Marehemu Sudy enzi za Uhai wake
TANZIA.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro. HATIMAYE jana tumempunzisha Mpendwa wetu Sudy Hamis Katoto kwenye nyumba yake ya Milele Makaburi ya Magomeni Jijini Dar jirani kabisa na Kaburi la Mpendwa baba yake Hayati Hamis Katoto tuliemzika pia kwenye makaburni hayo miezi 5 iliyopita.
Sudy alifariki dunia Jumapili maeneo ya Msamvu baada ya boda boda aliyokuwa akiendesha kugongana uso kwa uso na gari alifariki dunia Papo hapo huku abiri aliyempaki akijeruhiwa Vibaya.
lnauma sana Sudy ambaye baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia huku akiwe mtoto pekee wa kiume aliyebeba jukumu la kuwalea na kuwaongoza dada zake watatau Kulwa, Doto na Shamsa anayesoma darasa la 7.
Jumapili ilikuwa ni kumbukizi yake ya kuzaliwa’Happy Birthday’habari zilizopatikana juzi eneo la Msiba nyumbani kwao Kigurunyembe Manispaa ya Morogoro, zilidai kwamba siku hiyo ya Jumapili Sudy ilikuwa pia ni siku yake ya kumbukizi ya kuzaliwa.
Hivyo majira ya mchana alinunua Keki yake ya Birthday akawakabidhi dada zake huku akiwaeleza kwamba anaingia mtaa kusaka pesa na boda boda yake.
Akiwaeleza majira ya usiku atafika nyumbani hapo na Vinywaji kwa lengo la kusheherekea siku yake hiyo ya kuzaliwa akiwa sambamba na dada zake na marafiki zake wawili watatu.
lmeelezwa baada ya kuona usiku unazidi kusonga huku Sudy harejei nyumbani mmoja wa dada zake aitwaye Kulwa aliamua kumpigia simu na simu hiyo ilipokelewa na mtu Mwingine akisema.
“Simu hii ni ya boda boda amefariki dunia muda huu maeneo ya Msamvu kama ni ndugu yako fika Polisi au nenda chumba cha kuhifadhi maiti” alisema mtu huyo anayedaiwa kuwa ni Mwanausalama.
Hadi maiti yake inasafirishwa juzi jumatatu kuelekea Dar kwenye mazishi eneo la makaburi ya familia yao keki hiyo ya Birthday ya Marehemu Sudy ilikuwa ndani ya nyumbani hiyo na kwamba dada kila walipoiona keki hiyo walizidi kuangua kilio kwa uchungu.
Sudy arifariki dunia jumapili usiku na jumatu mchana msafari wa magari kadhaa ulielekea jijini Dar ambapo Sudy alizikwa jana jumanne.
Kila Nafsi itaonja Umauti Mbele yake nyuma yetu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu ya Kaburi Kijana wetu Sudy.
‘BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE AMINA’
No comments:
Post a Comment