Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, October 5, 2025

USITANGULIZE H0FU KWENYE JAMBO LOLOTE BALI TANGULIZA DHAMIRA HUKU TUKIMUWEKA MUNGU MBELE,

 


Ndege na wanyama wamefanyiwa ukatili uliowaadhiri watoto ambao waliwategemea mama zao hao kwa asiimia 100.

WAEBRANIA 11,1

“Basi lmani ni kuwa na hakika ya Mambo ya tarajiwayo,ni bayana ya Mambo yasiyoonekana”Hili ndilo neno letu la Jumapili ya Leo Octobar 5,

                UCHAMBUZI WA UJUMBE,

Nimechagua neno hilo la Mungu kufuatia baadhi ya watu kutanguliza hofu kwenye jambo wanalotarajia kulifanya badara ya kutanguliza dhamira huku wakimtegemea Mungu,

Baadhi ya viongozi wetu wa dini wanatufundisha kwamba maneno yanaumba,wakiwa na maana kwamba ukijitabiia dhiki utapata kwei  na ukijitabilia utajiri wa haki utaupata kweli. Nieleweke hapa si zungumzii utajiri wa dhuruma ya aina yoyote kwa sababu matajiri wa aina hiyo kamwe hawawezi kuuridhi ufalme wa Mungu,

Mimi ni shuhuda wa ujumbe huo wa Mungu,kwenye maisha yangu siku zote ninapofanya jambo langu lolote huwa natanguliza dhamira huku nikimtanguliza Mungu mbele nikiondoa hofu na kumuweka shetani kando,

Niwe mkwei si kila jambo nilifanikiwa ra hasha mengine niliferi lakini watu wangu wa karibu wenye mapenzi mema na mafanikio yangu wakiwemo  wangu walinitia moyo kwenye anguko hilo wakisema,

” kwenye jambo hili baba ulipambana sana lakini bahati haikuwa upande”kali hiyo ilinipafaraja na kuondoa machungu ya anguko hilo,

                        ONYO

Kwenye jambo lolote unalokusudia kulifanya usiweke dhuruma yaina yoyote,ukifanya hivyo  Mwenyezi Mungu atakutenga lakini ukifanya kwa haki Mungu atakufanyia wepesi kwenye kila gumu utakalokumbana nalo,

Wengi tunaferi kwa sababu hiyo ya dhuruma mfano kuwadhurumu haki zao watumishi wako,wanaokusaidia kazi au kununua kitu cha wizi kikusaidie kwenye jambo hilo unalofanya,

Mfano umemdhurumu Mjane Nyumba au kiwanja chake,chozi lake litageuka mafuriko ya kusomba mafanikio yako ya Duniani na Ahera,

Mfano mwinngine utakuta mama  wa familia unamdhurumu Mshahara mfanyakazi wake wa kazi za ndani, Maarufu Yaya au ‘House Girl’,

 Masikini ya Mungu mtoto wawatu katoka kijijini kwao kaja kwako kukulelea watoto wako huku akichezea kinyesi  kwa kufua nguo zao mara kwa mara,

Hakika chozi la House Girl huyo haliwezi kukuacha salama,

Kwa leo naishia hapa mwenye masikio na asikie asiye na masikio [……]

Shekidele sina hatia nakukumbusha na kuikumbusha pia nafsi yangu, Mungu akipenda tukutane jumapili ijayo kwa somo Lingine.                  

 

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...