Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, July 16, 2021

BAADHI YA WABONGO HATUJUI KUTUNZA VITI VYETU VIZURI, TAA ZA BARABARANI ZAENDELEA KUPUKUTIKA MORO.

Taa hii iko Mtaa wa Area 5 juu la kushoto mwa barabra juu la Mlima lakini cha ajabu imegongwa na gari licha ya uwepo wa Mlima huo na togari za zege kali

           Taa hii iko Kichani jirani na shule ya Msingi Mkwajuni

 


                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

NCHI za wenzetu huko mbele Ulaya na Marekani au baadhi ya mikoa hapa nchini, kama Vile lringa na Kilimanjaro wanaustaarabu wa kuweka Mji yao safi Sambamba na kutunza miondombinu ya barabara zao.

 

Kwa mkoa wetu wa Morogoro hali hiyo ni tofauti hatuna utamaduni huo wa kuweka mji wetu safi kubwa zaidi baadhi ya watu wanahujumu Miondombinu hiyo kwa kuiba baa, alama za barabara wakienda kuuza vyuma chakavu na wengine kuzigonga na magari au boda boda.

 

Hii inadhibitisha Mwaka jana mara baada ya barabara mpya kujenga mkoani Morogoro ile ya Kichangani, Pepsi,Oldvai na ile ya Makaburi ya Kolla mara baada ya kufungwa taa za sola Vibaka waliziba taa hizo nyakati za usiku.

 

Tunashukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro lilifanikiwa kudhibiti hali hilo kwa kuweka mitengo na kufanikiwa kuwanasa vibaka hao ambao walipewa kesi ya uhujumu uchumi wao na wateja wao. 

 

Kwa sasa hali ni tofauti  leo Mwandishi wa Mtandao huu alishuhudia taa 3 zilizogongwa na magari ili hali pembezoni mwa taa hizo kuna vizuizi vya tofari za zege kali.

 

 Taa ya kwanza iliyogongwa na gari iko eneo la Msamvu jirani kabisa  na kituo cha Mafuta’Sheli ya Abood’ barabara kuu ya Moro-Dar jirani kabisa na ilipotokea mripuko wa Lori la Mafuta  Agost 10 mwaka 2019.

 

Taa ya pili  iko Kichangani jirani kabisa na shule ya Msingi Mkwajuni na taa ya tatu iko barabara hiyo hiyo ya Kichangani  Mtaa wa Area Five.

 

 Chaajabu taa hiyo iko mlimani upande wa kushoto mwa barabara ukitokea Mjini kuelekea Nane nane lakini imegongwa na gari kama inavyonekana Pichani jirani na Pikipiki ya Mwandishi wa Mtandao huu.

 

Uwepo wa taa hizo umepunguza kama sio kuondosha kabisa vibaka kwenye mitaa hiyo hasa eneo la Pepsi awari saa 1 usiku ukipita eneo hilo umekabwa kwa sasa uwepo wa taa hizo watu  wanapita eneo hilo hata saa 4 usiku salama salmin. Faida ya Pili kufuatia mwanga wa taa hizo Wamachinga wakiwemo mama zetu na dada zetu wanafanya biashara zao hata za kuuza vigondi vya kuku kando kando mwa barabara hizo mpaka saa 5 usiku bila hofu yoyote.

 

Wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Martine Shigela alimueleza Rais Samia Suluhru kwamba Uongozi wa Mkoa uko kwenye mikakati kabamba ya kufanikisha mkoa huo kuwa jiji

No comments:

Post a Comment

HABARI KALI YA KITAA. NYAYA ZA UMEME ZAZUA TAHARUKI MTAA WA MAKABURI ‘A

 ’                               Na Dustan Shekidele,Morogoro. KAMA kawaida Leo Jumanne Mtandao Pendwa wa Shekidele unaendelea na kipengele ...