Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 10, 2025

DARAJA LA RELWE MWENDO MDUNDO.



 


        Na Dustan Shekidele Morogoro.

 Awari ya wote natangulisha samahani kwa kutokuwa hewani takribani wiki Moja hii ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

 

Baada ya hali kuwa swali Mtandao huu umerejea hewani kuendelea kurusha habari Moto moto za chini ya kapeti, hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao pendwa wa Shekidele Muda wote ambapo kwa leo tunaanza na habari ya ujenzi wa daraja la Mji Mpya Morogoro.

 

UJENZI wa daraja la Relwe Maarufu daraja la Ng’ombe lililopo Mto Morogoro Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa  lipo hatua za mwisho  kukamilika.

 

Katikati ya wiki iliyopita Mtandao huu ulitembelea daraja hilo na kushuhudia mafundi wakiendelea kusuka Nondo ‘Silabu’ ya juu kuelekea hatua ya mwisho ya umwagaji zege eneo la juu la daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa kata za Mji Mpya, Kichangani.na Kilakala.

 

Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu kesho Mtandao huu utakatiza tena kukagua maendeleo ya daraja hilo hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...