Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 10, 2021

ROBO FAINAL NDONDO CUP, GEMU YA MORO KIDS NA SALANGE KIPORO.

                                                               Kikosi cha Moro Kids

       Kikosi ch Salange Matajiri wa Stend ya Mabasi Msamvu, wakiwa na shabiki wao aliyejiita Mzee Mlipili wa Salange
Wingatajari wa Sangale Fc Salum Kihimbwa 'Chuji' anayekipiga Mtibwa Sugar akiwatoka Mabeki wa Moro Kids.
                                                            ......Chuji akipiga Krosi
.....Kihimbwa akigongna na Kipa wa Moro Kids ahata hivyo alishindwa kufunga bao akiwa yeye na gori

                                                   ......Kipa wa Moro Kids akinyaka Mpira








 

.

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

ROBO fainali ya Pili ya Michuano ya The Gunners Ndondo Cup Kati ya Salange Fc na Moro Kids Imelala tena  baada ya timu hizo kutoka sale ya 0-0 na ilipoamuliwa  Mikwaju ya Pelnaty Salange waligoma hivyo Mwamuzi Amina Kihondo alimaliza mchezo huu.

 

Mara baada ya gemu hiyo kutamatika ‘kimagumashi’ kundi la Mashabiki liliwavamia waamuzi wakilalamikia Michezo hiyo ya Robo fainali kutopatikana kwa mshindi ili hali wao wamelipa vingilio vyao kuona mshindi anapatika na sime mechi kulala kila siku.

 

Hii ni mara ya tatu kwa mechi kulala ambapo katika hatu ya awari ya 16 gemu ya Black People na Miembe 3 timu anayoitumikia mchezaji chipukizi wa timu ya Taifa ya Tanzania Nickson Kibabage ililala baada ta timu hizo kutoka sale ya bao 1-1 na zoezi la pelnaty lilikwama baada ya giza kutanda uwanjani.

 

Juzi kwenye robo fainal ya kwanza kati ya Black Viba na Wakushi pia gemu hiyo ililala kiporo baada ya kipa wa Viba Gumbo Mfaume kukataa kuendelea kudaka akidai giza limetanda.

 

Robo fainal ya Pili iliyopigwa jana kati ya Salange Fc inayomiliki na Mawakala wa mabasi kituo cha Msamvu na Moro Kids inayomilikiwa na Kituo cha kuibua na kukuza Vipaji cha Moro Youth ililala baada ya salange kugomea kupiga Pelnaty wakidai giza limetanda.

Katika gemu hiyo ya Jana Mtandao huu umekusanya matukio kibao yakiwemo ya Mwamuzi Amina Kihondo kuchezesha Michuano hiyo akiwa na hijabu kichwani mwenyewe afunguka ataja dini yake.

 

Tukio la Pili Mshambuliaji tegemeo wa Mtibwa Sugar Salum Kihimbwa ‘Chuji’ kamvunja Mkono beki kisiki wa Moro Kids Shabani Shishimbi ambaye alikimbizwa hospital na Usafiri wa boda boda.

Akizungumzia sintofahamu hiyo ya mechi kulala  Kaimu Mratibu wa Michuano hiyo Mrisho Chuchunge alisema kamati ya Mashindano itaketi leo Jumamosi saa 5 kutoa maamuzi ya mechi hizo pili baada ya kupokea ripoti za Waamuzi na Makamisaa.  

       MAONI YA MTANDAO HUU.  

 Mwandishi wa Mtandao huu amebaini kasoro zinazopelekea baadhi ya michezo ya michuano hiyo kutokamilika.

 

Mosi. Mechi hizo za mtoano zinachelewa kuanza kila siku zinaanza saa 11 kasoro.

 

Pili Waandaji wanashindwa kusimamia kanuni za mashindano yao jambo linalopelekea timu ikiona haina wapigaji wazuri wa pelnaty inatoa timu uwanjani kwa kisingizio cha giza.

 

Ngoja tuone waandaji hao watakuja na majibu gani juu ya gemu hizo mbili zilizolala, mtandao huu unafuatilia kikao hicho kwa lengo la kuripoti majawabu yatakayotolewa na Kamati hiyo kama gemu hizo zitarudia au timu iliyogomea pelnaty itaondolewa kwenye mashindano.

 

Robo fainali ya tatu itapigwa Jumatatu kati ya Bajaj Fc na Wakutu Fc na Robo fainali ya Mwisho itapigwa Jumanne kati ya Black People’ Taifa la Watu Weusi kutoka Kata ya Mji Mpya watakipiga na Chadongo kutoka Kata ya Mwembesongo.

.

No comments:

Post a Comment

JUMBE WA LEO.

          “Ukichoka kutembea na Dunia. Dunia haitasimama kukusubiri.”   Pichani   Dunstan Shekidele akitembe na Dunia Wilaya   mbali...