Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 31, 2021

MCHANGO WA KUMSAIDI GERALD MATHIAS MDAMU, MASTAA WA YANGA SIMBA KUKIPIGA MUDA HUU UWANJA WA SABA SABA.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa na Picha ya Mchezaji huyo, baada ya kuisafisha


                           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

lle gemu ya Mastaa wa Ligi kuu na Mastaa wa ligi daraja la kwanza inapigwa muda huu kwenye uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

 

Lengo la gemu hiyo ni kuchangia Matibabu ya Mchezaji wa timu ya Polisi Tanzania Gerald Mathias Mdamu ambaye ni Mkazi wa Mkoani Morogoro kama ilivyo wachezaji hao wanaocheza gemu hiyo ya leo.

 

Pesa ya Kiingilio itakayopatikana kwenye mchezo huo yote atakabidhi Mdamu nikiwa ni mchango kutoka kwa wachezaji wenzie wana Morogoro na wadau wa Soka wa Mkoa wa Morogoro.

Mechi hiyo imeratibiwa na wadau wa Soka Mkoa wa Morogoro wakiwemo Waandishi wa habari Wachezaji wa Simba na Yanga na Viongozi wa chama Cha Soka Mkoa na Wilaya ya Morogoro.

 

Katika Kamati hiyo Mwandishi wa Mtandao huu alipewa jukumu la Kutafuta na kusafisha Picha kubwa ya Mdamu ambayo ituzungumshwa uwanjani hapo kabala ya gemu hiyo kwa lengo la kutoa fursa kwa watu wasiomfahamu mchezji huyo.

 

 Picha Mwandishi wa Mtandao huu ameshakamiliza kazi hiyo muda huu anaweka kwenye frem Picha hiyo na kuelekea Uwanja wa Saba saba. Hivyo natumia fursa hii kuwaalika wananachi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kushuhudia mtanange huo kufika kwako uwanjani na kulipa kingilio cha shilingi elfu 2.

 

Kwa kufanya hivyo Moja kwa Moja utakuwa umeshiriki kikamilifu kwenye mchango wa Mwanasoka huyo Mkazi wa Mkoani Morogoro.

 

Baadhi ya wachezaji wanatarajiwa kuwepo kwenye mchezo huo ni Pamoja na Shiza Kichuya, Salumu Kihimbwa, Jafar Kibaya, Shomari Kapombe, Shomari Kibwana, Dikson Job, Zawadi Mauya. Mzamiru Yassin. Zubar Daby, Abdallah Waziri Hassan Kessy na Aishi Manura.


 

THE GUNNERS NDONDO CUP, REFA ASUSA DAKIKA 45 ZA AWARI, AINGIA REFA MWINGINE KUMALIZIA DAKIKA 45 ZA PILI

Refa Kassim Saleh Boko akipiga kura na Manahoda wa Salange Fc na Chadongo
.....Waamuzi na Manahodha wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu jana jionim kabla ya refa kasi kususa kuendelea na mchezo huo baada ya kuvamiwa na Mashabiki wa Salange

Baada ya refa Kassimu Kususa dakika 45 za pili aliingia refa Mwingine Simba Juma Pichani
...Kipa wa Chadongo Huseein Dio akilalamika Maumivu, huku Winga wa Salange Gambo lld akidai kwamba kiba huyo anapoteza Muda, beki wa Chadongo Nasry Scobber akimtania Gambo kwamba acha kipa apunzishe timu
...Refa Simba Juma'Difu' akimuhesabia dakika Kipa huyo wa Simba B
Kipa wa Chadongo Hussein Dio ambaye ni Kipa namba moja wa timu ya Simba B akiruka hewani kufuta bao la wazi mshuti huo ulipigwa na winga wa Salange Shiza Kichuya. lkumbukwe kwenye hatua ya robo fainal ya Michuano hiyo Kipa huyo aliidakia timu ya Black People taifa la watu weusi kutoka Mji Mpya

...Vituko vya ndondo Cup Shabiki huyu wa Salange alitinga uwanjani akiwa na silaha, Manati kubwa hata hivyo manati hiyo aliingia nayo uwanjani hapo kama show
Winga wa Chadongo Hassan Mkota 'Messi wa Chamwino akipiga Kic Taka huku akichungwa na beki wa Salange, Messi  ni mchezaji wa zamani wa Geita Gold na Mawenzi Market
Kipa wa Chadongo ambaye pia ni Kipa namba Moja wa Moro Kids ambaye hatua ya robo fainal ya Michuano hiyo aliidakia timu yake ya Moro Kids. lfahamike kanuni za Michuano hii ya Ndondo timu yako ikitolea kwenye Michuano mchezaji ana uhuru wa kuchezea timu nyingingi iliyovuka hatua iliyofuata. Katika robo fainal Moro Kid alifunga bao 3-2 na Salange Fc

                                Kikosi cha Chadongo Fc
Mastaa wa ligi kuu wanaokipiga Salange Fc Shiza Kichuya Kulia anayekipiga Namungo na Salum Kihimbwa Chuji anayekipiga Mtibwa Sugar
...Winga hatari wa Salange Fc ambaye anakipiga Mtibwa Sugar Jafar Salum Kibaya
Winga wa Salange Fc Salum Kihimbwa kulia akigombea Mpira na beki wa Chadongo


Hawa sio kwamba wanaomba Mungu la hasha wanajianda kuruka juu kugombea mpira
Winga wa  Salange Fc ambaye ni Mcheaaji wa zamani wa Mbeya City Gamba ldd ambaye kwa sasa anacheza soko la Kuliwa Uarabuni akijikunya kama kambara akijaribu kufunga bao kw akichwa bila mafanikio


Winga wa Salange Salum Kihimbwa Chuji akimshika kiuno beki wa Chadongo huku wakigombea Mpira wa juu
Winga wa Salange anayecheza soka la kulipwa uarabuni Gambo ldd Kushoto akisaka mbinu za kumtoka beki wa Chadongo
              ...Vita yawanaume mguni wa shingo kazi inaendelea
Baadhi ya Uamti wawatu uliotinga jana kwenye nusu fainali ya The Gunners ndondo cup kwa kiingilo cha buku 2

 Uhondo wa The Gunners Ndondo Cup ni kwa wote, warembo wakiingia uwanjani jana huku wakisema" Shekidele tupige Picha na sisis uturushe kwenye blog yako"

.

                                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

MWAMUZI Kassim Saleh Boko wa daraja la kwanza jana amegoma kuendelea kuchezesha nusu fainali ya Michuano Pendwa ya The Gunners Ndondo Cup’Super Sixsteen 2020-21’ kati ya timu zilizosheheni wacheza nyota wa ligi kuu Salange Fc inayomilikiwa na Matajiri wa Stend ya Mabasi Msamvu na Chadongo inayomilikiwa na Tajiri anayemiliki Maduka ya Vifaa vya Ujenzi.

 

Kwa Mshangazo wa wengi dakika 45 za awari zilipotamatika huku timu hizo zikiwa sale ya 0-0 kundi la Mashabiki wa Salange walimvaa Mwamuzi Boko Maarufu ‘Boko Haramu’wakimshutumu kwamba anawapendea Chadongo.

 

Wakati refa huyo aliyechezesha vizuri dakika hizo 45 akiwauliza amefanya kosa gani? mmoja wa mashabiki alimvamia na kumtovuga kwa kumwingiza kidole jichoni.

Kufuatia hali hiyo refa huyo Mmasai kutoka Mkoa wa Arusha kwakulinda usalama wake aliamua kusua kwa kuendelea kuchezesha mchezo huo uliofulika Umati Mkubwa Mashabiki.

 

Askari waliokuwepo uwanjani hapo walifanikiwa kumkamata shabiki huyo na kumtoa nje ya Uwanja,  licha ya kuombwa sana na Mratibu Mkuu wa Michuano hiyo Seleman Mpemba Maarufu Sele The Gunners’refa huyo alishikilia msimamo wake.

 Ili kunusuru gemu hiyo kuendelea  Sele Mpemba ambaye ni Mtoto wa Makamo wa Pili wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyestaafu hivi karibuni  Balozi Seif ldd alimteua refa Mwingine Simba Juma pia wa daraja la kwanza kumalizi dakika 45 za mwisho.

Leo Jumamosi kwenye uwanja huo wa Saba saba  kuna ile gemu kali ya kuchangia Matibabu ya Mchezaji wa Polisi Tanzania Mwana Morogoro Mathias Gerald Mdamu Kati ya wachezaji nyota wa ligi kuu wa kazi wa Mkoa wa Morogoro na wachezaji nyota wa ligi daraja la kwanza Wakazi wa Mkoa wa Morogoro.

 

Jumatatu Nusu fainali ya Pili ya The Gunners Ndondo Cup itaendelea kwa kuzikutanisha timu ngumu za Wakushi Fc Kutoka Misufiki Kata ya Mafiga na Nungutu Fc Kutoka Bong’ora Kata ya Kilakala.


Friday, July 30, 2021

Nusu Fainali ya Michuano Pendwa ya The Gunners Ndondo Cup ‘Super Sixsteen 2020-21’

Heka heka uwanjani wachezaji wa Salange na Chadongo wakiluka juu kugombea Mpira.

 Baadhi ya mashabiki wakimulika tochi za simu zao kushinikiza Mwamuzi amalize pambano baada ya giza kutanda uwaniani leo jioni.


 

                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mastaa wa ligi kuu,Kichuya, Kihimbwa na Kibaya washindwa kuipeleka Salnage Fc fainali wabanwa mbavu na Chadongo FC gemu imelala baada ya dakika 90 miamba hiyo kutoka sale ya 0-0 na kwenye Mikwaju ya Pelnaty pia

 

wametoka sale kwa kufunga pelnaty 5-5. Wameshindwa kuendelea kupiga Mikwaju hiyo ya pelnaty baada ya giza kutanda uwanja wa Saba saba hivyo gemu hiyo iliyo iliyojaa udambwi dambwi kwa muda wote wa dakika 90 lmelala na Waandaji watapanga siku nyingine timu hizo zenye uwezo kifedha kuludiana

 

kundi la Mashabiki waliofulika kwenye uwanja huo was aba saba jioni ya leo wamelidhika na hatu hiyo ya gemu hiyo kulala baada ya kushuhudia show kali kwa muda wote wa dakika 90 wakidai kwamba buku 2 yao waliolipa geni imekweda kihalali.

 

Baadhi ya Mashabiki hao walivamia gori ambalo lilitumika kupigwa Mikwaju hiyo ya Pelnaty wakawasha tochi za simu zao wakimshinikiza Mwamuzi Simba Juma kulaza gemu hiyo huku makipa wote wawili wakiwaunga Mkono Mashabiki hao.

 

Picha zaidi za gemu hizo zitaruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

              



MAUYA, JOB KAPOMBE KICHUA NA SHOMARI KIBWANA KUSHIRIKI MCHEZO WA HISANI YA KUCHANGIA MATIBABU YA MDAMU.




 Makocha walioibua Kipaji cha Mathias Gerald Mdam[Kocha Mkuu Athuman Juma 'Maarufu Ticha Micho'Kati' na Hamis Mtagwa[kulia wakiwa na Shiza Kichuja juzi kwenye Michuano ya The Gunners Super Sixsteen 2020-21. Makocha hao wakiwa na timu ya Champion Kids wamefanikiw akuibua Vipaji vingi vya wachezaji nyota nchini Kama vile Shiza Kichuya, Hassan Kessy, Mathias Gerard Mdam na Abdallah Waziri'Kuku'


                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Wadau Mkoani Morogoro wakiongozwa na Waandishi wa habari wameanda mechi kali yenye lengo la kuchangia Matibabu ya mchezaji wa Polisi Tanzania Mkazi wa Mkoa Morogoro Gerald Mathias Mdamu.

 

Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya Ushambuliaji  timu ya Polisi Tanzania  inayoshiriki ligi kuu alivunjika Miguu yote miwili kwenye ajari wakati timu hiyo ikitoka Mazoezini Mjini Moshi.

 

Awari kuliibuka taarifa kwamba huenda mchezaji huyo akakatwa Mguu ulioumia vibaya lakini baadae daktari bingwa wa hospital ya Muhimbili alipolazwa mchezaji huyo alikaririwa na chombo kimoja cha habari akikanushwa taarifa za kukatwa mguu kwa mchezaji huyo.

 

Katika kuchangia Matibabu ya Mchezaji huyo Wadau hao wa Mkoa wa Morogoro wameanda mchezo wa kirafiki utakaofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Saba saba kwa kiingilio cha elfu 2 kiasi cha pesa kitakachopatikana atabibidhiwa mchezaji huyo.

 

Gemu hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Ligi kuu wa kazi wa Mkoa wa Morogoro watakipiga na wachezaji wa ligi daraja la kwanza wanaocheza timu mbali mbali nchini ambao nao baada ya ligi hiyo kutamatika wamereja  nyumbani Morogoro.

 

Baadhi ya wachezaji nyota wa ligi kuu wakazi wa Mkoa wa Morogoro ni Pamoja na Shomari Kapombe, Mzamiru Yasin  na Aishi Manula[Simba] Kibwana Shomari Dickson Job Zawadi Mauya[Yanga] Nickson Kibabage’Taifa Stars’ Shiza Kichuya Namungo’ Zubari Daby [Ruvu Shooting] Abdallah Waziri’Kuku’ ‘JKT Tanzania’.

 

Wengine ni Hassan Kessy. lsmal Mwesa’Chomeka’  Salum Kihimbwa ‘Chuji’ Jafar Kibaya Abuutwarib Mshery [Mtibwa Sugar]

 

Kwa pamoja wachezaji hao wamekubali kushiriki kwenye mchezo huo kwa lengo la kumsaidia mchezaji mwenzao Mwana Morogoro.

 

Mdamu Mkazi wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro aliibuliwa Kipaji chake na Kocha Juma Athuman Maarufu Ticha Micho’ akiwa na timu ya Champion Kids ya Mwembesongo.

 

Baada ya Mdam kuchaguliwa timu ya Vijana ya Mkoa wa Morogoro iliyoshiriki michuano ya Copa Coca Cola Viongozi wa Mwadui ya Shinyanga walivutia na kiwango chake wakaamua kumsajiri. Ikumbukwe Mwaka Simba ilifungwa kwa Mara ya kwanza toka ligi hiyo kuanza na Mwadui na bao hilo Pekee lilifungwa na Mdamu.

 

Mwaka jana  Mdam aliihama timu hiyo ya wachimba Madini Mwadui na kujiunga na Maafande wa Polisi Tanzania timu aliyoitumikia mpaka anapata ajari mwezi uliopita. Kwa sasa Mtandao huu unajianda kutinga nyumbani kwa Wazazi wa Mchezaji huyo Maeneo ya Mwembesongo kwa lengo la kuzungumza nao  kuhusiana na ajari hiyo aliyoipata mtoto wao. Hivyo endelea kuwa jirani na Youtube ya Shekidele tv onli na blog ya Shekidele.

                       CAPTION  

Maafisa wa Jeshi la Polisi wakimjulia hali Mdau.

 Picha namba 2 basi la Polisi lililopata ajari iliyosababisha Mdam kuvunjika Miguu yote 2


MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...