Makocha walioibua Kipaji cha Mathias Gerald Mdam[Kocha Mkuu Athuman Juma 'Maarufu Ticha Micho'Kati' na Hamis Mtagwa[kulia wakiwa na Shiza Kichuja juzi kwenye Michuano ya The Gunners Super Sixsteen 2020-21. Makocha hao wakiwa na timu ya Champion Kids wamefanikiw akuibua Vipaji vingi vya wachezaji nyota nchini Kama vile Shiza Kichuya, Hassan Kessy, Mathias Gerard Mdam na Abdallah Waziri'Kuku'
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Wadau Mkoani Morogoro wakiongozwa na Waandishi wa habari wameanda mechi kali yenye lengo la kuchangia Matibabu ya mchezaji wa Polisi Tanzania Mkazi wa Mkoa Morogoro Gerald Mathias Mdamu.
Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya Ushambuliaji timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki ligi kuu alivunjika Miguu yote miwili kwenye ajari wakati timu hiyo ikitoka Mazoezini Mjini Moshi.
Awari kuliibuka taarifa kwamba huenda mchezaji huyo akakatwa Mguu ulioumia vibaya lakini baadae daktari bingwa wa hospital ya Muhimbili alipolazwa mchezaji huyo alikaririwa na chombo kimoja cha habari akikanushwa taarifa za kukatwa mguu kwa mchezaji huyo.
Katika kuchangia Matibabu ya Mchezaji huyo Wadau hao wa Mkoa wa Morogoro wameanda mchezo wa kirafiki utakaofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Saba saba kwa kiingilio cha elfu 2 kiasi cha pesa kitakachopatikana atabibidhiwa mchezaji huyo.
Gemu hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Ligi kuu wa kazi wa Mkoa wa Morogoro watakipiga na wachezaji wa ligi daraja la kwanza wanaocheza timu mbali mbali nchini ambao nao baada ya ligi hiyo kutamatika wamereja nyumbani Morogoro.
Baadhi ya wachezaji nyota wa ligi kuu wakazi wa Mkoa wa Morogoro ni Pamoja na Shomari Kapombe, Mzamiru Yasin na Aishi Manula[Simba] Kibwana Shomari Dickson Job Zawadi Mauya[Yanga] Nickson Kibabage’Taifa Stars’ Shiza Kichuya Namungo’ Zubari Daby [Ruvu Shooting] Abdallah Waziri’Kuku’ ‘JKT Tanzania’.
Wengine ni Hassan Kessy. lsmal Mwesa’Chomeka’ Salum Kihimbwa ‘Chuji’ Jafar Kibaya Abuutwarib Mshery [Mtibwa Sugar]
Kwa pamoja wachezaji hao wamekubali kushiriki kwenye mchezo huo kwa lengo la kumsaidia mchezaji mwenzao Mwana Morogoro.
Mdamu Mkazi wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro aliibuliwa Kipaji chake na Kocha Juma Athuman Maarufu Ticha Micho’ akiwa na timu ya Champion Kids ya Mwembesongo.
Baada ya Mdam kuchaguliwa timu ya Vijana ya Mkoa wa Morogoro iliyoshiriki michuano ya Copa Coca Cola Viongozi wa Mwadui ya Shinyanga walivutia na kiwango chake wakaamua kumsajiri. Ikumbukwe Mwaka Simba ilifungwa kwa Mara ya kwanza toka ligi hiyo kuanza na Mwadui na bao hilo Pekee lilifungwa na Mdamu.
Mwaka jana Mdam aliihama timu hiyo ya wachimba Madini Mwadui na kujiunga na Maafande wa Polisi Tanzania timu aliyoitumikia mpaka anapata ajari mwezi uliopita. Kwa sasa Mtandao huu unajianda kutinga nyumbani kwa Wazazi wa Mchezaji huyo Maeneo ya Mwembesongo kwa lengo la kuzungumza nao kuhusiana na ajari hiyo aliyoipata mtoto wao. Hivyo endelea kuwa jirani na Youtube ya Shekidele tv onli na blog ya Shekidele.
CAPTION
Maafisa wa Jeshi la Polisi wakimjulia hali Mdau.
Picha namba 2 basi la Polisi lililopata ajari iliyosababisha Mdam kuvunjika Miguu yote 2
No comments:
Post a Comment