Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, September 25, 2025

MGANGA AIBUKA KIDEDEA MBIO ZA MAGARI AFRIKA






Mshindi  Lasin Nasser akionyesha kidole kmoja kama ishara ya kuwa mshindi wa kwanza Afrika





 


Na Dustan Shekidele,Morogoro.

RAIA wa Uganda Nasin Nasser ameibuka kidedea mashindano ya  Magari Afrika alofanyika wiki iliyopita Mkoani hapa.

 

Mashindano hayo yalioshirikisha madereva 23 kutoka nchi mbali mbali barani Afrika yalianza kutimua vumbi September 19 na kutamatika September 21 na mganda huo kuibuka mshindi wa kwanza.

Mara baada ya dereva huyo na msomaramani wake kukabidhi vikombe na Mgeni rasm Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Mussa Kilakala.kundi a Waganda waliofunga safari kutoka Uganda na usafiri wao wa basi lililoandikwa .Friends’  walimvania dereva huyo na kumnyanyua juu huku wakipeperusha bedera ya nchi yao.

 

Ifahamike mashindao hayo yalikuwa na vipengere tofauti ambapo kipengere cha kwanza Mganda huyo umeibuka mshindi,badae Mtandao huu utarusha picha za washindi wengine akiwemo mshindi wa Jumla.

 

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao ya chini ya kapeti miongoni mwa matukio hayo ni dereva pekee wakike Mchanga mkazi wa Morogoro kunyakua nafasi ya 8 na kukabidhiwa zawadi.

 

Matukio mengine ni vituko vya Msanii nchini Mwijangu ambaye naye aikuwa kivutio kwenye mashindano hayo.

Kwa habari zote hizo  nakusihi uendelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...