...Kwenye gemu hiyo Chadongo walisingikizwa na Matarumbeta ya Wasambaa Mawenzi na Mindu
Katika gemu hiyo nyota wa mchezo alikuwa Jamaa huyu George Chota ambaye kwa hiyali yake mwenyewe msimu ulipita alijiondoa katika kikosi cha Mbeya City na kurejea nyumbani Morogoro, licha ya kubanwa na Mtandao huu Chota aligoma kutaja sababu iliyomfanya akaikimbia timu hiyo ya watoza ushuru wa jiji la Mbeya
Kikosi cha Chadongo, Mfungaji wa bao lililoza vulugu Hassan Mkota 'Messi' wapili kutoka kushoto waliochuchua
Baadhi ya umati wa Mashabiki waliofulika jana uwanja wa Saba saba wakifuatilia mtanange huo wa kibabe.
Kikosi cha Black People'Taifa la watu weusi'
.......Heka heka uwanjani
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Robo fainali ya Michuano ya The Gunners ‘Super 16’ ndondo Cup 2020-21 kati ya watani wa jadi Chadongo na Black People iliyopigwa jana uwanja wa Saba Saba imevunjika dakika ya 85 baada ya mashabiki wa People kumvamia Mshika kibendera namba 1 wakimlalamikia kulikubali bao la kuotea la Chadongo.
Kabla ya vulugu hizo kutokea dakika hizo za lala salama matokeo yalikuwa sale ya 0-0 na dakika ya 85 Mshambuliaji wa Chadongo Hassan Mkota’Messi wa Chamwino’ alifunga bao hilo lililolalamikiwa na Black People.
Kiukweli inga Mtandao huu haungi mkono vulugu hizo lakipi pia tunashumu mshikakibendera huyo aliteleza kutafsili sheria namba 11 ya kuotea ‘Off Side’ na Kamwe waamuzi wasijifiche kwenye kichaka cha ‘Waamuzi nao ni binadam wanakose’.
Stretion kama ya Jana kweli Messi Mchezaji wa zamani wa Geita Gold alipewa pasi ya mwisho na Twaribu Chacharo mchezaji wa zamani wa Mawenzi Market ambaye kwa sasa anakipiga Pitayosi ya Tabora akiwa peke yake nje kidogo ya boksi la Black People alichofanya akafumua shuti lililomshika Kipa wa People Hassan Hamis’ anayeidakia Simba A.
Kipa huyo kwenye michuano hiyo ameonyesha uwezo mkubwa pasina shaka yoyote uwezo wake binfsi ndio ulioivuka People kutinga robo fainali hiyo.
Kwenye hatua ya 16 Kipa huyo mbali ya kudaka mikwaji mikali ya washambuliaji wa timu ya Miembe 3 Nikson Kibabage mchezaji gedemo kwa sasa wa timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ na Mrisho Said ‘Ziko wa Kilosa’ Mtoto wa hayati Said Mrisho ‘Ziko wa Kilosa’ Hali hiyo ilipelekea timu hizo kutoka sale ya 1-1 na zilipoingia kwenye mikwaju ya Pelnaty Kipa huyo wa Simba A alinyaka mikwaju 2 huku People ikifanikiwa kufunga mikwaju yote 5.
Akizungumza na Mtandao huu kuhusiana na hatima ya mchezo huo uliovunjika Kaimu Mratibu wa michuano hiyo Mrisho Chuchunge alisema jana hiyo hiyo kamati imeketi na kutoa maamuzi ya kuipa ushindi Chadongo na kuiondosha kwenye michuano hiyo Black People ‘Taifa la Watu weuzi kutoka Mji Mpya.
”Shekidele kanuni ziko wazi timu inayoanzisha vulugu mchezo ukivunjika inaondolewa kwenye Mashindano na mpinzani wake anapewa ushindi”alisema Mratibu huyo.
Ukionoa dosari hiyo kwa muda wote wa dakika 85 gemu hiyo ilikuwa tafu na mashabiki waliolipa kiingilio chao cha buku 2 wali enjoy Show.
No comments:
Post a Comment