Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, December 20, 2023

MAPYA YA BIBI HARUSI ALIYEFARIKI DUNIA NJIANI AKIELEKEA ARUSHA KUFUNGA NDOA.


 

Noera akiwa ‘Location’ Siku ya Send Off yake ama kwa hakika alipendeza haswaa.

 Picha no Muonekani wa Gari lake mara baada ya ajari eneo la Mwanga.


      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Baada ya Bi, harusi Mteule hayati Rehema Chau Maarufu’Noera’kufariki dunia kwa ajari baada ya gari lake aliokuwa akiendesha  kutoka Morogoro kuelekea Arusha kugongana uso kwa uso na Lori eneo la Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Kwenye ajari hiyo Bi harusi huyo alifariki dunia Papo hapo pamoja na Mama yake Mzazi na Mfanyakazi wake wa kazi za ndani’House Girl’ huku dada yake akisalimika ingawa alijeruhiwa  maeneo kadhaa ya mwili.

lfahamike  Bi harusi huyo ambaye alikuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari SUA ya Mkoani Morogoro alipata ajari hiyo  Jumanne ya November 28 akielekea Arusha Kufunga ndoa na Mchumba’ke Bwana harusi Mteule Aman Moleni Jumamosi ya Desemba 2 siku 4 kabla ya kufunga ndoa.

Baada ya kutokea kwa ajari hiyo takrinani wiki mbili zilizopita wadau wengi wa Mtandao Pendwa wa Shekidele walisubini kwa hamu habari za  Chini ya Kapeti za  tukio hilo la kuhudhunisha bila mafanikio huku baadhi wakimpigia simu Mwandishi huyo wakisema.

”Shekidele tumesoma  habari za ajari ya Bi. hasusi lakini huko hatukushiba habari hizo tunasubiri kwako unayetupa habari zinazotushibisha, kila nikiingia kwenye Mitandao yako sioni habari hiyo kwa nini?”alisema mmoja wawadau wa Mtandao huu.

MAJIBU YA SWALI HILO KWA WADAU WOTE WA MTANDAO WA SHEKIDELE.

Nikweli toka ajari hiyo itokee sikuripoti chochote,hii ni kutokana na maumivu makali niliyoyapata juu ya kifo cha Mpendwa wetu Noera.

lngawa taarifa zote nilikuwa nazo lakini kila nikiwasha Lap Top nikitaka kuandika habari hiyo nasikia maumivu makali mwili mzima yaliyopelekea  kushindwa kuandika habari za Mpendwa wetu Noera.

Hii inatokana na ukaribu wangu na hayati Noera ambaye ni Mwanakwaya Mwenzangu KKKT Usharika  Mji Mpya,akiwa Mwimbaji Kiongozi wa Kwaya ya Sifuni huku Mwandishi wa Mtandao huu akiitumikia kwaya kuu ya Usharika huo.

Kila Mwaka kwaya zote za Usharika huo Mama KKKT Jimbo la Morogoro zinaungana kuunda kwaya ya Umoja inayowakisha Usharika huo kwenye Mashindano ya Kwaya jimbo la Morogoro.

Namshukuru Mungu kwa sasa maumivu yamepungua nimepata nguvu za kuandika habari za hayati Noera,kimsingi vyombo vingi vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii walianda sana habari za kifo hicho, hivyo sitarudia yaliyoandikwa kwenye vyombo hivyo vya habari.

Mbadara wake nitakupa habari mpya za hayati Noera ambazo hujawahi kuzisoma Popote na baadhi ya habari hizo nimeanza kuziweka hapo juu ya stori hii.

TICHA  REHEMA KAMA ALIKITABIRIA KIFO CHAKE.

Alhamisi Bi, harusi huyo Mteule baada ya kuvishwa pete ya Uchumba na Mchumba’ke Aman Moleni alifanyiwa sherehe ya kuagwa ‘Send Off’na Wazazi wake.

Send Off hiyo kabambwe ilifanyika Ukumbi wa Glonency uliopo Nane Nane Morogoro.

Wakati Wazazi wake wakimuandalia Send Off kwenye Ukumbi huo  siku hiyo hiyo Mchana hayati Noera alijiandalia Send Off yake ya Kiroho iliyofanyika ndani ya Kanisa ambapo wapendwa wake wa Kiroho tukiwemo wana kwaya wenzake, baraza la Wazee, waumini Wenzie na Viongozi wa dini kwa pamoja walishiriki Send Off hiyo iliyojaa utukufu wa Mungu.

Kipindi cha zawadi vikundi mbali mbali zilimkabidhi zawadi Bi. Harusi huyo Mteule na baada ya zoezi hilo kukamilika  naye kawaita mbele watumishi wote wa Usharika huo wakiongozwa na Mchungaji Dunia, Mwinjilisti Godfrey Nyange na Palishiweka wote aliwapa zawadi ya Vitenge vya Waksi.

Baada ya Send Off hizo mbili kutamatika Jumamosi Noera alitinga Ofisini kwa Mchungaji Dunia na kumueleza kwamba kesho jumapili kwenye lbada zote anataka kumtolea Mungu Sadaka ya Shukrani ya Pekee kwa kumjalia kupata ndoa aliyoitamani kwa miaka Mingi.

 Mchungaji huyo alimjibu” Hilo ni jambo zuri lakini nakushauri ungetoa sadaka hiyo baada ya kufunga ndoa jana tumekufanyia send Off tu ndoa yenye bado”.

Baada ya majibu hao Noera alimueleza Mchungaji kwa msisitizo.

”Mchungaji kuna kitu kinanisukuma nimtolee Mungu sadaka hiyo kesho kabla sijasafiri keshokutwa Jumanne.”

 Ushuhuda huo ulimgusa Mchungaji huyo ambaye alikubari ombi hilo, Jumapili Mpendwa wetu Noera akiwa na Mama yake Mzazi Bi Agnes Chao, dada yake na House Girl wake kwa pamoja walipita mbele na kumtolea Mungu Sadaka hiyo huku akisindikizwa na baadhi ya wanakwaya.

 Zoezi hilo lilipokamilika Jumanne Noera alifungasha kilicho chake kapiga gia gari lake na kuanza safari ndefu ya kuelekea Arusha na kwamba alipofika Mwanga alipata ajari na kufariki dunia, ambapo siku ya Jumamosi Desemba 2  siku ya kufunga ndoa iligeuka kuwa siku ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini Kwao Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro

Jumapili Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Mji Mpya aliwatangazi waumini  juu ya Kifo hicho ambapo kanisa zima liligubikwa na simani nzito baada kupokea taarifa hizo za kuumiza.

Baadhi ya waumini walishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi pale Mchungaji Dunia aliposema” Noera alikuja kwangu kuomba amtolee Mungu sadaka ya shukrani kwa kumpatia Mume nikamshauri afanye hivyo baada ya kufunga ndoa.

Akaniambia hapana kuna kitu kinamsukuma kutoa sadaka hiyo kabla hajaondoka nikamkubaria, nyote ni mshahidi jumapili alitoa sadaka hiyo, najiuliza nafsini mwangu kama ningeendelea kumkatalia asimtolee Mungu sadaka hiyo leo  moyo wangu ningeuweka wapi”alisema Mchungaji huyo kwa hisia kali kisha kainamisha uso wake chini na kukaa sekunde kadhaa bila kusema chocho.

Hali hiyo iliamsha tena vilio  kwa baadhi ya waumini.

Kwa sasa kumezuka Minong’ono Mingi juu ya Peke ya uchumba alivyovishwa hayati Noera na mchumba’ke Aman Molen kwamba amezikwa nayo au amerejeshewa kwa mchumba’ke huyo?.

 Kufuatia maswali hayo Mwandishi wa Mtandao huu jana alitinga Usharika wa Mji Mpya na kuzungumza na Mwinjilisti Godfrey Nyange  ambaye ametoa majibu sahihi ya swali hilo, majibu hayo yataruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

                                 


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...