Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, July 4, 2021

MASHABIKI WA YANGA WATINGA TAWI KUU LA SIMBA USIKU HUU.

 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 
Mara baada ya gemu ya watani wa Jadi Simba na Yanga kukamilika usiku huu kwa Yanga kuwanyuka Simba Simba 1-0 kwenye uwanja wa Mkamba mbele ya Rais Samia Suluu Hassan.
Kundi la Mashabiki wa Yanga wake kwa waume watoto kwa wazee, Muda huu wamelizingira tawi kuu la Simba la Mkoani Morogoro Maarufu tawi la Shujaa lililopo Pande za Mji Mpya Mkoani Morogoro, wakishangilia ushindi wa timu yao. 




 
 
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye muda huu yuko eneo la Tukio Live licha ya vijembe walivyotupiwana mahasimu wao Wanachama na Mashabiki wa Simba wanaendelea kuonyesha ustaarabu wa hali ya juu wa kutowajibu wala kuwafanyia vulugu mashabiki hao wa Yanga.
Baada ya kuona hawajibi Muda huu kundi hilo la Yanga linaondoka kwenye Tawi la Simba likielekea kwenye Tawi lao ya Yanga lililopo Pia Mji Mpya jirani na Stend ya Daladala. 
 
Mtandao huu unawapongeza Wanachama na Mashabiki hao wa Simba kwa uvumilivu wao ambapo licha ya machungu ya timu yao kuvungwa lakini pia wameweza kuvumilia machungu ya maneno ya shombo walioshushia na watani zao hao wa jadi waliowavuata kwenye tawi lao. 
 
Muda huu Mwandishi wa Mtandao huu anakimbia mchaka mchaka na kundi hilo la Yanga akiendelea kukusanya matukio hivvyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
Ila ninachokiona cha hatari ni madereva wa boda boda wanavyoendesha kwa kasi pikipiki zao kwenye msitu huu wa watu.

No comments:

Post a Comment

JUMBE WA LEO.

          “Ukichoka kutembea na Dunia. Dunia haitasimama kukusubiri.”   Pichani   Dunstan Shekidele akitembe na Dunia Wilaya   mbali...