Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 24, 2025

FOUNTAIN GATE YATWAA UBINGWA WA CRDB FEDERATION CUP.

                                Papatu papatu ya fainali hiyo







wachezaji,Viongozi na mashabiki wa Fountain Gate wakiwa katikati ya uwanja wakimshukuru Mungu kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa CRDB Federatin Cup
                                     Kipa wa mabingwa hao
Mgeni rasmi wa fainali hiyo Selestini Mbilinyi akimkabidhi zawadi ya jezi Nahodha wa Fountain Gate Denis Mwantenga.

                       Na Dunstan Shekidele, Morogoro.

TIMU ya Fountain Gate wiki iliyopita imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya kombe la Shirikisho’Wilaya ya Morogoro Maarufu CRDB Federation Cup.

 

Vijana hao wa Fountain Gate kutoka kituo cha kukuza na kurea Vipaji chenye maskani yake Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro kinachomilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu nchini Japhat Makao mwenyeji wa Morogoro mwenye maskani yake Jijini Dodoma,imenyakua ubingwa huo baada ya kuinyuka Moro Rangers kutoka Kilakala kwa pelnati 5-4 miamba hiyo imefikia hatua hiyo ya pelnati baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo huo wa fainali uliopigwa uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro Alhamisi iliyopita.

 

Baada ya kunyakua ubingwa huo na kukabidhiwa zawadi ya jezi na mwenyekiti wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro Selestin Mbilinyi, Vijana hao wa Fountain Gate wamesafiri kuelekea Wilaya ya Mvomero ambapo Leo Jioni watacheza mchezo wa fainali na Volucano Fc ambao ni mabingwa wa kombe hilo Wilaya ya Mvomero.

 

Mshindi wa mchezo huo atauwakilisha Mkoa wa Morogoro kwenye michuano hiyo inayoshika nafasi ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania.

 

lfahamike Japhat Makao anamiliki shule kadhaa mkoani Morogoro zinazojulikana kwa jina la Fountain Gate School.

              


 

 .

 

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...