Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, August 9, 2021

TANZIA. BODA BODA AFARIKI DUNIA KWENYE AJARI ILIYOTOKEA JANA USIKU MAENEO YA MSAMVU MORO.

                              Hayati Sud Hamis Katoto enzi za Uhai wake

                           Hayati Hamis Katoto Enzi za Uhai wake

                          

                          Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

             lNAUMA SANA.

Ikiwa ni takribani miezi 5 imepita toka Baba yake mzazi  Hayati Hamis Katoto afariki dunia ikiwa pia ni takaribani miaka 15 imepita toka Mama yake mzazi  Hayati, Khadija afarikiu dunia Sudi Hamis Katoto mtoto pekee ya kiume kwenye familia hiyo aliyeachiwa Jukumu la Malezi  ya dada zake 3 na wazazi wake hao waliotangulia mbele za haki.

 

Jana usiku Sudi akiwa kwenye kazi yake ya boda boda akisaka riziki ya kutumia na ndugu zake amefariki dunia baada ya bodo boda yake kugongana uso kwa uso na gari maeneo ya Msamvu na kufariki dunia papo hapo.

 

Baada ya kutokeka kwa Ajari hiyo Marehemu Sudi aliyekuwa akiegesha  boda boda yake kijiwe cha EQUTER Bar Kigurunyembe jirani na Makaburi ya Kolla Mwili wake ulihifadhi chumba cha Maiti hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro jana usiku.

 

Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ni Family Frend na familia hiyo ya Katoto hata kabla Hayati Khadija aliyekuwa Muhudumu  Kolla Hill Hotel wakati huo ikivuma akiwa na sura ya hotel ya Kitalii hajagariki dunia asubuhi na Mapema alifika nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Mahedu Kigurunyemba Kata ya Kilakala na kujumuika na familia katika Msiba huo Mzito.

 

 Swed Mkwabi Mkazi wa Dar ambaye ni baba mdogo wa Marehemu Sud alipofika muda huo wa asubuhi na kushiriki kikao cha familia kwa pamoja kikao hicho kiliafiki Sudi akazikwe Makaburi ua Magomeni Mapipa Dar eneo alilozikwa baba yake mzazi miezi 5 iliyopita.  

 

Hivyo  leo Majira ya saa 7 mchana Swed Mkwambi Mwenyekiti Mstaafu wa Klabu ya Simba aliongoza msafari wa magari 5 kuelekea Dar ambapo kesho Majira ya saa 7 mchana Mpendwa wetu Sudi atapunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele kwenye Makaburni hayo ya Magomeni.  

 

lkumbukwe Hayati Hamis Katoto aliyekuwa anamiliki kiwanda cha Ushonaji ndugu Uwanja wa Jamhuri jirani na Ofisi za Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro kabla hajariki dunia alikuwa alimfundisa Mwanaye huyo kuhona Nguo za na alishahitimu Mafunzo hayo na alikuwa mfundi Mzuri akimsaidi kazi baba yake kwenye kiwanda hicho. 

 

Mara baada ya Mpendwa baba yake kufariki dunia miezi 5 iliyopita Sud alisitisha kuendelea na ushonaji kwenye kiwanda hicho na badala yake aliamua kununua boda boda na kusaka kipato cha kutunza ndugu zake kwa bahati mbaya jana alizimika kama mshuma

                       Innalilahi Wainaillahii Rajiuon                                               


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...