Na Dunstan Shekidele Mogoro.
JANA Septemba 7 dunia ilishuhudia tukio adhimu la Mwezi kufunikwa na wingu kwa muda wa masaa 5.
Tukio hilo lilianza saa 1 usiku mpaka saa 5 usiku huku Mwandishi wa habari hizi kulifuatilia tukio hilo Mwanzo Mwisho kwa muda wote wa masaa matano akiwa nje ya nyumba akipiga picha tukio hilo akitumia kamera ya kisasa yenye uwezo wa kupiga picha umbari mrefu.
Katika hali ya kuondoa mashaka na makando kando ya tukio hilo, Mpiga picha huyo aliamua kuseti kamera yake tarehe na saa hivyo kila picha iliyopigwa ilionyesha tarehe muda [saa].
Baada ya wingu hilo kuukamata Mwezi huo kuanzia saa 1 mpaka saa 3,ilipotimu saa 4 usiku wingu hilo taratibu limeanza kuachia Mwezi kama vile Nyoka anayejivua gamba la zamani na kubakia na jipya.
Muda huo wa saa 4 Mpiga picha huyo Dunstan Shekidele alipiga picha kila dakika mpaka mwezi huo ulipoachiwa saa 5,00 usiku, nimeamua kurusha baadhi ya picha hizo kuanzia saa 4 na dakika 34 mpaka Mwezi huo ulipoachiwa saa 5.00 usiku angaia saa kwenye kila picha.
lfahamike Mwaka mkubwa unasiku 366 na mdogo unasiku 365 hivyo kwenye moja ya siku hizo tukio hili hutoke mara nyingine hutokea mchana kwa Jua kufunikwa na Mwezi.
lkitokea mchana huwa na mvuto zaidi kwa sababu ya uwepo wa giza zito kufuatia Nuru kupotea kwa muda baada ya Jua kufunikwa na.
Baada ya kazi hiyo kutamatika Mpiga picha huyo alizima kamera yake kisha akaingia kwenye kiota chake kulala.
‘Mwacheni Mungu aitwe Mungu’
No comments:
Post a Comment