Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 12, 2021

AJARI YA MOTO SHULE YA WASICHANA,MLINZI APAMBANA KIJESHI NA KUNDI LA VIJANA WALIOMVAMIA.


           Afande Simon Elias akihojiwa na Mtandao huu jana jioni


                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MLINZI wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya AT-Tauun iliyopo Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, Simon Elias amefanikiwa kudhibiti kundi la Vijana waliotaka kuingia kinguvu kwenye shule hiyo wakati Moto ikiteketeza  bweni na Msikiti wa shule hiyo inayomilikiwa na Taasisi ya dini ya Kiislamu.

 

Tukio hilo lilitokea Juzi muda mfupi baada ya Moto huo kuanza Majira ya saa 3 usiku, na kwamba Vijana hao  licha ya kuzuiwa na Afande huyo  walitumia nguvu wakitaka kuingia ndani kinguvu.

 

Awari Mlinzi huyo aliwaeleza kistaarabu kwamba wasubiiri Polisi na Zima Moto wakifika atawafungulia geti vijana hao walipinga vikali.

Wakidai wanataka kuingia ndani kuzima Moto huo, Zima Moto na Polisi watakapofika watawakuta wanaendelea kuuzima Moto  huo.

 

“Msikiti wetu Unaungua na Bweni linaungua tunataka tukadhibiti Moto huo usiendelee kushika kasi Faya wakija watakuta tunaendelea kuzima  we Mgambo unatuzuia”walisema Masela hao huku wakimsukuba Mlinzi huyo wakishinikiza awafungulie geti.

 

Wakati hayo yakiendelea Wanafunzi wa kike wengi wao wakiwana nguo za kulalia walikurupuka kwenye Mabweni yao na kukimbilia geti wakitaka kutoka nje kunusufu maisha yao  huku giza nene likiwa limetanda shuleni hapo kufuatia Tanesco kuzima Umeme Mtaa huo wa Ngoma A kwa lengo la kuuthibiti Moto  usiendelee kuathiri majengo mengine yenye Umeme.

 

Mwandishi wa Mtandao huu aliyewahi  eneo la tukio muda mfupi baada ya moto huo kuanza,alipoona kamanda huyo amezingirwa na kundi hilo Vijana wengi wao wakiwa na Viduku kichwani kama ndege Swolwe alimfuata na kumnong’oneza kwamba asipoteze muda wa kuzungumza nao  pia asiwaruhusu wanafunzi hao kutoma nje ya geti na badala yake afunge geti hilo mpaka Polisi na Zima Moto watakapofika.

 

Mlinzi huyo wa kampuni ya Ulinzi ya DD Security alikubari ushauri huo akafunga geti hilo na muda mfupi baadae Polisi na Zima Moto waliwasili eneo la tukio na kutimiza majukumu yao ya kuzima Moto na kulinda usalama eneo hilo. 

 

Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Mohamed Bafadhiri alisema.

 

 “Tunampongeza sana huyu Mlinzi na wewe Shekidele kwa kukabiriana na tukio hilo, kundi hili la Vijana wanaoradhimisha kuingia ndani huenda walikuwa na nia hofu ya kutaka kuwaibia wanafunzi mabegi yao au kuwabaka kama unavyojua shule hii ni ya wasichana na umeme umekatwa ndani giza nene” alisema Mohamed ambaye hayati baba yake Mzee Bafadhiri hadi umauti unamkuta alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

 

Mara baada ya vurugu hizo kutokea   kwenye geti la shule hiyo iliyozungushiwa ukuta, jana habari zilizagaa mtaani wananchi wakimpongeza Mlinzi huyo huku wengine wakidai kwamba alipokea kichapo kutoka kwa vijana hao aliowazuia kuingia ndani.

 

Baada ya kupokea taarifa hiyo ya Chini ya kapeti ambayo huwezi kuipata popote, jana Mtandao huu ulitinga shule hapo kwa lengo la kuzungumza na Mlinzi huyo kuhusiana na madai hayo ya kupigwa na Kundi hilo la Masela.

 

” Hawakunipiga ingawa walinisukuma sukuma na mimi nilikuwa makini na kazi yangu”alisema Afande Elias.

 

 Clip Video ya Mahojiano hayo imeruka Yotub ya shekidele online tv. Zama huko ushuhudie tukio hilo

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...