyo wa Gest.

 

Baada ya kupokea maelezo hayo Mwandishi wa habari hizi alitinga kwa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mchuma Kata ya Kichangani  Mh Athanael Chacha na kwamba alipoulizwa kama anataarifa ya taa ya barabarani iliyopo mtaani kwake kung’olewa na kukutwa kwenye Gest ya Mama Mtui alijibu.

 

”Taa ile iliangushwa na Mti kipindi cha Masika Mwaka jana na baada ya kuangushwa wananchi walinipa taarifa na mimi nikawapigia simu Polisi akaja mkuu wa Upelelezi Wilaya na Meneja wa TARURA wa Wilaya.

Kwa vile walikuja na gari ndogo tukaichukua taa ile na kumuomba Mama Mtui atuhifazie kwenye gest yake huku meneja huyo wa TARURA akiahidi kuja kuichukua siku inayofuata na mimi nikamuomba afanye upesi ili mtaa wangu uendelea kuwa na nuru ya Mwanga. Sasa nashangaa Mwandishi unavyoniambia Mpaka leo taa ile bado iko kwa Mama Mtui” alisema Mwenyekiti huyo kwa Mshangao.

Alipoulizwa kwa nini Mali hiyo ya Serikali wameiweka kwenye nyumba ya Mtu binafsi ili hali Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kichangani iko jirani kabisa na Gest hiyo  Majengo hayo yakitazamana Ofisi ya Mtendaji ambayo kimsingi ni jengo la Serikali liko kulia na Gest hiyo ya Mtu binafsi iko kushoto. Mwenyekiti Chacha alijibu

“ Swali zuri tumeshindwa kuweka taa ile kwenye ofisi ya Mtendaji kwa vile pale hakuna Mlinzi lakini kwenye gest ya Mama Mtui kuna walizi ndio maana usiku pia unakuta magari na Bajaj zinaegeswha pale sehemu salama”alisema  Mwenyekiti huyo ambaye kimsingi ni mlinzi wa Amani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mtaa huo.

 

Leo Mwandishi wa Mtandao huu ametinga ofisi za TARURA Wilaya kwa lengo la kuzungumza na Meneja wa TARURA kuhusiana na madai ya kuitelekeza mali hiyo ya serikali kwa mtu binafsi kwa muda mrefu.

 

P.C wa Meneja huyo alidai  bosi wake yuko nje ya ofisi kikazi huenda alikuwa kwenye ziara ya Mbizo za Mwenge ambao leo umezinduia Miradi mbali mbali katika Wilaya ya Morogoro.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...