Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 13, 2021

THE GUNNERS NDONDO CUP. NUGHUTU FC YANGINA NUSU FAINALI.

                          Kikosi cha Nughutu Fc kilichoanza jana
   Kikosi cha Bajaj Fc kinachomilikiwa na madereva wa Bajaj
Mastaa walioshiriki robo fainali hiyo jana huyu ni beki wa kutumainiwa wa Lipuli ya lringa Salum Rajab Jana aliitumikia Nughutu Fc

Kiungo 'Fundi' wa Gwambina Fc ya jijini Mwanza inayoshiriki Ligi kuu Said Gerald, jana aliitumikia Bajaj Fc ya SUA

Robo fainali hiyo ya The Gunners Ndondo Cup imechezesha na refa wa ligi kuu Raphael lkambi'Webb'

Morrison wa Simba kaamsha wengi, beki wa Nughutun akigadi wakati Mwamuzi Raphael lkambi akijianda kupima hatua, gemu ya Simba na Azam wakati Mwamuzi anazungumza na wachezaji wa Azam Madevu Bernard Morrison alibutua mpira akamkuta Konde Boy akitikisa nyavu akimuacha kipa wa Azam Kigonya akiinua mikono juu kama anapiga dua.licha ya wachezaji wa Azam kulalamiki kitendo hicho Refa alishikilia Msimamo wake akidai goma liende kati
           Heka heka uwanja jana kati ya Bajaj Fc na Nughutu Fc
                       IMANI ZA KISHIRIKINA SASA. 

Kiongozi huyu wa Bajaj baada ya kuna wachezaji wake wanakosa mabao ya wazi kwenye lango la Nughutu kipindi cha kwanza aliamu kutoka nje akanunua Chumvi ya Mawe akaimwaga kwenye lango la Nughutu. kama alivyonaswa na kamera za Mtandao huu. Kwa watu wenye lmani haba wanaamini chuvi inaondoa uchawi kwenye eneo lolote lile.


 Kiongozi huyo akiangua kicheko baada ya kubaini amenaswa na kamera za Mtandao huu " Shekidele kausha nifanye yangu"alisema kiongozi huyo


                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Nughutu Fc imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya Michuano ya The Gunners Ndondo Cup 2020-21.  

 

Nughutu kutoka Kati ya Kilakala imefanikiwa kufanya hivyo  jana  kwenye dimba ya Saba saba Mkoani hapa,baada ya kuitandika bira huruma timu ngumu ya Bajaj Fc kutoka Kata ya Magadu kwa bao 2-0.

 

Mastaa kibao wanaonekana kila siku kwenye michiano hiyo ya The Gunners ambayo kwa sasa ndio gumu kwenye mitaa mbali mbali ya Mkoa wa Morogoro. Mastaa walioonekana jana kwenye Robo fainali hiyo ni Kiungo hatari wa Gwambina Fc ya Misungwi Mkoani Mwanza Said Gerald ambaye kabla ya kujiunga na Gwambina ametokea timu ya daraja la tatu ya Changarawe ya Mzumbe Morogoro, akajiunga na Polisi Morogoro kisha akatimkia Coastal Union ya Tanga na sasa yuko Gwambina.

 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana Said alisema”Mkataba wangu na Gwambina unakwisha Msimu huu kwa sasa kuna ofa nyingi zimekuja hivyo naweza kusalia Gwambina au kaondoka”alisema Said ambaye kwa jana aliitumikia Bajaj Fc.

 

Staa mwingine aliyenaswa na Mtandao huu ni beki kisiki wa Lipuli ya lringa Salum Rajab’ a.k.a Ali Ali mchezaji huyo kabla ya kujiunga na Lipuli ametokea Changarawe ya Mzumbe iliyoshiriki ligi daraja la tatu Mkoa wa Morogoro.

Baada ya ligi hiyo kukamilika kwa timu ya Jeshi kikosi cha 515 Kutwaa ubingwa huo walivutiwa na kiwango cha Salum na kumvuta kwenye timu yao.

 

Wanajeshi hao kutoka kambi hiyo ya 515 iliyopo Kinonko Bwawani waliposhiriki ligi ya shirikisho inayozaminiwa na Azam Media nilipokwenda kucheza mkoani lringa na mabingwa wa ligi daraja la tatau Mkoa wa lringa Viongozi wa Lipuli walivutiwa na kiwango cha Salum na kuamua kumsajiri.

 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi mara baada ya kukamilika kwa Mchezo huo wa jana Salumu alisema” Kweli Kaka nilipotoka timu ya jeshi nilijiunga ana Lipili kama unavyojua kwenye Play Off  Pan walitufunga Dar bao 3-0 na walipokuja lringa tukasuluu hivyo Lipuli imeshuka daraja la Pili. Kwa sasa nimepta dili ya kujiunga na timu ya daraja la kwanza ya Fountain gate ya jijini Dodoma”alisema Salumu ambaye kwa jana aliitumikia timu ya Nughutu Fc. 

 

Staa mwingine ni Mwamuzi wa ligi kuu Tanzania bara Raphael lkambi’Webb’ ambaye juzi kati ndiye aliyechezesha nufu faina ya kombe ya Shirikisho FA Cup kati ya Yanga na Biashara ya Mara gemu ikipigwa uwanja wa Alhj Ally Hassan Mwingi Tabora.  

 

Katika robo fainali ya Jana ilichezeshwa vizuri na refa huyo Mkazi wa Mawenzi Morogoro. Kutokana na Ukubwa wa Michuano hiyo ya The Gunners Robo fainali zote zimechezesha na marefa wa ligi kuu, ambapo Robo fainal ya kwanza iliyolala kati ya Wakushi Fc na Black Viba ilichezeshwa na Ally Mnyupe ambaye juzi alichezesha gemu ya Simba na Coastal Union, Robo fainal ya pili kati ya Moro Kids na Salange imechezeshwa na refa bora wa ligi daraja la kwanza Msimu huu mwana dada Amina Kihondo.

            ROBO FAINALI YA NNE INAPIGWA LEO. 

Waluguru wanasema’Kigira Mwali Kivika’ maana yake siku ya kumnema Mwali imefika. Sio ile siku yetu ya tarehe 25 Kigoma moto mwingine ni leo kati ya watani wa Jadi wa ndondo Cup mkoa wa Morogoro Black People’Taifa la watu weuzi’ kutoka Kata ya Mji Mpya watakipiga na Matajiri wa soko Mkoa wa Morogoro Chadongo Fc kutoka Kata ya Mwembesongo.

 

lfahamike kata hizo ni jirani zinapakata hivyo kutokana na jeuzi ya pesa ya Chadongo asilimia 50 ya wachezaji wa Chadongo wanatoka Black People. Kufuatia hali hiyo Mtandao huu umetinga Maskani ya Black People kufanya upepelezi wachezaji gani wakali watawatumia kufuatia nyota wao kutekwa na Chadongo.

 

Kiongozi mmoja wa timu hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema

 

”Shekidele sisi ni taifa kubwa Chadogo kachukua nyota wetu wote leo njoo Saba saba  uone watu labla nikuibia siri kwa kuwa wewe ni wa Mji Mpya mwenzetu tunamshusha Salum Machaku na Poul  Yule Rasi aliyewahi kuchezea Polisi Moro.

 

Muda huu Mwandishi wa Mtandao huu anajiandaa kuelekea uwanja wa Saba saba kukusanya matukio yote yatakayojiri hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...