Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 31, 2021

THE GUNNERS NDONDO CUP, REFA ASUSA DAKIKA 45 ZA AWARI, AINGIA REFA MWINGINE KUMALIZIA DAKIKA 45 ZA PILI

Refa Kassim Saleh Boko akipiga kura na Manahoda wa Salange Fc na Chadongo
.....Waamuzi na Manahodha wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu jana jionim kabla ya refa kasi kususa kuendelea na mchezo huo baada ya kuvamiwa na Mashabiki wa Salange

Baada ya refa Kassimu Kususa dakika 45 za pili aliingia refa Mwingine Simba Juma Pichani
...Kipa wa Chadongo Huseein Dio akilalamika Maumivu, huku Winga wa Salange Gambo lld akidai kwamba kiba huyo anapoteza Muda, beki wa Chadongo Nasry Scobber akimtania Gambo kwamba acha kipa apunzishe timu
...Refa Simba Juma'Difu' akimuhesabia dakika Kipa huyo wa Simba B
Kipa wa Chadongo Hussein Dio ambaye ni Kipa namba moja wa timu ya Simba B akiruka hewani kufuta bao la wazi mshuti huo ulipigwa na winga wa Salange Shiza Kichuya. lkumbukwe kwenye hatua ya robo fainal ya Michuano hiyo Kipa huyo aliidakia timu ya Black People taifa la watu weusi kutoka Mji Mpya

...Vituko vya ndondo Cup Shabiki huyu wa Salange alitinga uwanjani akiwa na silaha, Manati kubwa hata hivyo manati hiyo aliingia nayo uwanjani hapo kama show
Winga wa Chadongo Hassan Mkota 'Messi wa Chamwino akipiga Kic Taka huku akichungwa na beki wa Salange, Messi  ni mchezaji wa zamani wa Geita Gold na Mawenzi Market
Kipa wa Chadongo ambaye pia ni Kipa namba Moja wa Moro Kids ambaye hatua ya robo fainal ya Michuano hiyo aliidakia timu yake ya Moro Kids. lfahamike kanuni za Michuano hii ya Ndondo timu yako ikitolea kwenye Michuano mchezaji ana uhuru wa kuchezea timu nyingingi iliyovuka hatua iliyofuata. Katika robo fainal Moro Kid alifunga bao 3-2 na Salange Fc

                                Kikosi cha Chadongo Fc
Mastaa wa ligi kuu wanaokipiga Salange Fc Shiza Kichuya Kulia anayekipiga Namungo na Salum Kihimbwa Chuji anayekipiga Mtibwa Sugar
...Winga hatari wa Salange Fc ambaye anakipiga Mtibwa Sugar Jafar Salum Kibaya
Winga wa Salange Fc Salum Kihimbwa kulia akigombea Mpira na beki wa Chadongo


Hawa sio kwamba wanaomba Mungu la hasha wanajianda kuruka juu kugombea mpira
Winga wa  Salange Fc ambaye ni Mcheaaji wa zamani wa Mbeya City Gamba ldd ambaye kwa sasa anacheza soko la Kuliwa Uarabuni akijikunya kama kambara akijaribu kufunga bao kw akichwa bila mafanikio


Winga wa Salange Salum Kihimbwa Chuji akimshika kiuno beki wa Chadongo huku wakigombea Mpira wa juu
Winga wa Salange anayecheza soka la kulipwa uarabuni Gambo ldd Kushoto akisaka mbinu za kumtoka beki wa Chadongo
              ...Vita yawanaume mguni wa shingo kazi inaendelea
Baadhi ya Uamti wawatu uliotinga jana kwenye nusu fainali ya The Gunners ndondo cup kwa kiingilo cha buku 2

 Uhondo wa The Gunners Ndondo Cup ni kwa wote, warembo wakiingia uwanjani jana huku wakisema" Shekidele tupige Picha na sisis uturushe kwenye blog yako"

.

                                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

MWAMUZI Kassim Saleh Boko wa daraja la kwanza jana amegoma kuendelea kuchezesha nusu fainali ya Michuano Pendwa ya The Gunners Ndondo Cup’Super Sixsteen 2020-21’ kati ya timu zilizosheheni wacheza nyota wa ligi kuu Salange Fc inayomilikiwa na Matajiri wa Stend ya Mabasi Msamvu na Chadongo inayomilikiwa na Tajiri anayemiliki Maduka ya Vifaa vya Ujenzi.

 

Kwa Mshangazo wa wengi dakika 45 za awari zilipotamatika huku timu hizo zikiwa sale ya 0-0 kundi la Mashabiki wa Salange walimvaa Mwamuzi Boko Maarufu ‘Boko Haramu’wakimshutumu kwamba anawapendea Chadongo.

 

Wakati refa huyo aliyechezesha vizuri dakika hizo 45 akiwauliza amefanya kosa gani? mmoja wa mashabiki alimvamia na kumtovuga kwa kumwingiza kidole jichoni.

Kufuatia hali hiyo refa huyo Mmasai kutoka Mkoa wa Arusha kwakulinda usalama wake aliamua kusua kwa kuendelea kuchezesha mchezo huo uliofulika Umati Mkubwa Mashabiki.

 

Askari waliokuwepo uwanjani hapo walifanikiwa kumkamata shabiki huyo na kumtoa nje ya Uwanja,  licha ya kuombwa sana na Mratibu Mkuu wa Michuano hiyo Seleman Mpemba Maarufu Sele The Gunners’refa huyo alishikilia msimamo wake.

 Ili kunusuru gemu hiyo kuendelea  Sele Mpemba ambaye ni Mtoto wa Makamo wa Pili wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyestaafu hivi karibuni  Balozi Seif ldd alimteua refa Mwingine Simba Juma pia wa daraja la kwanza kumalizi dakika 45 za mwisho.

Leo Jumamosi kwenye uwanja huo wa Saba saba  kuna ile gemu kali ya kuchangia Matibabu ya Mchezaji wa Polisi Tanzania Mwana Morogoro Mathias Gerald Mdamu Kati ya wachezaji nyota wa ligi kuu wa kazi wa Mkoa wa Morogoro na wachezaji nyota wa ligi daraja la kwanza Wakazi wa Mkoa wa Morogoro.

 

Jumatatu Nusu fainali ya Pili ya The Gunners Ndondo Cup itaendelea kwa kuzikutanisha timu ngumu za Wakushi Fc Kutoka Misufiki Kata ya Mafiga na Nungutu Fc Kutoka Bong’ora Kata ya Kilakala.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...