Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 13, 2025

MWAKA MPYA MAMBO MAPYA MOSHI MWEUPE UNAANZA KUONEKANA UJEZI WA DARAJA LA RELWE.




 

              Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

KAMA nilivyoahidi juzi kwamba panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu jumatatu ya wiki hii ningetembelea tena kwenye ujenzi wa daraja la Relwe lililopo mto Morogoro Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa,kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ni maarufu kwa jina la daraja la Ng’ombe.

 

Mwenyezi Mungu ametii maombi yetu amempa afya njema na kibari Mwandishi wa habari hizi cha kutimiza ahadi hiyo niliyoitoa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mtandao huu pendwa wa Shekidele.

 

Mwandishi huyo alipofika ‘Site’ alishuhudia Mkandarasi huyo Mzawa anayefanya kazi hiyo kwa kasi ya ajabu ameshamwaga zege eneo la juu ya daraja.

 

Mpiga picha wa Mtandao huu alipanda juu ya daraja hilo na kushuhudia mafundi wakiwa katika hatu za mwisho za kufunga mabosi ya nguzo za pembezi tayari kwa kumwaga zege ambapo hiyo ndio hatua ya mwisho ya ujenzi wa daraja hilo.

 

Kama kawaida daraja hilo litakapo kamailika Mtandao huu utarusha hewani hivyo endelea kuwa jirani na mtandao huu muda wote

    

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...