Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, July 30, 2021

Nusu Fainali ya Michuano Pendwa ya The Gunners Ndondo Cup ‘Super Sixsteen 2020-21’

Heka heka uwanjani wachezaji wa Salange na Chadongo wakiluka juu kugombea Mpira.

 Baadhi ya mashabiki wakimulika tochi za simu zao kushinikiza Mwamuzi amalize pambano baada ya giza kutanda uwaniani leo jioni.


 

                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Mastaa wa ligi kuu,Kichuya, Kihimbwa na Kibaya washindwa kuipeleka Salnage Fc fainali wabanwa mbavu na Chadongo FC gemu imelala baada ya dakika 90 miamba hiyo kutoka sale ya 0-0 na kwenye Mikwaju ya Pelnaty pia

 

wametoka sale kwa kufunga pelnaty 5-5. Wameshindwa kuendelea kupiga Mikwaju hiyo ya pelnaty baada ya giza kutanda uwanja wa Saba saba hivyo gemu hiyo iliyo iliyojaa udambwi dambwi kwa muda wote wa dakika 90 lmelala na Waandaji watapanga siku nyingine timu hizo zenye uwezo kifedha kuludiana

 

kundi la Mashabiki waliofulika kwenye uwanja huo was aba saba jioni ya leo wamelidhika na hatu hiyo ya gemu hiyo kulala baada ya kushuhudia show kali kwa muda wote wa dakika 90 wakidai kwamba buku 2 yao waliolipa geni imekweda kihalali.

 

Baadhi ya Mashabiki hao walivamia gori ambalo lilitumika kupigwa Mikwaju hiyo ya Pelnaty wakawasha tochi za simu zao wakimshinikiza Mwamuzi Simba Juma kulaza gemu hiyo huku makipa wote wawili wakiwaunga Mkono Mashabiki hao.

 

Picha zaidi za gemu hizo zitaruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

              



No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...