Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, July 11, 2021

MSIKITI WA SHULE YA WASICHANA MORO WATEKETEA KWA MOTO.

Msikiti wa At Tauun Mji Mpta ukiendelea kuteketea kwa Moto jana kulini na Mabweni ya Madent wa Kike wa shule hiyo  ya Sekonderi ya wasichana inayomilikini na taasisi ya dini ya Kiislama , mbele nguo za madeni hao walizozifua na kuanika kwenye kamba



 

  •  MAJANGA.

  •  
  • Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
  •  
  • MOTO Mkubwa  umeuteketeza Msikiti wa shule ya Sekondani ya wasichana ya AT=TAAUN ISLAMIC iliyopo maeneo ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.
  •  
  • Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2 usiku kwenye Msikiti huo ambao uko jirani kabisa na mabweni ya madent wa shule hiyo.
  •  
  • Mwandishi wa Mtandao huu anayeishi jirani na eneo la tukio alikuwa wa kwanza kufika eneo hili hata kabla ya Maafande wa kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kutinga eneo hilo.
  •  
  • Mwandishi huyo alipofika alishuhudia madeni walioko juu ya ghorofa wakipiga kelele za kuomba msaada waliposhuhudia Moto Mkubwa ukiuteketeza Msikiti wao uliopo mita kama tatu kutoka kwenye Mabweni yao.
  •  
  • Mungu ni Mwema katika tukio hilo hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa ikanga Vifaa vilivyokuwemo ndani na Msikiti huo ikiwemo Vitabu vya dini vyote viliteketea kwa moto.
  •  
  • Wakizungumza na Shekidele blog Mashuhuda wa tukio hilo Mohamed Bafadhiri ambaye ni Mtoto wa aliyekuwa sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Hayati Bafadhiri na Aziz Kapilima Agent wa Mabasi ya BM walisema
  •  
  • “Shekidele kama unavyojua sisi tunaishi jirani kabisa na shule hii ya mida ya saa 2 tuliona Moshi mkubwa ukitokea eneo hili na ghafla umeme ulizima Mtaa mzima, tumefika eneo la tukio na kushuhudia Msikiti ukiteketea kwa Moto” 
  •  
  • Jeshi la Zima Moto na Uokoaji lilifanikiwa kuzima Moto huo ingawa msikiti yote uliteketea kwa Moto. 
  •  
  • Wakati Moto ukiendelea kuuteketea Msikiti huo sheikh katinga eneo la tukio na kufanya jambo la hekima jambo gani hilo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
  •  
  • Clip Video za tukio hili zitaruka hewani hivi punde Shekidele onelive Tv

No comments:

Post a Comment

JUMBE WA LEO.

          “Ukichoka kutembea na Dunia. Dunia haitasimama kukusubiri.”   Pichani   Dunstan Shekidele akitembe na Dunia Wilaya   mbali...