Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, July 8, 2021

MAKALLA. BAADA YA KUMSHUHUDIA MCHUNGAJI HARUSINI NAWIWA KUANDIKA MAKALA HII SEHEMU YA PILI.




Nikiwa kwenye harusi na gari hilo Picha


 
Nikiingia ndani ya Uwanja wa Jamhuri kwenye maandamano ya siku ya Wafanyakazi duniani  nikinyoosha Mkono kuonyesha moja ya Magazati ya Global Publishers.
 
 Na Mwandishi Wetu Morogoro.
 KAMA ambavyo nilitangulia kuripoti kwenye Makalla hii sehemu ya 1 kwamba baada ya kumshuhudia,Mchungaji Kachua Heliamini harusini ambaye baada ya kuniuzia gari mwaka 2007 sijaonana naye mpaka tulipokutana juzi ukumbi wa Mango Garden uliopo pande za Nunge Manispaa ya Morogoro. 
 
Baada ya utambulisho huo wa Makalla ya Kwanza sasa tuendelee sehemu ya Pili,Katika familia ya Hayati Mzee Peter Shekidele tumezaliwa watoto 7 wote ni wa baba moja na Mama Mmoja.
Kati yetu mmoja wetu wa 4 kuzaliwa aliyeniachia ziwa’Jina lihifadhi’ alikuja duniani akiwa na Ulemavu wa Miguu yote 2, alipohitimu elimu ya sekondari alijiunga na chuo cha Uguzi na baadae alifanikiwa kupata ajira hospital ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro anapohudumu mpaka sasa. 
 
Kila siku alitoka nyumbani Mji Mpya na usafiri wake wa baiskeli ya mataili 3 ambapo njiani alikumbana na changamoto nyingi hasa wakati wa Masika ambapo Mara kadhaa alikumbana na Mvua njiani. 
 
Changamoto hizo ziliniumiza ambapo niliamua kusimamisha Ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi, hukunikimuomba Mungu anipe uwezo wa kununua gari ili liweze kumpeleka ndugu yangu kazini.
 
Mungu wetu ambaye ni Msikivu alisikia Maombi yangu na Mwaka 2007 nilipata Pesa kiasi cha milioni 2 kwa njia ambazo Mungu Mwenyewe anajua nilikuwa na hakiba ya milioni 2 za kupau nyumba na ishu hiyo ya ujezi niliipiga chini na pesa hizo zikaamua kuziunganisha zikafika Million 4 nikatafuta gari kwa watu kwani pesa hizo haikuwa na uwezo wa kuingia dukani kununua gari Mpya. 
 
Chaajabu kwa njia ambazo Mungu anazijua aliniunganisha na Mchungaji Heliamini ambaye aliniambia kwamba Mwanaye aliyekuwa nje ya nchini alimtumia gari Jipya la kisasa aina ya Baloon Pichani, 
 
Alisema hakulipenda gari hilo hivyo aliamua kuliuza million 7 ili anunue gari ambalo analipenda. 
 
Mfukoni nilikuwa na Milion 4, nikaamua kufunguka nikitoa matatizo ya ndugu yangu huku nikimuonyesha ushahidi wa Picha za huyu ndugu yangu anavyopitia changamoto za barabarani na baiskeli yake. 
 
Ghafla nikamuona Mtumishi huyo wa Mungu akibadilika ambapo usowake ulisomeka kuwa na huzuni kubwa ambapo nilipoweka nukta ya maongezi yangu alisema.
 
” Nimeguswa sana hivyo nitakuzia hili gari kwa million 6 badala ya million 7 kwa vile unamilion 4 unitakukabidhi gari na kila mwezi utanilipa laki 5 ukimaliza deni nitakukabidhi Document Original za gari hii”alisema Mchungaji Heliamini anayechunga kanisa la Sabato lililolopo Misufini Manispaa ya Morogoro.
 
KUJISIFU SIO DHAMBI ZAMBI NI KUZIENDEKEZA HIZO SIFA
.
Baada ya kununua gari hilo nilimtafuta dereva ambaye sharti kuu ni kila siku asubuhi amfuate ndugu yangu nyumbani na kumpeleka kazini then anaelekea stend kufanya kazi ya Taksi mchana anamfuta kazini anamrejesha nyumbani na kuendelea na kazi yake ya Taksi.
 
Lfahamike Mwaka 2007 Baloon ndio gari la kifahari ambalo matajiri wengi walilitumia kwenye mitoko yao, wahindi walilitumia vyakati za jioni wakielekea Jamatini na Waarabu walilitumia wakitafuta Mishikaki yenye piliiki nyingi na familia zao Mida hiyo ya jioni baada ya kumaliza kazi zao. 
 
Baadhi ya matajiri hao wa Manispaa ya Morogoro walinishangaa kununua gari hilo la ‘kibosile’ na kuligeuza kuwa Taksi ili hali wao wanalitumia kama gari la matanuzi.
 
Wakati huo dereva wangu Yahaya Makweta aliegesha Stend ya Mabasi ya Msamvu kutokna na kali wa gari hilo aligonga show kiuraini hali iliyopelekea kulipa deni hilo la gari kwa wakati.
Kufuatia ufahari wa gari hilo kila Jumamosi lilikodishwa kubeba maharusi na kazi hiyo ya kubeba Maharusi niliendesha gari Mimi Mwenyewe kama inavyoonekana Pichani nikiwa na maharusi kanisa kuu la Mt Patrick Morogoro. 
 
Baada ya miaka 4 mbele gari hilo lilikamatwa na Polisi na kukaa kituoni zaidi ya wiki Moja huku ndugu yangu akikwama kwenda kazini kwa nini lilikamatwa sehemu ya tatu na ya mwisho ya Makalla hii itadadavua kila kitu hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote. 
 
 

 

No comments:

Post a Comment

JUMBE WA LEO.

          “Ukichoka kutembea na Dunia. Dunia haitasimama kukusubiri.”   Pichani   Dunstan Shekidele akitembe na Dunia Wilaya   mbali...