Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 20, 2025

CRDB FEDERATION CUP, WILAYA YA MOROGORO IMEFIKA PATAMU.

                                                 Kikosi cha Chamwino Rangers
                               Kikosi cha Zuia Fc
Kocha Mkuu wa Chamwino Juma Mgonja akiwapa maelekezo vijana wake kabla ya gemu kuanza




Mshambuliaji wa Zuia akiokota mpira wavuni baada ya kufunga bao la Kwanza
..... Baada ya kufunga alikwenda kwenye Bench kushangalia na wenzake
             Mshambuliaji wa Zuia akifunga bao a kwanza


                Kipa wa Chamwino akipangua mpiia wa Kona.



 

   

            Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 MICHUANO namba mbili kwa ukubwa Tanzania,Ligi ya Shirikisho’FA’ Maarufu ‘CRDB FEDERATIN CUP’inayoanzia chini kabisa hatua ya Wilaya,imefika patamu Wilaya ya Morogoro.

Timu mbili za Fountain Gate yenye maskani yake kata ya Kihonda Maghorofani na Moro Ranger yenye Maskani yake Kata ya Kilakala, zimefanikiwa kutinga hatua ya fainaii itakayopigwa Leo Alhamisi katika uwanja wa Saba Saba Manispaa ya Morogoro.

Bigwa wa Michuano ataiwakilisha wilaya ya Morogor kwenye hatua ya Mwisho ya kucheza na mabingwa wa wilaya nyingine za kumsaka Bingwa atakayeuwakilisha Mkoa wa Morogoro kucheza hatua ya Mtoano na mabingwa wa mikoa mengine.

Mtandao huu utakuwa uwanjani hapo kukusanya matukio yote hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

Pichani ni matukio mbali mbali ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi hiyo kati ya Chamwino Ranger[Jezi nyeusi] kutoka Kata ya Chamwino dhidi ya Zuia Fc Kutoka kata ya Lukobe.

 

Katika mchezo huo Zuia alisonga mbele baada ya kuinyuka Chamwino bao 2-0.

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...