Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 12, 2021

HII KALI REFA CHEZEFA MASHINDANO YA SOKA NA MTANDIO KICHWANI.

Mwamuzi bora wa ligi daraja la kwanza Tanzania Bara Msimu huu Bi,Amina Kihondo akiwa na Mtandio uwanjani juzi
.....Waamuzi wakiwa na manahodha wa timu za Moro Kida na Black Viba
......Amina akizozana na mahodha wa Moro Kids Bonifasi akilalamika Kipa wake kumizwa, anasuhuluhsi bifu nilo  wimba wa Salange Fc Salum Kihimbwa 'Chuji' ambaye pia ni mchezaji tegemo wa Mtibwa Sugar
 

 

                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MWAMUZI Bora wa ligi daraja la kwanza Tanzania Bara msimu huu Amina Kihondom ljumaa iliyopita amechezesha robo fainali ya Michuano ya The Gunners Ndondo Cup huku akiwa amejifunga mtandio kichwani.

 

Amina aliyechezesha Vizuri Robo fainali hiyo kati ya Salange na Moro Kids, ndiye aliyechezesha daby ya Ligi kuu ya wanawake kati ya Simba na Yanga iliyokamilika kwa Simba kuinyuka Yanga bao 3-0.

Vile vile Amina ndiye aliyechezesha fainali ya ligi daraja la kwanza mwezi uliopita kati ya Mbeya Kwanza na Geita Gold gemu hiyo ilipigwa Uwanja wa Uhuru Temeke Dar es salaam na Geita kuitandika Mbeya kwanza bao1-0. Mara baada ya gemu hiyo kukamilika Uongozi wa TFF Taifa ulimtangaza  Amina Kihondo kuwa Mwamuzi bora wa ligi hiyo Msimu huu huku mshikakibendera bora pia akitokea Mkoani hapa.

 

Mara baada ya gemu hiyo ya Ndondo Cup iliyopigwa uwanja wa Saba saba  kukamilika Mwandishi wa Mtandao huu alimfuata Amina na kumuliza sababau za kuchezesha gemu hiyo akiwa na Mtandio kichwani tofauti na tunavyomshuhudia kwenye Luninga akichezesha mechi kubwa za Ligi alijibu.

 

”Shekidele bhana na hii nayo ni habari? Mwandishi alimjibu ndio ni habari naomba majibu Amina ambaye kiasili ni Mnyalukoro kutoka lringa  alisema. “lnaruhusiwa kuchezesha na Mtandio ila ufanane na jezi uliovaa kama ambavyo unaona unafanana ne jezi hii”,  Mwandishi- Mbona ulivyochezesha gemu ya Simba na Yanga na ile ya fainali ya ligi daraja la kwanza mbona hukuvaa Mtandio kwa nini uvae leo?

Amin- Leo ljumaa nimetoka Msikitini bado ninaudhu ndio maana  nimevaa Mtandio pamoja na taiti ndefu iliyoficha mapaja’ .

 

Mwandishi- Ok kwa majibu hayo sina swali na ziada zaidi nikupe hongera kwa kiwango chako bora cha uchezeshaji ulistahili kuwa Mwamuzi bora lai yangu usibweteke na mafaniko hayo pambana uvae beji ya FIFA.

 

Amina. Asante kwa pongezi na ushauri mzuri.  


Mwandishi-  Swali la Mwisho Mtandio huu uliojisokota shigoni si hatari, kwani hii ni michuano ya ndondo Cup unaweza kuvamiwa na mchezaji au shabiki akatumia mtandio huu kama silaha ya kukakaba shigo na kukudhuru.

 

Amina Hapana siku zote mimi natenda haki kwenye kazi hii ya uamuzi ingawa manung’oniko hayakosekani kwa wachezaji na mashabiki pia sivai Mtandi mara kwa mara niwapo uwanjani.         

   MAJIBU YA KAMATI GEMU 2 ZILIZO LALA 

Leo nimefanikiwa kuzungumza na kaimu Mratibu wa Michuano yenye msisimko wa The Gunner Ndondo Cup Mrisho Chuchunge ambaye amesema kamati imeamua michezo hiyo kurudiwia ambapo Jumatano  Salange watakipiga na Moro Kids na ljumaa Black Viba watakipiga na Wakushi.

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...