Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 9, 2023

DENT WA LA 3 ALIYESOMBWA NA MAJI, MAMA AFUNGUKA MAZITO.

Hayati Sabrina enzi za uhai wake akiwa na Umri wa miaka 4 hadi mauti inamkuta alikuwa na Umri wa miaka 9.

Tumeradhimika kutumia Picha hii baada ya Mama yake kudai simu yake kubwa iliyokuwa na Picha nyingi za Mpendwa Mtoto wake imeharibika.

lnauma sana jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu Sabrina likiwa mbele ya Mashehe kwenye ibada ya kumuombe dua iliyofanyika nyumbani kwao
Mama Sabrina akizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Hashimu Bito akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi eneo la Makaburi ya Kolla.

Picha no 4 Bito akiaza kuandika jina la Dunstan Shekidele baada ya kupokea pesa ya mchango wa Muokoaji Juma Vigogo
 


       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Mama Mazazi wa Mtoto Sabrina Abdallah[9] aliyefariki dunia Desemba 6, baada ya kuteleza na kuzama kwenye Maji mengi ya Mto Morogoro, amefungua mazito  kifo cha Mwanaye.

Akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi jana Bi Hellena Abdallah  Maarufu Mama Sabrina  alieleza A-Z tukio hilo lililoondoa uhai wa Mwanae.

”Jana Desemba 6 Majira ya saa 8 mchana Mpendwa Mwanangu Sabrina alitoka shuleni nikamuandalia chakula alipomaliza kula Mvua ikanyesha mimi na yeye tukatoka nje kukinga maji ya Mvua.

 Mvua lipotaka mimi na Sabrina tukaingia ndoo hizo za maji ndani,wazazi wangu wanaishi Chamwino juzi alikuja Prinsess ambaye ni mtoto wa ndugu yangu lika lake ni kama Sabrina baada ya mvua kukata wakaniaga kwamba wanakwenda  kucheza na dada yake huyo mgeni”alisema Mama Sabrina na kuongeza.

“Kama unavyoona nyumba yetu ipo jirani kabisa na Mto Sabrina alimuambia dada yake huyo mgeni waenda Mtoni kutazama Maji yamejaa.

Walipofika Mwanangu aliteleza na kusombwa na Maji, nikiwa ndani na Ongea na simu Prinsess alikuja huku akilia na kuniambia Sabrina ametumbukia Mtoni nikakimbia kuelekea Mtoni  nilipofika sikumuona Mwanangu jinsia maji yalivyokuwa mengi sikuamini kama Mwanangu atakuwa hai.

Watu wakaingia majini kumtafuta baada ya lisaa hivi namuona Mwanangu analetwa na boda boda akiwa tayari amefariki”alimalizia kusema Mama Sabrina na kuangua kilio.

Naye Maneno Shabani ambaye ni Fundi Selemara katika Mtaa huo akizungumza na Mtandao huu alisema.

”Shekidele jana sikulala nimeweweseka usiku kucha, Mtoto Sabrina alikuwa akicheza hapa na wenzie baada ya Muda nasikia amesombwa na Maji wakati tunatafakari hilo nimeshuhudia anapitishwa hapa akiwa amepakatwa na Juma Vigogo kwenye boda bado huku shigo yake akiregea regea na tumbo kujaa maji huku akiwa tayari amefariki nilishindwa kujizuia nakaangua kilio”alisema Fundi huyo. 

Akihojiwa na Mtandao huu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro,Hashimu Bito alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye Mtaa wake.

Alipotakiwa kueleza tukio hilo na hatua alizochukua Mwenyekiti huyo alisema.

”Baada ya kupata taarifa nilipiga simu Faya walifika na kuzama kwenye Maji wakimtafuta Mtoto huyo bila Mafanikio, wakati Maafande wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji wakiendelea kumtafuta eneo hilo.

Mkazi wa hapa Mtaa Juma Vigogo alisema kutokana na kazi ya Maji Mtoto hawezi kuwepo hapa atakuwa huko bondeni, aliwaacha Maafande wa Faya wakiendelea kumsaka hapo Top Ten yeye kambia kuelekea bondeni alipofika  Daraja la Kichangani  kuna watu wanaosha osha Pikipiki na Magari pembezoni ya daraja hilo.

Wakamueleza  muda huu tumeona mguu wa mtoto ukielea juu ya Maji”alisema Mwenyekiti huyo na kuongea

Taarifa hizo zilimtia moyo  kakimbia hadi daraja la Mafisa Mzambarauni barabara kuu ya Moro-Dar baada ya kama  dakika 5 kamuona Sabrina anapita kazama kwenye Majia kamuopoa.

Baada ya kumuopoa Kakodi Boda boda kampakata na kuja naye hapa kamabaidhi kwa Maafande wa Faya,wakati anazama kwenye Maji viatu vya Juma Kigogo vilisombwa na Maji kaja hapa akiwa Pekupeku”alisema Mwenyekiti huyo.

Mwandishi wa habari hizi alimshauri Mwenyekiti huyo kichangisha Pesa Mtaa kumpatia Juma Vigogo kama asante lakini pia akanunue Viatu vingine na arejeshewe Pesa aliyokodi boda boda.

Mwenyekiti huyo msikivu alikubali wazo la Mwandishi akisema” Shekidele kwa vile umetoa wazo hilo basi wewe uwe kwa kwanza kuchangia na zoezi hilo naanza kulifanya hapa kaburini kabla ya watu hawajatawanika nipe karatasi na karamu”alisema Mwenyekiti huyo. Mwandishi alitoa kiasi cha Pesa sambamba na kumpatia karatasi na Karamu Pichani mwenyekiti huyo akianza kuandika jina la Du

Akihojiwa kwa njia ya simu leo Asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

lfahamike  Kutoka eneo aliliozama Mtoto huyo nyuma ya baa ya Top Ten  mpaka daraja la Mzambarani ni takribani umbali wa Mita elfu Mbili kwa maana ya Viwanja vya Mpira wa Miguu kama Jamhuri viunganishe 20.

 Kufuatia taarifa hizo Mwandishi wa Mtandao huu amemtafuta Muokoaji huyo Juma Vigogo ambaye hana mafunzo yoyote ya Uokoaji na kueleza mbinu alizotumia kumpata Mtoto huyo.

Clip Video ya Mahojiano ya shujaa huyo Mwamba Juma Vigogo na Mwandishi wa Mtandao huu itaruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu Muda wote.

                         

 

 



 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...