Babu kichuya akikagua daraja hilo jana mchana
Jengo linaloonekana kwa mbali lenye paa la vigae vyekundu ni eneo a Stesheni ya Morogoro
Babu Kichuya kushoto akiwa na Mwandishi wa habari hizi wakijiandaa kuelekea darajani
.......Safari ya kuelekea darajani akianza
Na Dustan Shekidele,Morogoro,
Mzee Ibrahim Mohamed Mangwende Almaarufu ‘Babu Kichuya’ amekagua ujenzi wa daraja la Relwe Maarufu daraja la Ng’ombe lililopo mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoania hapa.
Jana majira ya mchana Mzee huyo akiwa na Mwandishi wa habari hizi wakitumia usafiri wao wa baiskeri walitinga kwenye daraja hilo na kushuhudia Mkandarasi akiwa Site akiendelea na kazi kwa kasi ya kuridhisha.
Akizungumza na Mtandao huu mara baada ya kukagua daraja hilo ambalo lipo mto Morogoro mzee huyo alisema.
” Mimi ni mwananchi wa Morogoro niiyekulia Mji Mpya nimeamua kuja kukagua ujenzi wa daraja letu ama kwa hakika nimefurahishwa na kazi nzuri inayondelea kwenye mradi huu,kipekee naipongeza serikali yetu kwa ujenzi wa daraja hili litakalofungua barabara hii muhimu ya kuelekea kichangani”alisema babu kichuya ambaye ni fundi bomba mstaafu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mkoa wa Morogoro’MORUWASA’
Ifahamike Mzee huyo mmoja wa wamjuu zake ni mchezaji nyota wa Maafande wa JKT Tanzania Shiza Ramadhan Kichuya aliyewahi kutamba na Simba kabla ya kutimkia Misri kucheza Soka la Kulipwa.
KWA NINI LIITWE DARAJA LA NG’OMBE?
Miaka ya nyumba wakati Mwandishi wa habari hizi anasoma shule ya Msingi Kaloleni iliyopo jirani kabisa na daraja hilo,walishuhudia Makundi ya Ng’ombe yakivushwa kwenye daraja hilo dogo linaloonekana pichani yakitokea Machinjio ya Morogoro yaliyopo Mtawara wakipelekwa Stesheni ya Morogoro inayoonekana kwa mbali yenye vigae vyekundu.
Baada ya kufika stesheni hapo Ng’ombe hao hupakiwa kwenye Treni ya Mizigo na kupelekwa Machinjio ya Ng’ombe Vingunguti Jijini Dar es salaam.
Takribani miezi 5 iliyopita daraja hilo lilikatika na kukata mawasiliano ya pande mbili, huku Mtandao huu ukiwa wa kwanza kuripoti habari hiyo.
Baadae Mkandarasi wa daraja hilo alijenga daraja a muda linaloonekana pichani sambamba na Mkandarasi huyo kuanza kwa kwa kasi ujezi wa daraja kubwa huku akiwa kwenye hatua za mwisho za kulikamilisha kama.








No comments:
Post a Comment