Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, September 30, 2025

BARTHDAY YA NYOTA WA TAIFA STARS YAFANA,








 

Na Dustan Shekidele, Morogoro,

SHEREHE ya Kumbizi ya Siku ya kuzaliwa’Happy Birthday’ ya Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’imefana vilivyo baada ya walikwa kula na Kunywa Mwanzo Mwisho,

 

Nyota huyo si Mwingine ni Peter Tino aliyefunga bao pekee Jijini Ndola  Zambia Mwaka 1979 dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia ‘Kipolopo’

 

Bao hilo Pekee lililowanyamazisha Wazambia kwenye uwanja wao wa Nyumbani liliipa tiketi Tanzania ya kufudhu kwa mara ya kwanza  mashindano ya Mataifa ya Afrika yaliofanyika mwaka 1980  nchini Nigeria.

 

Peter Tino Mkazi wa Kigurunyembe Mkoani Morogoro jumapili iliyopita Septemba 28 alifanya sherehe yake ya kumbukizi ya kuzaliwa nyumbani kwa Mpwa wake Mtaa Maarufu wa Tubuyu B Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro, lfahamike Mtaa huyo wa Tubuyu wanaishi Mastaa wengi akiwemo Mzee Ramadhan Kichuya baba mzazi wa Shiza Kichuya Staa mwingine ni anayeishi mtaa huo ni Emanuel Kimbawala katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro,

 

Katika sherehe hiyo iliyoratibiwa kisomi kundi a wageni waalikwa wali ‘Enjoy’ kwenye vipengere vyote vitatu muhimu Kula,Kunywa na Kucheza.

 

Kabla ya kukata keki ukumbi mzima ulisimama na kumfanyia maombi Maalum ‘Streka’ huyo wa zamani wa timu ya Pan Afrikam ya Dar es salaam.

 

Baada ya maombia hayo Mshambuliaji huyo aligongewa muziki wa zamani na kulisakata Rhumba huku akimwagiwa bia kichwani ikiwa ni ishara ya kuadhimisha siku yake hiyo muhimu kwenye maisha yake.

Akizungumza na Mtandao huu  Tino alisema

” Leo nimetimiza Miaka 66 namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kunijaia kufika umri huu mkubwa kuna wengi walitamani kufika umri huu lakini ahawakufanikiwa”

 

Kipengele cha Mwisho kwenye sherehe waalikwa wakimshika Mkonono wa pongezi shujaa huyo wa Tanzania kwenye medani ya Soka Mtandao huu Unamuomba Mwenyezi Mungu azidi kumlinda shujaa wetu huyo aliyemwaga jasho lake uwanjani kuipigania nchi yake ya Tanzania,


 

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...