Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 27, 2021

TWAHA KIDUKU AWASHUKURU WAKAZI WA MORO KWA MAPOKEZI MAKUBWA, C.E.O MSJ AIBUKA KWENYE SHANGINGI LAKE NA KUFANYA KAZI YA UPAPARAZI.

Bondia Twaha kiduku akiwashukuru wananchi wa Mkoa wa Morogoro
Diwani wa Kata ya Mkundi Mh Seif Chomoka akishiriki mapokezi hayo akichomoka juu ya ndinga yake ya bei mbaya Shangingi V8

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Aziz Abood akiongoza mapokezi yake akichomika juu ya Shangingi lake Titota V8 Wanasisi hao wawili Abood na Chomoka ndio ambao walitisha na magari yao ya kifahari akishiriki maandamano hayo ya kuchomoka juu ya magari yao


 

                          Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Bondia Maarufu  nchini asiye na Mpinzania kwa sasa kufuatia  kuwatwanga Mabondia Maarufu na wengine kukacha kupigana naye Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’ amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa mapokezi makubwa waliyompatia baada kumtwanga kwa mara ya Pili bondia  Abdallaha Pazi Dulla Mbabe Mkazi wa Dar.

 

Baada ya kushuhudia Umatia Mkubwa wawatu hasa alipofika katikati ya Mji wa Morogoro Kiduku alishangwaza na Umati huo na akaamua kunyoosha mikono yake kisha akaiunganisha ikiwa ni ishara ya kuwashukuru.

Mara baada ya kuwasili maeneo ya Mikese akiwa ndani ya gari yake Mpya ya zawadi Crown akitokea Dar Kiduku alishuka kwenye gari hilo na kupanda kwenye gari la wazi pamoja na Mwandishi wa Mtandao huu na kuanza safari ya kuelekea Moro Mji kutoka Mikese umbali wa kilomita 25.

 

Katika Msafara huo walikuwepo watu wengi Maarufu wakiongozwa na  Afisa Mtendaji Mkuu [C’E,O] wa Chuo Cha Uandishi wa Habari Morogoro’MSJ’ Seif Chomoka ambaye pia ni Mh Diwani wa Kata ya Mkundi kwa leseni ya CCM.

 

Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Big Boss huyo wa MSJ akiibuka kwa juu kwenye Shangingi lake ‘Totota V8’ na kuanza kupiga Picha Msafara huo akitumia kamera ya simu huku akitinga Flana nyeupe yenye Picha ya Twaha Kiduku.

 

Mh Chomoka mbali ya kuwa Mwanasiasa pia ni Mwanamichezo Mzuri ambapo juzikati kwenye uchanguzi  Mdogo wa kujaza nafasi za Viongzi wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Mh Chomoka aligombea nafasi ya Katibu Mkuu kwa mshangao wawengi jina lake lilikatwa dakika za mwisho kuelekea kwenye mchaguzi huo ambapo Mchungaji Emmanuel Kimbawaya Mkazi wa Tubuyu aliibuka kidedea kwenye nafasi hiyo ya Katibu Mkuu.

 

lkumbukwe Mh Chomoka pia kwenye Uchaguzi wa Umeya awari alishinda kwa kura 20 zidi ya 19 za Mpinzani wake Pascal Kihanga aliyekuwa akitetea kiti chake.

Siku chache mbele uchaguzi huo uliludiwa kwa maelezo kwamba Chomoka ahakuvuka nusu ya kura za wajumbe 42 waliopiga kura.

 

Hivyo goma likaludiwa  huku mgombea wa 3 aliyepata 3 aliamua kujitoa wakabaki Kihanga na Chomoka kura zikapigwa zaidi ya mara 2 wawili hao walifungana kwa kupata kura 21 kwa 21 baadae majina yote 2 yakapelekwa Dodoma na majibu yakaludi Mh Kihanga ambaye ni Diwani wa Kata ya Mazimbu  katangazwa Mshindi hivyo akaendelea na nafasi yake hiyo ya Umeya.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...