Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 31, 2021

MCHANGO WA KUMSAIDI GERALD MATHIAS MDAMU, MASTAA WA YANGA SIMBA KUKIPIGA MUDA HUU UWANJA WA SABA SABA.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa na Picha ya Mchezaji huyo, baada ya kuisafisha


                           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

lle gemu ya Mastaa wa Ligi kuu na Mastaa wa ligi daraja la kwanza inapigwa muda huu kwenye uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

 

Lengo la gemu hiyo ni kuchangia Matibabu ya Mchezaji wa timu ya Polisi Tanzania Gerald Mathias Mdamu ambaye ni Mkazi wa Mkoani Morogoro kama ilivyo wachezaji hao wanaocheza gemu hiyo ya leo.

 

Pesa ya Kiingilio itakayopatikana kwenye mchezo huo yote atakabidhi Mdamu nikiwa ni mchango kutoka kwa wachezaji wenzie wana Morogoro na wadau wa Soka wa Mkoa wa Morogoro.

Mechi hiyo imeratibiwa na wadau wa Soka Mkoa wa Morogoro wakiwemo Waandishi wa habari Wachezaji wa Simba na Yanga na Viongozi wa chama Cha Soka Mkoa na Wilaya ya Morogoro.

 

Katika Kamati hiyo Mwandishi wa Mtandao huu alipewa jukumu la Kutafuta na kusafisha Picha kubwa ya Mdamu ambayo ituzungumshwa uwanjani hapo kabala ya gemu hiyo kwa lengo la kutoa fursa kwa watu wasiomfahamu mchezji huyo.

 

 Picha Mwandishi wa Mtandao huu ameshakamiliza kazi hiyo muda huu anaweka kwenye frem Picha hiyo na kuelekea Uwanja wa Saba saba. Hivyo natumia fursa hii kuwaalika wananachi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kushuhudia mtanange huo kufika kwako uwanjani na kulipa kingilio cha shilingi elfu 2.

 

Kwa kufanya hivyo Moja kwa Moja utakuwa umeshiriki kikamilifu kwenye mchango wa Mwanasoka huyo Mkazi wa Mkoani Morogoro.

 

Baadhi ya wachezaji wanatarajiwa kuwepo kwenye mchezo huo ni Pamoja na Shiza Kichuya, Salumu Kihimbwa, Jafar Kibaya, Shomari Kapombe, Shomari Kibwana, Dikson Job, Zawadi Mauya. Mzamiru Yassin. Zubar Daby, Abdallah Waziri Hassan Kessy na Aishi Manura.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...