Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WADAU wa Mtandao wa shekidele nawasalimu katika Jina la Jamhuri ya Mungano Tanzania.
Ama baada ya salamu tumekutana tena kwenye ukurasa wetu Pendwa wa Makala za Kijamii,Michezo na Mapenzi.
Mada ya leo ni ya kijamii ishu ikiwa ni Ukatili. Na dhuruma
Hivyo ungana nami na bila kupoteza muda nakudadavulia Mada hiyo.
UNAPOTOA Uhai wa mtu kwa namna yoyote ile kwa uonezi iwe kumpiga risasi, kumuua kwa kumpiga ngumu au kumuua kwa nguvu za giza wafikilie pia watu viumbe wanaomtegemea miongoni mwa viumbe hivyo wako watoto wake wakiwemo wachanga, wapo wazazi wake pamoja na ndugu na jamaa wanaomtegemea.
Pia kumdhurumu mjakazi wako Jasho lake hapa namaanisha ujira wake fikiria mara mbili watu wanaomtegemea.
Hii si kwa binadamu tu hata kwa wanyama na Ndege, mfano picha hii Mtu amemua huyu ndege ili hali alikwenda kusaka chakula cha Makinda’Watoto wake’ inauma sana watoto wanalia njaa huku mama yao emeuwawa kikatia jirani na kiota chake kilichojaa watoto wake.
Ukati kama huu si kwa mauaji tu hata unapomdhumu mtu haki yake Pesa na n.k huo nao ni ukatili kama ukati huo wa mauaji, katika kudhibitisha hili Mungu kupitia vitabu vya dini alitoa onyo kwenye tukio hili la dhuruma au kucheleweza malipo ya Mjakazi wako akisema
”Ukimpa Mjakazi wako kibarua cha kulima Mraba akimaliza kazi kwa usahihi kabla jasho halijakauka mwilini mwake mlipe ujira wake”
Zama hizi baadhi ya waajiri wanachuma dhambi kwa kukiuka agizo hili la Mungu tunapozungumzia waajiri ni pamoja na wewe mama au baba ulioajiri dada wa kazi’House Girl’ au kaka wa kazi’House Boy’.
Mwisho wa mwezi ukifika mlipe ujira wake na usimletee rongo rongo kwa sababu anakura ugari wako na kulala kwenye nyumba yako hayo hayahusiani na ujira wake.
Mwandishi wa Makala hii anajua ugumu wa maisha pia anajua wafanyakazi pia ni binadam wanauelewa hivyo kama ikitokea bosi umepata matatizo mwezi husika kayumba kiuchumia, kuugua, nk ni vyema ukazungumza na mfanyakazi wako mapema ukimuomba kusogeza mbele malipo yake.
Kama akilidhia naamini ataridhia kwa vile stretion husika ameishuhudia atakubali ombi lako, akikubali namini hapo nakuna tatizo ila dhambi itakupata ukitumia ubabe wa ubosi wako kumdhurumu mfanyakazi wako.
Kwa vile anashida na bado anahitaji hiyo kazi na hana sehemu nyingine ya kupata kazi atakubali shigo upande huku kila siku akinung’unika moyoni, naamini naye kuna watu kawakopa kwa ahadi kwamba mwisho wa mwezi akipokea haki yake atalipa hayo madeni hivyo kitendo cha bosi kutomlipa kwa wakati au kumdhurumu kabisa unamsababishi matatizo itaradhimika achume dhambi kuwadanganya wanaomdai naamini dhambi hiyo haipati yeye utaipata wewe bosi au mdaiwa.
Kwa leo naishia hapa tukutane wiki ijayo kwa Makala Moto moto ya Mahusiano, kwa ushauri au Maoni wasiliana nami kwa namba 0715 20 90 73.