MAKALLA.
Picha no 2 nikiwa na Bos Shigongo kwenye moja ya Vikao vya kikazi.
Na Mwandishi Wetu Morogoro.
KAMA ambavyo nilitangulia kusema kwenye Makalla hii sehemu ya 1 kwamba baada ya kumshuhudia baada mchungaji Kachua Heliamini harusini ambaye baada ya kuniuzia gari mwaka 2007 sijaonana naye mpaka tulipokutana juzi kwenye harusi ukumbi wa Mango Garden uliopo Pande za Nunge Manispaa ya Morogoro.
Baada ya utamburisho huo wa Makalla ya Kwanza sasa tuendelee sehemu ya tatu na ya Mwisho.
Takribani miaka 4 mbele mke wa Kigogo mmoja wa Polisi Mkoa wa Morogoro alinipa, habari akimlalamikia Mumewe kutelekeza familia na kuhamia kwa kimada.
Baada ya kumhoji sambamba na kukusanya ushahidi wote ikiwemo Picha na kurekodi mahojiano hayo niligeukia upande wa pili kwa lengo la kusikia kauli ya Kigogo juu ya tuhuma hizo dhidi yake.
Kigogo huyo ambaye jina lake na cheo chake vinahifadhi ila ifahamike kwamba kati ya Vigogo 3 wa Jeshi la Polisi Mkoa yeye ni mmoja wapo.
Nilitinga kituo Kikuu cha Polisi nakuelezwa kwamba kigogo huyo amepata msiba yuko nje ya Mkoa wa Morogoro.
Nilimvutia waya ‘simu’ na kumsomea tuhuma zake ambapo alijibu kwa mkato.
”Du huyu Mwanamke mambo haya ya familia kayapeleka kwa Waandishi ok Shekidele siwezi kuzungumzia swala hilo kwani ni lakifamilia ila naomba kama unaweza kunisaidi achana nalo”alisema Kigogo huyo.
Nilimkubalia kwa masharti kwamba kama anataka nisirushe habari hiyo gazetini basi arejee kwa familia yake. Alijibu
“Kwa sasa niwezi kurejea kwani swala hilo liko kwenye vikao vya familia na wakati wowote litafika Mahakamani hivyo naendelea kukusihi kama huto jali achana na habari hiyo”.
Mwandishi wa habari hizi alimjibu kwamba kwa vile anatenda haki kwa watu wote bila kujali cheo cha mtu, utaji wa mtu au umasikini wa mtu na kamwe hata andika habari kwa uonezi au kwa shinikizo la kitu cha aina yoyote ‘So’ habari hiyo itaruka hewani.
“Kamanda habari hii itaruka hewani ila kwa kukusaidi nitaipunguza Makali sitaweka Picha zenu wala sitataja jina lako na cheo chako na hii ni kwa sababu bado naendelea na uchunguzi wa habari hii.”
Siku tatu mbele habari hii ilitoka ukurasa wa mbele gazeti la ljumaawikienda ikiwa na kichwa cha habari
”KIGOGO WA POLISI MORO ADAIWA KUTELEKEZA FAMILIA AHAMIA KWA KWA KIMADA’
Gazeti hilo liliuzika sana Mkoani Morogoro ilipofika saa 7 mchana copy zote zilikata mtaani, mara baada ya habari hiyo kutoka Bosi Shigongo alinipigia simu awari alinipongeza kwa kazi hiyo ngumu lakini pia alinitia moyo akisema nimeandika habari nzito ya kigogo wa Polisi hivyo lolote litakalotokea nimjulishe haraka.
Baada ya wiki mbili Shigongo kaniulizia tena nikamwambia niko salama hakuna tatizo lolote.
Chaajabu wiki ya tatu Majanga ya kaanza Mke wa dereva wangu wa taksi amenipigia simu akidai amemewe amekamatwa na Polisi.
“Shemeaji Makwete kanitumia sms muda huu kasema amekamatwa yuko kituo kikuu cha Polisi mimi naelekea huko Muda huu’alisema
Fasta nilitinga Polisi nikamkuta Makweta yuko chini ya ulinzi akitoa maelezo, nilipomuliza kosa kasema
”Nilikuwa na abiria mtaani nikapigiwa simu na madereva wenzangu pale Msamvu wakidai kwamba kuna wadada 2 wametoka Dar naulizia gari yangu Baloon ya Bluu iliyoandikwa ‘Ez Come Ez Go’ wakidai kwamba wameelekezwa kwamba mimi ndio najua sehemu ya kuwapeleka”alisema Makweta na kuendelea kufunguka.
“Nikawaambia wanisubiri nilipoachana na yule abiria nikawafuata nilipofika sikuwafahamu ila wamepiga simu kwa wenyeji wao nikaongea nao huyo Mwanaume kaniambia niwapeleka hao wadada Baa ya King Tom nilipofika wale wanaume wakanilipe.
Kisha wakachukua namba zangu za simu wakasema kesho saa moja asubuhi wataniita niwachukua hao wa dada niwapeleke Msamvu warejee Dar.
Saa moja wakanipigia wakiniambia niwafuta gest ya Sanivina Kichangani nilipofika wakaniambia tupitia kituo kikuu cha Polisi wakaagane na hao jamaa zao chaajabu tulipofika hapa kituoni hawa dada wakaanza kulia wakidai nimewapa madaya ya kulevya kisha nimewaibia mabegi, Pesa na pete zao za dhahabu jambo ambalo si kweli”alisema Makweta kwa uchungu.
Nilichofanya nikampigia huyo kigogo wa Polisi niliyeandika habari yake na kumueleza jambo hilo ambapo alionekana kusigitika kisha akaniambia yuko mbali kidogo hivyo baadae akifika kituoni alilishughulikia jambo hilo.
Nilipoona mpaka saa 12 hakunipigia nikaamua kumpigia akaniambia yuko Kituoni ila dereva wangu hawezi kutoka kwani bendera imeshashushwa hivyo mtuhumiwa hataweka kutoka Mpaka kesho.
Asubuhi nilipofika kituo nikaelezwa kwamba tayari dereva wangu ameshapelekwa Mahakamani hivyo mambo yote ya dhamana yako huko, nilifika mahakama ya Mkoa wa Morogoro nikiwa na mke wa dereva huyo pamoja na Mke wa kigogo huyo ambaye kwa uchungu alisema’ Kijana wawatu anateseka bila kosa wakati habari nilitoa mimi kama kukamatwa angenikamata mimi’alisema mke huyo wa kigogo ambaye pia ni Afande.
Dereva wangu kasomewa mashitaka 3 ambayo alikana na kuludishwa Mahabusu mpaka tarehe nyingine.
Baada ya kutoka mahakama hapo mida ya saa 9 Alasili nilimpigia bosi Shigongo nikamueleza kila kitu akaniambia jioni hiyo hiyo nipande basi niendele Dar, nilitoka Msamvu saa 10 jioni nikafika dar saa 2 usiku nikaenda kulala nyumbani Kigamboni kwa vile muda huo ofisi ilishafungwa.
Asubuhi nikaamukia Ofisi za Global Publishers wakati huo zilikuwa Mtaa wa Msimbazi Kariakoo nilikuta chumba cha habari Upo Uongozi Mzima wa Global, Wahariri wakiongozwa na Mhariri wa gazeti la Uwazi Mzee Stambuli na Wanasheria wa Kampuni, Moja kwa Moja nikatoa maelezo yangu kwenye kikao hicho.
Baada ya maelezo hayo Moja wa wahariri akasema kama yeye ametumia Upolisi wake na sisi tutumie Uandishi wetu na gazeti la kesho tuandike hivi
‘Licha ya kazi nzuri inayofanywa na jeshi la Polisi chini ya IGP Omar Mahita na Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete bado kuna baadhi ya Polisi wanalichafua Jeshi hilo la kuwabambikizia kesi wananchi’hii ilikuwa ni ‘lntro’ ya Stori hiyo.
Kutokana na ukali wa stori hii kuna Mwanasheria mmoja anafahamiana na Kigogo huyo akaomba azungumze naye kwanza kabla ya habari hiyo kwenda hewani akatoka kwenye kikao akampigia simu kisha akarejea na kusema.
”Nimezungumza naye kasema sio yeye aliyefanya hivyo ila atalishughulikia swala hilo gari la Shekidele litatoka Kituoni na kesi itafutwa kwa vile haikuwa na ushahidi”alisema.
Nikatoka ofisini nikaelekea Ubungo nikapanda basi nikiwa njiani Kigogo huyo alinipigia akinieleza kwamba nikifika Moro moja kwa moja nifike kituoni nichukue gari langu.
Na kesi ilifutwa baada ya walalamikaji wadada hao kutoonekana mahakamani
NDUGU YANGU MLEMAVU SASA.
Gari hilo ambalo kimsingi lilikuwa miguu ya kumpeleka ndugu yangu Mlemavu kazi likiwa kituoni zaidi ya wiki, ndugu yangu aliamua kutoa sehemu ya mshahara wake kukodi Taksi kumpeleka kazi na kumludia.
Mungu Mkubwa kuna siku ndugu yangu wakati nafika hospital hapo akihangaika kufungua Pochi amlipe dereva wa Taksi katokea Katibu Mkuu wa Hospital ninayemkumbuka kwa jina Moja la Beda akashuhudia tukio hilo.
”My God yani kila siku unakuja kazi na taksi mshahara wako si unaishi kwenye taksi wakati hospital inamagari mengi nimeumia sana sisi wazima tunatumia magari ya serikali kuja kazi wewe mlemavu unakodi taksi.
Sasa kuanzia leo nakuamulu dereva wangu kila siku badala ya kunifuta mimi utamfuta Shekidele mimi nitatumia gari langu binafsi ”alisema Katibu Mkuu huyo.
Baada ya katibu mkuu huyo kunipokea Kazi hiyo niliamua kuliuza gari langu ili sasa niweze kununua mabati ya kuezeka nyumbani yangu niliyoitelekeza kwa zaidi ya miaka 5 kufutia hakiba ya kununua mabati kuongeze kwenye ununuzi wa gari hilo.
Nilifanikiwa kuliuza gari hilo kwa Mtanzania mwenye asili ya Asia’Singa Singa’
Mtihani Mpya Miezi 4 mbele Katibu Mkuu huyo wa hospital alipata uhamisho kuelekea hospital ya Wilaya ya Kilosa lakini Mungu ni Mwema licha ya Kiongozi huyo Mwenye Moyo wa kipekee kuhamishwa alitengeneza mazingira ya ndugu yangu kuendelea kutumia usafiri wa hospital.
Niliapa kwamba siku nikibahatika kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiniambia nimueleze shida yangu japo ninashida nyingi lakini ningemueleza kwamba naomba ampandishe cheo Katibu huyo Beda.
Na hapa ndio tamati ya Makalla hii ambayo matukio yake yametokea zaidi ya Miaka 10 iliyopita na sijawahi kuripoti Popote lakini kwa mshangao mara baada ya juzikati kuonana na Mchungaji aliyeniuzia gari roho Mtakatifu alinisukuma kuandika Makalla hiyo lengo kuu ni Kumshukuru Mungu kwa miujiza aliyonifanyika kwenye mchato mzima wa kumsaidia ndugu yangu pia kumshukuru Katibu Mkuu Beda kwa Moyo wake wa huruma.
No comments:
Post a Comment