....Wanafunzi wenzie wa aliokuwe akisoma nao darasa moja wakishiki kumuombea dua
....Jeneza lililobeba mwili wa Sabrini likiingizwa kwenye gari tayari kuelekea makaburini
...Wanafuzni hao wa la 3 waliofika eneo la Msiba na walimu wao walibaka hapo nyumbani wakati mwili wa mwenzao ukipelekwa makaburini
...Sabrini akizikwa huku dent mwenzi wa kiume alishindwa kubaki nyumbani akawatoka walimu na sare zake za shule akatinga makaburini kumzika mwenzie
Hapa ndipo alipolala mpendwa wetu Sabrina
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Mamia ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro leo Jioni wamejitokeza kwa wingi kumzika Dent wa la 3 hayati Sabrina Abdallah, aliyefariki dunia jana jioni baada ya kusombwa na maji ya Mto Morogoro.
Awari Mtandao huu jana ulianda habari hii kwa mfuno wa udakuzi baada ya habari husika kutokamilika kwa maana ya kuzungumza na Wafiwa, pamoja na Uongozi wa serikali ya Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro alipokuwa akiishia Marehemu huyo.
Mwandishi wa habari hizi leo aliingia kazi na kufanikiwa kuzungumza na Mwenyekiti wa Mtaa huo Hashim Bito ambaye alithibisha denti huyo kusombwa na Maji na kuelezea A-Z tukio hilo.
Dent huyo anayesoma darasa la tatu shule ya Msingi Mwere ‘B’ alifariki dunia jana baada ya kutereza kwenye kina kirefu cha Maji ya Mto Morogoro Majira ya saa 9 Alasiri muda mfupi baada ya kutoka shuleni.
Mpendwa wetu Hayati Sabrina alizikwa leo muda huo huo wa saa 9 Alasiri katika Makaburi ya Kolla huku Umati Mkubwa wawanchini kutoka maeneo mbali mbali ulijitokeza kushiriki mazishi hayo wakiwemo wanafunzi wenziye wa darasa la tatu ambao walikuwa jirani na jeneza wakishiriki kumuombea dua mwanafunzi mwenzo waliyekuwanaye darasani kutwa nzima ya siku ya jana kabra leo asubuhi kupokea taarifa za kifo cha mwenzo huyo.
Baada ya kurejea Makaburi Mwandishi wa habari hizi alirejea nyumbani kwa wafiwa hapo Mama Sabrina alikuwa bado hajawa sawa kutokana na maumivu makali ya kuondokewa na Mpendwa mtoto wake huyo pekee aliyezimika kama mshumaa, hivyo busara zimemuongoza Mwandishi wa habari hizi kusitisha zoezi la kumhoji.
Kesho panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu tutazungumza naye na kukamilisha habari hii iliyogusa watu wengi. Cha Msingi endelea kuwa jirani na Mtandao huu Muda wote.
Angalia Picha mbali mbali za matukio ya mazishi hayo kesho mambo yakienda vizuri tutarusha picha ya Sabrina enzi za uhai wake.
No comments:
Post a Comment