Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 5, 2021

PONGEZI NYINGI KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUFUNGULIA BLOGS.


Licha ya Ulemavu wake Matma alishiriki kwenye ujenzi huo ikiwemo kubeba misuko ya Saruji kutoka dunika mpaka nyumbani kwake au Site
                   Nikimkabiidhi Pesa zilizo tumwa kwenye simu yangu kutoka nje ya nchi

Hayari Mzee Hussein[Kulia] akichora mchora wa nyumba hiyo huku Mmilkiki wa Matama akishuhudia
Mwandishi wa Mtandao kama ilivyo kwa Matama naye alishiriki kufanya kazi kwenye ujenzi wa nyumbani hiyo Pichani akishriki kichimba Msingi.
....Kamwe hatukupoa kwenye harambee ya uchangiaji Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro RPC Urlch  Matei baada ya kuguswa ha bahari za Matama naye alichangia kiasi cha Pesa
                         Matama akizama kwenye dimbwi la Maji Machafu akielekea Msalamani
 
 
Bi Mausa Said akimsaidi akimfungulia Mlango Mume wake ili aingia Msalani.

       Mjengo wa Mtama ukiwa hatua za Mwisho Mwisho kukamilika



                                           Matama akipanga matofari kweny Mjengo wake


 

                                              Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

NATOA shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya Sakafu ya Moyo wangu zimfikie Mama yetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mtetezi wa kweli wawanyonge kwa kufungulia Blogs zote bila mashati yoyote.

 

Niliposikia kauli hii nilifurahi  sana kama ambavyo niliumizwa sana siku ambayo serikali ya awamu ya 5 ilivyotangaza kuzifungia Blogs zote kwa maelezo ya kulipia ada ya million Moja.

  

                                            NIANZE  NILIVYOUMIZWA.

 

lfahamike kwamba Lengo kuu la Blogs hii ya www.shekidetz.blogspot.com ni Sauti ya wasio na Sauti, Msaada kwa wanaohitaji Msaada.

 

Kupitia taaluma yangu  ya Uandishi wa habari kupitia Mtandao huu nimewasaidi wengi kama maandiko ya kitabu kitakatifu cha Biblia Marko 10-45 yanavyo sema.

 

“Kwa Maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa bali kutumika na kutoa Nafsi yake iwe faida ya wengi, Kuponywa kwa Kipofu Bartimayo”.

 

Kupitia taaluma yangu ya Uandishi wa habari nimewasaidi wengi kupitia Mtandao huu miongoni mwao ni Mlemavu wa Miguu Mohamed Athuman Matama.

 

Mwaka 2017 nilimtembelea Matama nyumbani kwake Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, msimu wa Masika mwezi wa 3.

Ni kama mipango ya Mungu nilipofika kwenye nyumba hiyo aliyopanga nimemkuta Matama akisindikizwa chooni na Mkewe Bi, Maua Said.

 

Choo hicho kilikuwa mita kama 10 kutoka kwenye chumba cha uali alichopanga na kuelekea kwenye choo hicho, njiani  kulikuwa na dimbwi kubwa la Maji ya Mvu ambapo mwenye nyumba pamoja na wapangaji wengine waliweka kidaraja kwa lengo la  kulikwepa dimbwi hilo kwa vile walikuwa na Miguu timilivu.

 

Kwa ndugu yetu Matama ambaye hakuwa na timilivu kwake ilikuwa changamoto aliradhimika kuongelea kwa mikono kwenye dimbwi hilo la Maji Machafu kuelekea Msalani huko nako alikumbana na tole lililochanganyika na kinyesi kufuatia choo hicho kutoezekwa juu na kutosakafiwa chini.

 

Tukio hilo liliniumiza sana hivyo nikajikuta naongozwa na roho Mtakatifu kumpiga Picha wakati akipiga mbizi kwenye dimbwi hilo kuelekea chooni kisha kupitia Picha hizo niwashirikishe wananchi wenye Mapenzi Mema ili kwa pamoja tumjengee nyumba Mpendwa wetu huyo aepukane na kadhia hiyo.

 

Kwa miujiza ya Mungu wadau wengi wa Mtandao huu  pande zote za dunia waliguswa na picha hizo pamoja  na simulizi ya tukio hilo na kuamua kuniunga mkono kwenye harambee Maalumu ya kumjenge nyumba ndugu yetu Matama kupitia mtandao huu wa www.shekideletz.blogspot.com.

 

Mwitikio ulikuwa mkubwa ambapo miezi 2 mbele tulifanikiwa kupata pesa za kununua Kiwanja maeneo ya Kichangani na mwezi wa 12 mwaka huo huo wa 2017 tulianza ujenzi ambapo baadhi ya mafundi walijitolea kufanya kazi hiyo bure akiwemo Mzee Husein aliyejitolea kudizani nyumba hiyo kwa kuchora Ramani kujenga boma la nyumba hiyo bure, alichoomba kwetu ni nauli na chakula yeye na wasaidizi wake wakati wa mchana. Pia kwa niaba ya Matama naendelea kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna yoyote ile kufanikisha ujenzi wa nyumba hii sisi hatuna cha kuwalipa ila mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema yeye ndiye ambaye atawalipa.

 

Mungu kupitia maandiko yake anasema “Mtu akimsaidi Mja wangu wenye shinda amenikopesha Mimi nami nitamlipa mara dufu’

 

Wakati nyumba hiyo ikiwa usawa wa Madirisha lnjinia Mzee Husein alifariki dunia akiwa bado hajamaliza msaada wake huo, tunaamini Mungu atampatia dhawabu zake timilivu kwa moyo wake huo wa huruma.

 

Nilitafuta fundi mwingine ambaye alituchaji pesa ya ufundi wa kukamirisha kazi hiyo,boma hilo  lilipokamilika wakati naendelea na harambee ya kununua mabati ya kupaua nyumba hiyo.

 

Katikati ya zoezi hilo serikali ya awamu ya 5 ilitoa agizo la Blogs zote kufungwa huku yakitoka maelekezo kwamba anayehitaji  ajisajiri TCRA kwa gharama ya Milioni Moja kwa vile sikuna kiasi hicho cha Pesa na kwa vile natii amri za serikali yangu niliufunga Mtandao huu.

 

Nilifunga Blogs hii ili hali  sijakamirisha hadhima yangu ya kuendeleza harambee ya kukamilisha nyumba ya ndugu yetu Matama nakumbuka siku moja nikiwa bafuni naonga nilipokumbuka jambo hilo machozi yalitoka nikimkumbua Hayati Mzee Huseni aliyeaga dunia kabla hadhima yake haijakamilika na Mtandao wangu kufunga kabla hadhima yangu pia haijakamilika.  

 

Baada ya mwezi mmoja Mtandao huu unaofuatiliwa na watu wengi pande zote za dunia kutoonekana hewani watu wengi walipiga simu kuniulizia niliwaeleza hali hali wakaelewa lakini kuna Mdau Mmoja Mtanzani anayeishi Marekani Henery Challo niliongea naye kupitia Mtandao wa Watsap alisema

 

” Du watanzania wengi tuoishi huku Marekani kila siku tulikuwa tukifuatilia Mtandao wako binafsi nisipoperuzi Mtandao wa shekidele nahisi kama sijashiba habari, tulikuwa tukizipata habari za huko nyumbani kwa kina kupitia Mtandao wako.

 

Ahadi yangu kwako Bwana Shekidele nitawahamasisha watanzani wenzangu huku Marekani tukupatie hiyo Milion ukalipie TCRA na kama wakikata nitauza hata mataili ya gari langu nikupe hiyo Pesa ili uendelee kuwasaidia wanyonge na sisi tulio bali na nyumbani uendelee kutuhabarisha yanayojiri huko"alisema Mtanzani huyo Bw. Challo.

 

Changamoto, kabla hadhima ya Challo haijatimia Mama yake Mzazi aliyekuwa akiishi Mitaa ya Sultan Area Manispaa ya Morogoro alifariki dunia ambaye alipunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele kijijini kwao Mpwapwa Mkoa Dodoma.

 

Mungu ni Mwema licha ya Mtandao huu kutokuwa hewani kuna baadhi ya wananchi waliendelea kutuma Michango yao na hatimaye kwa Rehema za Mwenyezi Mungu tulikamilisha nyumba hiyo na sasa Mpendwa wetu Matama yeye na familia yake wameshahamia kwenye Mjengo huu kira ‘kiyoyozi’ huku chumba chake kikiwa Master Choo ndani.      

                      FURAHA.

Wiki iliyopita serikali ya awamu ya 6 chini ya rubani mahiri Rais Mama Samia aritangaza kufungulia Blogs zote na kufuta tozo zote ikiwemo Usajiri na kiasi hicho cha pesa Milioni Moja.

 

Mimi nilibakatika kusikia habari hiyo kwenye kituo Kimoja cha redio kupitia Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh lnnocent Bashungwa niliposikia taarifa hizo  nilifurahi sana nikaangua kicheko cha furaha kiwa peke yangu kama mtu aliyepagawa.

 

Kwa niaba ya wadau wote wa Mtandao huu wa ndani na nje ya nchi tunamshukuru sana Mama Samia Suluhu ambaye kwa utawala wake wa siku 100 tumeshuhudia akiongoza nchini kwa Hekima, hofu ya Mungu, Utawara Bora ahadi za kweli na kuwatete wa nyonge kwa vitendo.

Binfsi Mama Samia sina cha kukupa zaidi ya kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akuepushe na mabaya, akupe afya njema ili uweze kuwatumikia wananchi,  zawadi yangu kwako itakuwa kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi wowote ambao nikiliona jina lako na sura yako ya Upendo wa kweli kwa watu wako watumbukiza kura yangu ya ndio kwenye  boksi hilo.

                                                                  HITIMISHO

Wadau wa Mtandao wa Shekidele Mama kaurudisha hewa sasa kazi inaendelea kwa kasi ile ile ya awari kikubwa kila siku usikose kutembelea www.shekideletz.blogspot.com kwa habari moto moto.

No comments:

Post a Comment

WANANCHI WAELEZA SABABU TANESCO KUSUASUA KUBADILISHA NGUZO.

       Na Dustan Shekidele,Morogoro. IMEFICHUKA. Wananchi Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, wamefichua siri ya Tane...