Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, July 15, 2021

MICHUANO YA NDONDO CUP,BEKI WA MORO KIDS AVUNJWA MKONO NA MSHAMBULIAJI WA MTIBWA SURAR.

Salumu Kihimbwa akishirlikiana na Viongozi wa Moro Kids kumpa huduma ya kwanza beki wa Moro Kids Shabani Shishimbi aliyevunjwa mkno kwa bahati mabya na Kihimbwa. wakati wakigombea mpira wa juu
Baada ya kokosekana gari la wagonjwa uwanjani bonda boda alijitolea kuingia uwanjani kumbeba majeruhi huyo kwa lengo la kumkimbiza hospital
Mshambuliaji wa Salange Kipira ambaye misimu ya nyuma  walicheza timu Moro na Shaban Pum Fc ya Kichangani akimpa Pole kwa dhahama aliyoipata
Kiongozi wa Moro Kids akimfariji Mchezaji wake aliyevunjika mkono wakati akiitumikia timu hiyo ya Moro Kids inayoongoza nchini kwa kutoa wachezaji wengi nyota wanaotamba kwa sasa timu kubwa za Simba Yanga na Azam
Shabani akitoka uwanjani kuelekea kwenye boda boda yake huku akiwa amepatiwa huduma ya kwanza ya kuvungwa bendeji na Vigogo vya Miti

 Mwamuzi Kassim Salehe Boko akimkimbiza Shabani hospital

 

 

                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

BEKI kisiki wa timu ya Moro Kids Shabani  Shishimbi, amevunjwa mkono wa kulia na mshambuliaji hatari ya Salange Fc Salum Kihimbwa’Chuji’ ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo wa Mtibwa Sugar inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

 

Toka gemu hiyo ya robo fainali ya Michuano ya The Gunners ndondo Cup inaza beki huyo alitembea na Kihimbwa anayeongoza kuipachikia mabao Mtibwa asitikise nyama za timu yake.

 

Dakika 81 nje kidogo ya lango Moro Kids Shaban na Kihimbwa waliruka hewani kugombea Mpira Chuji akitaka kufunga kwa kichwa na Shishimbi alimthibiti asifunge.

 

Beki huyo alifanikiwa kuondoa Mpira huo na kwamba wawili hao walianguka chini na kwa bahati mbaya Shabani aliangukia Mkono huku Kihimbwa akimlalia kwa juu.

 

Ghafla kihimbwa baada ya kushuhudia mkono wa Shabani umevunjika alishika kichwa kwa uchungu huku akipiga kelele za kumwalika Daktari aingia uwanjani.

 

Daktari na Viongozi wa Moro Kids waliingia uwanjani na kutoa huduma ya kwanza ya kunjoosha Mkono huyo kasha kuvunga kamba na Vijiti  kufuatia kukosekana gari la wagonjwa uwajani hapo dereva mmoja wa boda boda alijitolea kuingia uwajani kwa lengo la kumkimbiza hospital mchezaji huyo.

 

Kwa vile Mwandishi wa Mtandao huu anamfahamu vyema mchezaji huyo anayemiliki pia boda boda alimuamulu kutoa funguo ya pikipiki yake na kumkabidhi Kasimu Saleh Boko aliyepiga gia na kumkimbiza hospital.

 

Shaban, Kasim na Mwandishi wa Mtandao huu yoye wanaishi jirani maeneo ya Mji Mpya.

 

Siku iliyofuta Mwandishi wa Mtandao huu alitinga nyumbani kwa Shabani kwa lengo la kumjulia hali ambapo Mama mwenye nyumba wake alipoulizwa alisema

 

“Tunashangaa Shaban hajaludi hapa nyumbani toka jana mchana chumba chake kile pale kimefungwa”

 

Mwandishi alimjulisha kwamba mpangaji wake huyo amevunjika mkono akiwa uwajani akiitumikia timu yake ya Moro Kids.

 

Bi Mkubwa huyo alishangaa huku akisema” ndio maana hakuludi hapa kaenda kwa wazazi wake ngoja nimpigia simu nijue kinachoendelea”alisema Mama huyo.

Mwandishi huyo pia alitupia Picha ya shabani kwenye Group la Whatsap la Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro ambapo baada ya wadau kuona Picha  hiyo waliguswa na kushauri Uongozi wa Goup hilo uweke mkeka wa kumchangia mwanasoka huyo.

 Uongozi wa Chama Cha Soka Manispaa ya Morogoro’MDFA’ kwa vile ni wasikivu walipokea Ushauri huo na sasa michango inaendelea kwenye Group hilo.

 

Kesho Mwandishi wa Mtandao huu atatinga tena nyumbani kwa shabani kwa lengo la kumjulia hali sambamba na kujua maendeleo yake kwa sasa hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.


No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...