Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 14, 2021

NJEMBA ANASWA USIKU MNENE AKIDAIWA KUIBA VITI VYA BAA

                                                  ....Akijitwishwa viti hivyo

                              ,,,Akihojiwa na masele wa Mji Mpya

                      ...Akiondoka zake na lumbesa hilo la Viti 


.
                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
JAMAA Mmoja ‘Njemba’aliyefahamika kwa jina la Ally Toll amenaswa na lundo la Viti anavyodaiwa kuvikwapua kwenye baa kwa lengo la kwenda kuvipiga bei. 
 
Tukio hilo limetokea juzi usiku Maeneo ya Mji Mpya jirani na Soko, ambapo mtuhumiwa huyo aliyetajwa kuw ana katabia ka udokozi alinaswa akiwa amebebe lundo la Viti vya Prastik anavyotumiwani kuviiba kwenye moja ya baa zilizopo Kata hiyo ya Mji Mpya. 
 
Baada ya kushuhudia tukio hilo, baadhi ya Wananachi waliamua kutoa taarifa kwa Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika eneo la tukio ndani ya dakika o na kushuhudia Njema huyo akipokea kichapo toka kwa wananchi wenye hasira. 
 
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Bashiri Kiwamba walisema
 
” Huyu Jamaa ni mdokozisana hapa Mtaani akikuta nguo kwenye kamba anaanua, akikuta ndoa ana beba akikuta viti ana somba, ndio maana tulivyomuona usiku huu na hivi vipi tumejua tu ameviiba tulivyomsimamisha kavibwaga kikambia, tumemkimbiza tukamkamata ndio wananchi wakaanza kumshushia kichapo.
 
” Mtuhumiwa huyo alipohojiwa na Mwandishi wa habari hizi alishindwa kujibu maswali kwa kile kilicho onekana kuzidiwa na kilevi Sambamba na maumivu ya kichapo hicho havi kutoka kwa raia. 
 
Katika hali ya kushangaza baadae Wananchi hao walimuachia Mtuhumiwa huyo ambaye baada ya kupata upenyo huo alijitwisha Viti hivyo na kutokomea navyo kusikojulikana kama anavyoonekana Pichani. 
 
Utafiti wa awari uliofanywa na Paparazi wa Mtandao huu ulibaini kwamba Wananchi hao walifika uamuzi huo wa kumuachia Mtuhumiwani huyo kwa kuwa Mlalamikaji kwa Maana ya Mmiliki wa Viti hivyo hakuwepo eneo la tukio. 
 
Taarifa nyingine ambazo hazijadhibitishwa na mtu yoyote zilidai kwamba baadhi ya wananchi hao walimfuatilia kwa nyunba Njema huyo Mlevi na kumpora Viti hivyo na kwendao kuvipiga bei yao kufuatia Mmiliki wa Viti hivyo kutojulikana. 
 
Kufuati hali hiyo Mwandishi wa Mtandao huu alitinga Kituo cha Polisi cha Mji Mpya kilichopo jirani na Soko hilo la Mji Mpya kwa lengo la kutoa taarifa za tukio hilo, alipofika Muda huo wa saa tatu usiku alikuta kofuri likining’inia Mlangoni.

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...