Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, July 9, 2021

DIWANI MSUYA AFANYA BALAA MICHUANO YA NDONDO CUP.

                                   Kikosi cha Black Viba kilichosheheni wachezaji wa Mtibwa  B

Kikosi cha Wakushi Kikiongozwa n mchezaji wa zamani wa Simba Mohamed  Kijiko wa                 tatu kutoka kulia waliosimama

Diwani wa Kata ya Mbuyuni Mh Samwel Msuya kulia akiingia uwanja jana akiwa na Rais wa Black Viba Charles

        Mh Msuya mwenye miwani akizungukwa na wananchi wake wa kata wa Mbuyuni wakifuatilia       mchezowa robo fainali kati ya timu yao ya Black Viba na Wakushi.
                         Warembo wakiingia Uwanjani  kushuhudia robo fainal ya ndondo Cup

Kigogo wa timu ya Black Viba Rama Mboto' Bonge' na Musa Nabi kulia wakichangisha pesa ya maji kwa wachezaji wao
Mratibu Mkuu wa Michuano ya The Gunners Ndondo Cup Seleman Mpemba 'Sele The Gunners' wa Mwisho Kushoto akiwa na Viongozi wa Bajaj Fc wakifuatilia mchezo wa Robo fainal ya kwanza jana kwenye uwanja  wa Saba saba kati ya Black Viba na Wakushi Fc
Heka heka uwanja  Mshambuliaji wa Wakushi Omary Chipo Kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki kisiki wa Black  Viba Nasry Scobber ambaye pia ni beki wa Mtibwa B



Kiba wa Viba Mfaume Gumbo ambaye pia ni Kipa namba Moja wa Mawenzi Market akinyaka shuti la Ras





 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

WAKATI Kampuni ya Azam Media jana imefanya balaa la kuimwangia  Yanga Mabilioni ya Pesa, naye Diwani wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro Mh Samwel Msuya jana amefanya balaa kwenye michuano ya Ndondo Cup.

 

Mh Msuya anayeiongoza Kata hiyo kwa kipindi cha  tatu mfurulizo kwa leseni ya CCM amefanya hivyo kufuatia kukubalika na wananchi wa kata hiyo.

 

Jana aimefanya kufuru kwenye Michuano ya Ndondo Cup inayoendelea Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro, baada ya timu yake ya Black Viba kutoka maeneo ya Vibandani Kata ya Mbuyuni kufanikiwa kutinga hatua ya Robo fainari ya Michuano hiyo ya The Gunners Ndondo Cup.

 

Baada ya Vijana wake  kutinga hatua hiyo ya robo fainali Mh Msuya jana alishusha kikosi kizima cha Mtibwa B kilichotwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara kwa Vijana wa umri chini ya Miaka 20’Under 20’Mwezi uliopita.  

 

Katika robo fainali hiyo ya kwanza Viba ilikipiga na Majirani zao Wakushi Fc kutoka Kata ta Mafiga ambapo gemu hiyo imelala kiporo baada ya timu hizo kutoka sale ya 0-0 na walipoingia kwenye mikwaju ya Palnaty pia walitoka sale kwa kufungana Pelnaty 4-4 huku kila timu ikokosa Pelnaty Moja.

 

 Zoezi hilo la upigaji penalty lilikwa kwenye hatua hiyo baada ya kiza kutanda uwanjani hapo hivyo waandaji wapatanga siku nyingine gemu hiyo kuludiwa.

  

Robo fainali ya Pili itaendelea leo kwa Mchezo Mkali kati ya Mataji wa Stend ya Mabsi ya Msamvu’Salange Fc watakapokipiga na Moro Vipaji timu ya Moro Kids inayoongoza kwa kutoa wachezaji wengi wa ligi kuu ligi daraja la kwanza na ligi daraja la Pili nchini huku wachezaji wote wa Mtibwa B waliocheza jana wanatokea Moro Kids.

 

 Timu nyingine zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo ya robo fainali ni Black People  kutoka Kata ya Mji Mpya, Bajaj Fc kutoka SUA Kata ya Magadu na Wakutu Fc kutoka Kata ya Kilakala na Chadongo Fc kutoka Kata ya Mwembesongo.

 

Katika Michuano hiyo Mwandishi wa Mtandao huu mara zote anamshuhudia Diwani wa wa Kata ya Mbuyuni Pekee anayeambatana na timu yake akiitendea haki ilani ya CCM ya Viongozi  kusimamia michezo kwenye Kata zao.

 

Mratibu Mkuu wa Michuano hiyo Seleman Mpemba Maarufu ‘Sele za Gunners’anayemiliki duka la Vifaa vya Michezo mkoani hapa la The Gunners World Sports’anawaalika mashabiki kujitokea kushuhudia michuano hiyo kwa kiingilio cha shilingi elfu 2.

 

lfahamike Sele Mpemba ni Mtoto wa  Makamo wa Pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh Balozi Seif ldd.

 

Shekidele Blog itarusha hewani matokeo na Picha za matukio ya Michuano hiyo kuanza hatua hiyo ya Robo fainali Mpaka fainali hivyo endelea kuwa jirani na www.shekideletz.blogspot.com Muda wote.


 

No comments:

Post a Comment

MENEJA TANESCO ASIKIA KILIO CHA WANANCHI.

Lori la Tanesco likiwani huku likiwa na lundo la mafundi               Lori la pili likiwanini na nguzo mbili za kisasa ........Mafunsdi wak...