Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, August 25, 2021

MAPOKEZI YA KISHINDO YA TWAHA KIDUKU, KWA WAKAZI WA MORO SIO STORI AMEFUATA NYAYO ZA WATANGULIZI WAKE.

 
Twaha Kiduku akiwapungi mashabiki waliojitokeza kwa wingi kumlaki
..Gari ambalo amekabidhiwa baada ya kumtwanga Dulla Mbabe likiwasili Mkoa Morogoro eneo la Nane nane

..Mh Abood akiongoza Manimia ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro kumlaki Twaha Kiduku
Msafara huo ukiwa eneo la Kingolwira jirani na Kituo cha Polisi
Msafara huo ukiwa Mkambarani jirani na baa ya Afande Zombe
Mc wa shughulia hiyo Calvin Ponela 'Zombi' akiwajibika kuamsha amsha
..Heka heka gari la Samora Mwarabu Maarufu Samora Simba Oil liliganga na gari lingine kwenye heka heka hizo za aMapokezi ya Twaha

Twaha Kiduku akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa ndani ya gari hilo la Wazi akuchukua matukio mbali mbali
Twaha Kiduku akiwa na Kocha wake Chaaz Mbwana'Power lranda'
Twaha Kiduku akiiwa ndani ya studio za Planet Redio Morogoro
Bondia Francsi Cheka akiwa na Mwandishi wa Mtandao huum siku chache baada ya kumtwanga Thomas Mashali
Afande Sele akiwa na wattoto wa Mwandishi wa Mtandao huu Kulia Tumain Dustan Shekidele, ambaye alisoma darasa Moja na mtoto wa Afande Sele Tunda shule ya Msingi Nguzo Eglish Mediam[ kushoto ni Neema Dustan Shekidele.
                       Mwishi Mwampamba


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

TAKRIBANI Mwezi mzima Wananchi wa Dar[Wazalamo] na wenzao Moro[Waluguru] walikuwa wakitambia huku wakipigana vijembe kila Moja akidai Bondia wake ataibuka kidedea na kunyakua zawadi ya Gari.

 

Agost 20 Promoto Maarufu wa ngumi nchini ‘Mjeda’ Kanali Seleman Semunyu ambaye pia asili yake ni Morogoro aliisimamisha nchini na kwa kuandaa Mpambano wa Ngumi uliowahusisha wapinzani wa Jadi Twaha Kassim’ Twaha Kiduku Kutoka Morogoro na Abdallah Pazi’ Dulla  Mbabe Mkazi wa Dar.

 

Katika Mpambano huo usio wa ubingwa wa kugombea gari aina ya Crown ambapo mpambano huo umepewa jina la ‘Crown toa Roho’ulipigwa Ukumbi wa Ubongo Plaza jijini Dar nyumbani kwa bondia Dulla Mbabe.

 

Kwenye tambo hizo wananchi wa Dar Wazalamo waliwatania wenzao wa Moro’Waluguru kwamba gari hilo la kifahari litabaki Dar kwa vile Morogoro hakuna barabara za kupiga gari hilo.

 

Huku wananchi wa Moro wakijibu mapigo wakiwaeleza Wazalamo kwamba maisha yao siku zote yanategemea wananchi wa Morogoro, wakitolea Mfano Maji ya kunywa na Umeme wananchi hao wanategemea kutoka Moro pia Mkuu wa wa Mkoa Mh Amos Makalla ni Mwana Morogoro.

 

Mwandishi wa habari ambaye naye ni Mkazi wa Morogoro anawaongezea nyama wananchi hao wa Moro kwa kuwaeleza kwamba Promota wa Pambano hilo Kanali Semunyu ni Mwanamorogoro kwao ni Msamvu Magodoroni na Meneja wa Ukumbi wa Ubungo Plaza lilipofanyika pambano Mr Sozi ni Mwanamorogoro ambaye alisoma shule ya Msingi na Mwandishi wa Mtandao huu. 

HII NI MARA YA 4 WASANII WA MORO WANANYAKUA GARI MBELE YA WASANII WA DAR.

 

Kwa wakazi wa Morogoro kukusanyika kwa wingi kuwapokea wasanii walionyagua magari mbele ya wasanii wa Dar hii si Mara ya kwanza kwa Kiduku’. Mara ya kwanza ni Mwaka 2003 ambapo umati Mkubwa wawananchi wa Moro walijitokeza Maeneo ya Mikese kumpokea Mwisho Mwampamba aliyeibuka mshindi wa Pili kwenye jumba kubwa la Afrika Kusini Big Brother Afrika’BBA’na kuzawadi Milion 50 kwenye shindano hilo wasanii wa Dar na wamataifa mengine walitolewa hatua za awari huku Mwampamba akiin’alisha Tanzania na Mkoa wake wa Morogoro,

 

Kama hiyo haitoshi Mwaka 2004 Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Selema Msindi ‘Afande Sele’ alipokelewa na Umati Mkubwa wawananchi wa Morogoro waliojipanga toka Mikese Mpaka Mo Town baada ya Msanii huyo kunyakua zawadi ya gari kwenye shindano la  kumsakali mkali Vina Mfalme wa Rhymes lililofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar.

 Mwandishi wa Mtandao huu alikuwa ndani ya Nyumba ambapo Shindano hilo liliwashirikisha wasanii 10 nyimbo zao kwenye mabano 1.Afande Sele[Dalubini Kali]

2.Inspector Harun[Bye Bye]

3.Man dojo na Domokaya[Nikupe Nini]

4.Mwana-FA[Umenitega]

5.JayMo[[ Kama Unataka]

6. Solo Thang[[Mtazamo]

7.Madee [Kazi yako Mola]

8. Soggy Dogg[Kulwa na Dotto] .

9. Prof J [Goma lake limenitoka kichwani]

10. Dully Sykes ambaye alijitoa kwenye shindani hilo dakika za Mwisho huenda akihovia Moto wa Afande Sele. Haikuishia hapo ndio maana tunasema Mapokezi makubwa kwa wasanii wa Moro sio habari kubwa inaweza kuwa habari kubwa kwa wananchi wa Dar ambao hawajawahi kushinda zawadi ya gari mbele ya wasanii kutoka Moro kama Mwaka 2017 Bondia Francsi Cheka mbali ya kuingwanga Familia ya Masumbwi ya Matumla alimtwanga Mwana Dar nyumbani kwake Dar  Thomas Mashali kwenye Pambano la kugombea gari aina ya Noah, ambapo umati Mkubwa wawananchi wa Moro walijipanga toka maeneo ya Mikese Mpaka Mo Town wakilisukuma gari halo umbali wa takribani kilometa 25.

 

Juzi Twaha Kiduku hapo hapo Dar amempiga kwa mara ya Pili Dulla Mbeba na kuzawadiwa Gari ambapo mapokezi yake ya kufana ndio hayo Pichanim huku Dulla Mbabe na wazalamo wake wakiwa Dar wakishuhudia Mapokezi hayo kwenye Mitandao ya Kijamii huku wakienda kununia kwao kwa hasira. Wana Moro wanasema Bendera Chuma, Mlingoti Chuma Show Show kituoa kinachofuatani Where? Tanga au ila Tanga sio powa kama mnavyozani.

 

 
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...