Mwandishi wa Mtandao huu akionyesha mavazi hayo ya kiume.
Ujumbe wa neno la Mungu jumapili ya Leo Septemba 14,kupitia Maandiko Matakatifu kutoka kumbumbu ya Torati 22 Mstari 5.
“ Mwanamke asivae Mavazi yampasayo Mwanamume wala Mwanamume asivae mavazi ya Mwanamke kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana Mungu wako”
UCHAMBUZI WA NENO HILO.
Kwa kipindi kirefu sasa baadhi ya wanawake wanavaa nguo za kiume Suluari, Kaptura, Mashati na kofia [Kapero] wanadunda mitaani bila wasi wasi wowote.
Wengine wanafika mbali zaidi wanaingia kanisani wakiwa na nguo hizo za kiume zilizo wabana makalio.nafurai makanisa mengi yamepiga marufuku wanawake kuingia kanisa na mavazi hayo.
Kama hiyo haitoshi wengine wanakwenda ukweli wakiwa wametinga mavazi hayo ya kiume, siku zote mavazi yanamdharaulisha mtu na mavazi hayo hayo yanamuheshimisha mtu aliyevaa mavazi ya staha.’Heshima’
Wakishatoka huko ukweli kama familia husika ina hofu na Mungu moja kwa moja vikao vya kumjadili mkwe wao huyo vitaanza chapu kwa haraka.
Niwapongeze wanaume binafsi sijashuhudia Mwanaume amevaa nguo ya kike Mfano kavaa gauni anaendesha boda boda lakini nimeshuhudia Mwanamke kavaa suluari anaendesha boda boda.
Pia nimeshuhudia baadhi ya wanaume wakijipodoa kama wanawake,ingawa Kwenye maandiko hayo ya Mungu swala la Mwanaume kujipodoa halipo lakini naamini hilo nalo ni chukizo kwa Mungu.
Mara nyingi wanaojipodoa ni wale ‘kuku watamu. Mtoto Si Riziki’ Makaka Poa a.k.a Mashoga. Majina yote hayo mabaya ni yao.

No comments:
Post a Comment