YEREMIA 33-3
“Niite nami nitakuitika nami nitakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua”hilo ndilo neon letu la leo Jumapili ya Julay 18.
Pichani nilimuita Mungu naye akaniitikia akafanya mambo makubwa yaliyonishangaza.
Mambo hayo ni kuweka kanisa kwenye nyumba yangu toka naanza kujenga waumini wa kanisani hilo la T.A.G walikuwa wakiabudu ndani ya boma.
Baada ya waumini kuongezeka wamejenga kanisa nje ya eneo la nyumba hiyo ambapo leo jumapili asubuhi hii ninapoandika habari hii nikiwa chumbani nasikia lbada kabambe inaendelea kwenye kanisa hilo.
MAMBO MAGUMU.
Wakati huduma ikiendelea kwenye kanisa hilo na kwa vile eneo ni kumbwa zaidi ya heka moja,Siku moja Mchungaji kiongozi alinipigia simu akiomba kufanya Mkutano mkubwa nje ya kanisa hilo.
Nilimkubalia na siku za kuanza kwa mkutano huo zilivyokaribia Mchungaji huyo alijiongeza kwa kusomba kuni kutoka Mkundi kuja kanisani hapo kwa lengo la mabishi kwa wageni watakaoshiriki kwenye Mkutano huo. Wakati akisomba kuni hilo kwa usafiri wake wa Pikipiki alipofika Oil Com Nane nane barabara kuu ya Moro-Dar ndani ya daraja la Mzambarauni basi la Upendo lililotokkes nyuma yake liligusa mzigo huo wa kuni Mchunagji akayumba na kuanguka upande wa barabara.
Tairi za nyuma za basi hilo lilimkanyaga Kichwani mtumishi huyo wa Mungu na kupoteza maisha hapo hapo akiwa na mzigo wake wa kuni.
Tukio hilo lilikuwa gumu sana kwangu, nikawa kama siku nikibahatika kuingia peponi nisipomuona Mtumishi huyo wa Mungu eneo hilo naweza kumhoji Mungu kwa nini mchungaji huyo hayupo eneo hilo pa Uzima wa Milele.
Nilishiriki lbada ya mazishi ya mchungaji huyo iliyofanyika nyumbani kwake kabla ya kwenda kuzikwa nyumbani kwao Makete Mkoani Njombe.
Katika lbada hiyo ya mazishi iliyohudhuriwa na zaidi ya wachungaji 50 waliongozwa na Mke wa Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assembles Of God’T.A.G Barnabas Mtokambali na Askofu Mkuu wa Jimbo la Morogoro.
Mara baada ya lbada hiyo kukamilika Askofu wa Jimbo la Morogoro alinieleza kwamba huduma zitaendelea kama kawaida kanisani hapo na kwamba ametamteua mchungaji Mwingine kuja kuendeleza huduma kanisania hapo.
No comments:
Post a Comment